Homa ni hali ya wanyama kuwa na halijoto ya mwili juu ya halijoto ya kawaida (37 °C katika mamalia).

Kipimajoto ni kifaa cha kupimia homa.

Halijoto ya kawaida ya mwanadamu ni kati ya 36.6 na 37 sentigredi za Selsiasi ikipimwa chini ya ulimi.

Maelezo

hariri

Mara nyingi homa husababishwa na ugonjwa; ni dalili ya kwamba kingamwili inapambana na vijidudu au vijimea vinavyosababisha ugonjwa fulani.

Homa si ugonjwa wenyewe bali dalili ya magonjwa mbalimbali. Katika lugha ya kila siku malaria mara nyingi huitwa "homa" ingawa kupanda kwa halijoto ya mwili wakati wa malaria ni dalili ya mapambano dhidi ya vijidudu vya plasmodium tu. Katika Kenya "homa" hutumiwa kumaanisha mafua, mafua ya kawaida hasa.

Hadi kiwango cha sentigredi 39 homa si hatari sana, lakini ikipanda juu ya 40°C inaanza kudhoofisha umbile la mtu hadi kuwa hatari yenyewe.

Inashauriwa kumwona daktari na kutumia madawa ya kutuliza homa. Kufikia 42°C homa inaweza kumwua mtu kwa kusababisha uharibifu wa viungo vya ndani vya mwili.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Homa kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.