Khanyisa Patricia Jaceni (alizaliwa Oktoba 3, 1995)[1], ni mtu wa vyombo vya habari na msanii akijulikana kama Khanyisa,[2] alipata umaarufu wake zaidi kupitia akaunti yake ya TikTok na baadae kuanza safari yake ya muziki mwishoni mwa mwaka 2021[3].

Akiwa kama mtumiaji mashuhuri wa TikTok[4] amejizolea zaidi ya wafuasi millioni 1.7 na video zake hutazamwa na watu zaidi ya millioni 37, huku akiwa na msemo wake mashuhuri wa BOTTOM LINE!![5], ni miongoni mwa waundaji wa maudhui wachache waliothibitishwa na TikTok.

Alianza safari yake ya muziki mnamo mwaka 2021, alitafutwa na nguli wa muziki wa Amapiano, Mr JazziQ, wote kwa pamoja wakaja na kichwa kiitwacho 'Ungangi Bambi'. Wote pia wakaenda kuachia kilicho tokea katika nyimbo yake Khanyisa na Lady Du, jina la nyimbo likiitwa "Bheka Mina Ngedwa", na kupewa tuzo ya mwanamuziki bora chipukizi wa mziki wa 'Amapiano'.[6] Baadae aliachia EP yake mnamo Novemba 2021 ikiitwa 'Soft'.[7]

Marejeo

hariri
  1. "Jaceni's Covid-19 lockdown blues ushered in era of transformation". Sunday World (kwa Kiingereza). 2021-11-09. Iliwekwa mnamo 2022-04-24.
  2. "Lovablevibes | South Africa | Nigeria | Africa | WORLD | Entertainment & News". Lovablevibes | South Africa | Nigeria | Africa | WORLD | Entertainment & News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-04-24.
  3. https://www.kaya959.co.za/elite-nites-with-khanyisa-jaceni/
  4. https://sundayworld.co.za/shwashwi/celebrity-news/entertainment/jacenis-covid-19-lockdown-blues-ushered-in-era-of-transformation/
  5. Jamal Grootboom. "TikTok star Khanyisa Jaceni is ready to take amapiano by storm". www.iol.co.za (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-24.
  6. "TikTok star Khanyisa Jaceni plans to showcase 'soft' amapiano on new EP". The South African (kwa Kiingereza). 2021-11-21. Iliwekwa mnamo 2022-04-24.
  7. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-26. Iliwekwa mnamo 2022-04-24.