Mapafu ni sehemu ya mwili inayoingiza oksijeni mwilini na kuituma kwenye seli za mwili. Ni ogani kuu ya mfumo wa upumuaji, yaani tendo la kupumua.

Mapafu pamoja na moyo ya mwanadamu.
Kazi ya mapafu
(Njia ya hewa inaanza mdomoni na puani; misuli ya kiwambo tumboni (njano-nyekundu) zinajikaza au kulegeza na hivyo kupanua au kupunguza ukubwa wa mapafu (buluu nyeupe/zambarau)
pafu la kushoto la binadamu

Ni kawaida kwa wanyama wa faila ya chordata walio na uti wa mgongo na kupumua hewa.

Hutokea kwa jozi maana yake kuna mapafu mawili, si moja tu kama moyo.

Kuna pia samaki na konokono kadhaa wenye mapafu.

Mapafu huvuta hewa ndani ambamo oksijeni ya hewa inaingizwa katika damu na kupelekwa kwenda seli za mwili.

Ndani ya mapafu kuna viputo vidogo sana ambavyo ndio mwisho wa njia ya hewa kutoka nje. Damu inazunguka viputo hivi katika mishipa midogo inayotenganishwa na nafasi ya hewa kwa ngozi nyembamba sana. Oksijeni inaweza kupita kwenye ngozi na kuingia katika damu inapopokewa na seli za damu nyekundu.

Chordata walio wengi huwa na mapafu mawili.

Kuna wanyama wadogo wasio na mapafu. Wachache wanapokea oksijeni yote kupitia ngozi.

Njia nyingine ni wadudu walio na neli nyingi ndogo zinazoingiza hewa mwilini na kupokea oksijeni kupitia kuta za neli hizo.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mapafu kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.