Nex Benedict
(Elekezwa kutoka Kifo cha Nex Benedict)
Nex Benedict (11 Januari 2008 – 8 Februari 2024)[1] alikuwa mwanafunzi wa shule ya upili nchini Marekani mwenye umri wa miaka 16 asiyejibainisha kwa jinsia (non-binary).
Alifariki siku moja baada ya kushiriki katika ugomvi wa kimwili kwenye choo cha wasichana katika shule yao. [2] Wachunguzi walibaini baadaye kuwa kifo cha Benedict kilitokana na kujiua baada ya kuzidisha dawa za Prozac na Benadryl.[3] Tukio hilo lilivuta hisia za vyombo vya habari kitaifa kwani baadhi ya watu wamedai kuwa kifo cha Benedict kilisababishwa na sera zinazopinga ushoga katika jimbo la Oklahoma walikotoka.
Marejeo
hariri- ↑ "Non-binary student Nex Benedict who died after bathroom assault was a 'shining light'". The Independent (kwa Kiingereza). 2024-02-22. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ "Death of Nex Benedict", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-09-16, iliwekwa mnamo 2024-09-19
- ↑ "President Biden releases statement on Nex Benedict's cause of death". 2 News Oklahoma KJRH Tulsa (kwa Kiingereza). 2024-03-13. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nex Benedict kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |