Ndubwi
(Elekezwa kutoka Kiluwiluwi (amfibia))
Ndubwi (pia: kiluwiluwi) ni ngazi ya kwanza katika metamofosi ya chura na amfibia wengine ni kama utoto wao.
Vyura hutega mayai katika maji na ndubwi anatoka. Anapumua kwa matamvua na mwanzoni hana miguu bali mapezi kama samaki na mkia. Ndubwi wengi wakiwa kwenye maji wanakula majani au mwani hata kama baadaye chura mzima atakula wanyama wengine.
Baada ya muda ndubwi anakuza miguu minne na mapafu. Utumbo unabadilika na kujiandaa kwa chakula kipya kinachopatikana kwenye nchi kavu. Umbo linaelekea kufanana zaidi na zaidi na chura mzima.
Kipindi hiki cha utoto kwenye maji kinadumu kati ya wiki tatu hadi miaka miwili kutegemeana na spishi za chura. Mara nyingi ni kama wiki 10 - 15.
Mkia unapotea ama kwenye maji au baada ya kutoka nje.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ndubwi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ndubwi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |