Chuo Kikuu cha Kenyatta

(Elekezwa kutoka Kenyatta University)

Chuo Kikuu cha Kenyatta (kwa Kiingereza: Kenyatta University) kilichoko katika mji wa Nairobi, Kenya, ndicho chuo kikuu cha umma cha pili kwa ukubwa nchini Kenya (baada ya Chuo Kikuu cha Nairobi). Chuo Kikuu cha Kenyatta kimo katika eneo la Kahawa, umbali wa kilomita 20 (maili 12) kutoka mji wa Nairobi, katika barabara kuu ya kuelekea mji wa Thika.

Kenyatta University
Chuo Kikuu cha Kenyatta
Kimeanzishwa1985
ChanselaDr. Harris Mule
MahaliNairobi, Kenya
Kampasimain campus, along Thika Road
Parklands campus, located in Nairobi's Parlands suburb
Ruiru campus, located in Ruiru, a satellite town of Nairobi
Kitui campus
Tovutihttp://www.ku.ac.ke/

Historia

hariri
 
Mlango wa kuingia Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Chuo Kikuu cha Kenyatta kina historia yake kutoka kwa kambi la wanjeshi wa ukoloni kwa jina Templer Barracks ambapo mnamo mwaka wa 1965 Templer Barracks ilibadlishwa na kuwa Kenyatta University College, yaani taasisi ya mafunzo ya mwalimu wa shule za msingi.Baadaye,ilipata muinuko na kuwa sehemu ya [Chuo Kikuu cha Nairobi] katika mwaka wa 1970.Mnamo mwaka wa 1985 chuo hiki kilifanywa kiweze kujisimamia ana aliyekuwa rais wa jamhuri ya [Kenya], [Daniel arap Moi] kisha kikaitwa Chuo Kikuu cha Kenyatta. Hii ilifanyika baada ya mswada kupitishwa bungeni kulingana na katiba ya Kenya.

Wahitimu wake wengi walikuwa kutoka daraja la elimu, kukifanya chuo hiki kuongoza katika masomo ya daraja ya elimu. Jinsi wakati ulivyozidi kusonga chuo hiki kiliendelea kupanuka na kuanzisha masomo katika taaluma na daraja nyinginezo.

Leo chuo kikuu kina shule zifuatazo[1]:

  • Shule ya Kilimo na maendeleo ya viwanda
  • Shule ya Sayansi za Kibinadamu
  • Shule ya Biashara (ina idara kuu tatu)
    (a) Idara ya Akaunti na Fedha
    (b) Idara ya Sayansi ya Usimamizi
    (c) Idara ya Usimamizi wa Biashara
    • Shule ya Kilimo na maendeleo ya viwanda
    • Shule ya Sayansi za Kibinadamu
    • Shule ya Biashara (ina idara kuu tatu)

(a) Idara ya Akaunti na Fedha (b) Idara ya Sayansi ya Usimamizi (c) Idara ya usimamizi wa biashara

    • Shule ya Biashara Archived 16 Agosti 2018 at the Wayback Machine.-inatoa masomo ya biashara kwa shule nyingine hasa ile ya Elimu na wale wanafunzi wanaosomea B.Ed (Sanaa). Hata hivyo msingi ni kiini kwa wanafunzi kuchukua B.Com na MBA.) wana maeneo sita idara tatu ambapo wanaweza kufuatilia baada ya kumaliza mwaka wa pili.

Chini ya Idara ya Hesabu na Fedha, wanafunzi wanaweza fuatilia katika ha Hesabu au Fedha. Chini ya Idara ya Usimamizi wa Sayansi, wanafunzi wanaweza kufuatilia katika Usimamizi aidha Sayansi au Actuarial Science. Chini ya Idara ya Biashara Utawala, wanafunzi wanaweza kufuatilia katika aidha Marketing au Human Resource Management. Mkuu wa sasa wa shule hii ni Profesa Chege.

Hali kwa sasa

hariri

Chuo kikuu kina mbinu mbalimbali za kufunza, kuanzia kusoma kutoka mbali(open learning), kusoma kutumia technolojia, masomo ya likizo, masomo ya muda na ya kila wakati, hili limegeuza taasisi kuwa chuo kikuu cha pili kwa ukubwa nchini Kenya. Mwaka wa 1997 kilikuwa na wanafunzi 8,000,lakini hivi sasa(2009) kina wanafunzi takriban elfu ishirini na wanne.

Mikakati ya sasa

hariri

Chuo Kikuu cha Kenyatta kimeanzisha mikakati ya upanuzi wa haraka kwa lengo la kukifanya chuo kuwa daraja moja na vyuo vikuu duniani na pia kupanua kozi kinazotoa. Ili kuifanikisha hatua hii,chuo kikuu kimeunda miundo msingi ya technologia ya ICT mpya ambayo ni pamoja na mtandao wa chuo kwa msingi wa teknolojia ya fiber optic; kasi ya internti ya gigabit kwa mtandao kwa wanafunzi na wafanyakazi wote kuwezesha upatikanaji wa intaneti na huduma ya habari kwa chuo .

Pia imejenga nyumba ya kuhifadhi maiti pamoja na kuanzisha masomo ya upasuaji na utabibu. Chuo kikuu pia kinajenga maabara zaidi na kufufua miradi ambayo ilimekuwa imesimama kwa miaka, ikiwa ni pamoja na kukamilisha ukumbi wa mafunzo ya sanaa. Juhudi zaidi pia zinawekwa kwa mtiririko wa habari kwa kuwekeza katika mitambo ya mawasiliano na kupata maoni kutoka kwa wanafunzi, hii ni pamoja na redio ya jamii, ambayo inatolewa kupitia kwa tovuti kwa matawi yote ya chuo nchini.

Hakika, Ukumbi wa mafunzo ya Sanaa tayari umekamalika (awamu ya 1 na 2) na maabara ya Sayansi inazidi kukamilishwa. Maendeleo mengine ni kukamilishwa kwa jumba kubwa la ghorofa tatu lenye viti mia nane linalotumiwa kama maabara ya tarakilishi na lina tarakilishi mpya zilizoundwa na kampuni ya Dell.

Makampasi

hariri

Chuo kikuu cha Kenyatta inaendelea kupanuka na kimefungua matawi mengine fauka ya tawi lake kuu. Matawi hayo ni pamoja na:

Chuo cha Parklands

hariri

Tawi hili liko Parklands karibu na mji wa Nairobi: Hili linatoa masomo ya biashara na masomo ya Tecknolojia.Masomo haya ni ya kiwango cha shahada na shahada za Uzamili. Tawi hili pia hutoa masomo ya sheria . (Bachelors of Law)

Tawi la Ruiru

hariri

Tawi hili liko katika mji wa Ruiru, kilomita tano kutoka tawi kuu.Kwa jumla ni ugani wa tawi kuu.

Tawi hili halitoi masomo mbalimbali kamili kama vile ilivyo katika tawi kuu.

Tawi la Mombasa

hariri

Liko mjini Mombasa katika pwani ya Kenya. Lilianza kazi Mei 2007.

Tawi la Kitui

hariri

Hili lilianza operesheni mnamo Oktoba mwaka wa 2007.

Usimamizi

hariri

Chansela wa sasa ni Dr Harris Mule na Makamu wa Chansela ni Prof Olive Mugenda, ambaye ni Makamu wa kwanza wa kike wa chuo kikuu cha umma nchini Kenya.Chini ya Makamu wa Chansela, kuna manaibu Makamu wa Chansela watatu na Wasajili watatu.

Makamu wa Chansela

hariri
  • Makamu wa Chansela - Prof Olive mugenda

Manaibu wa Makamu wa Chansela

hariri
  • Naibu Makamu wa Chansela wa Masomo - Prof Mwakio P. Tole (Kaimu)
  • Naibu Makamu wa Chansela wa Usimamizi - Prof G. Muluvi
  • Naibu Makamu wa Chansela wa Fedha, Mipango na Maendeleo - Prof D. Mugendi

Wasajili

hariri
  • Msajili wa Masomo - Daktari Gabriel Katana
  • Msajili wa Usimamizi- Profesa Godfrey Mse
  • Msajili wa Fedha, Mipango na Maendeleo- Daktari Nelson Karagu

Mkuu wa Wanafunzi

hariri
  • Daktari.Edwin Gimonde

Maandamano ya 29 Machi 2009

hariri

Tarehe ishirini na tisa mwezi wa Machi mwaka wa 2009, sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kenyatta waligoma huku wakiiba mali na kuchoma majengo katika tawi kuu na tawi ndogo la [Ruiru]. Wanafunzi walikuwa wakiandamana kupinga kufukuzwa kwa viongozi wao na Makamu wa Chansela, Profesa Olive Mugenda.Miongoni mwa masuala mengine ilikuwa kuanzishwa kwa sare za shule, na kutolewa kwa huduma ya uchukuzi ya wanafunzi wakaazi tawi la Ruiru. Majengo yaliyochomwa ni pamoja na malazi ya Nyayo , maabara ya tarakilishi,afisi za viongozi wa wanafunzi na jumba la Harambee. Polisi wa kupambana na ghasia waliotumwa na Olive Mugenda walishutumiwa kuwa walitumia nguvu ya kupindukia ambao ulisababisha vifo vya wanafunzi wawili na majeraha makubwa kwa wanafunzi kumi na wawili. Pia kulikuwa na madai ya ubakaji ya wanafunzi wa kike na polisi hasa katika jumba la malazi la Ngong. Chuo Kikuu kilifungwa kwa muda usiojulikana baada ya ghasia hizo.[2]

Chuo Kikuu kilifunguliwa kama ifuatavyo

  • Vikundi vya 2006 na miakaya ya awali: Jumapili, 27 Septemba 2009
  • Vikundi vya 2007 na 2008: Jumatatu 28 Septemba 2009
  • mafunzo kwa wanafunzi wa kuendelea: Jumanne 29 Septemba 2009

Marejeo

hariri
  1. "Unaweza Kuangalia mashule haya kwa tovuti ya Kenyatta University". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-02. Iliwekwa mnamo 2018-08-20.
  2. [1]

Viungo vya nje

hariri
 
Wanafunzi katika stesheni ya KUFM

]

  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Kenyatta kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.