Kidingapopo kwa Kiingereza (Dengue) ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya kidingapopo. Watu hupata virusi vya kidingapopo kutoka kwa mbu. Homa ya kidingapopo pia inaitwa homa ya kukatika mifupa, kwa sababu inaweza kusababisha maumivu mengi ambayo watu huhisi kama mifupa inataka kuvunjika.

Uenezi wa kidingapopo duniani
Uenezi wa kidingapopo duniani

Watu wengi wenye homa ya kidingapopo wanaweza kujisikia vyema tu kwa kunywa maji vya kutosha. Hata hivyo, idadi ndogo ya watu hupata homa ya kidingapopo ya hemorrhagic. kuna dharura ya matibabu na inaweza kuua mtu kama hatopata matibabu.

Hakuna chanjo ambayo inaweza kuwazuia watu kupata virusi vya kidingapopo. Pia hakuna matibabu au tiba ya homa ya kidingapopo. Madaktari wanaweza tu kutoa "huduma ya kukuangalizia," ambayo ina maana kwamba wanaweza tu kutibu dalili za kidingapopo.

Tangu miaka ya 1960, watu wengi zaidi wamepata homa ya kidingapopo. Tangu Vita Kuu ya II, kidingapopo imekuwa tatizo duniani kote. Ni kawaida katika nchi zaidi ya 110. Kila mwaka, watu milioni 50 na milioni 100 hupata homa ya kidingapopo.


Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kidingapopo kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.