"Kipi Sijasikia" ni wimbo uliotoka tarehe 15 Septemba, 2014 kutungwa na kuimbwa na msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Professor Jay. Katika wimbo, ameshirikishwa mwimbaji wa Bongo Flava - afisa mtendaji mkuu wa WCB, Diamond Platnumz. Wimbo umetayarishwa na P. Funk wa Bongo Records. Wiki ambayo wimbo huu umetoka, Jay alitoka nyimbo tatu kwa siku tatu mfululizo. Ya kwanza "Chafu Tatu", ya pili "Kipi Sijasikia" na ya tatu "Sauti ya Ghetto". Wimbo una madongo kibao dhidi ya wale wanaomsema vibaya maisha ya Jay. Video ya muziki huu imeongozwa na Adam Juma wa Next Level Production. Walionekana katika video ni pamoja na Rommy Jones, DJ Choka, P. Funk, Kulwa Kikumba (Dude) na wengine wengi. Jay anaimba kwa uchungu mno dhidi ya wenye visonoko na ngebe juu yake.[1]

“Kipi Sijasikia”
“Kipi Sijasikia” cover
Kava la Kipi Sijasikia
Single ya Professor Jay akiwa na Diamond Platnumz
Imetolewa 15 Septemba, 2014
Muundo Upakuzi wa kidijitali
Imerekodiwa 2014
Aina Hip hop
Urefu 4:05
Studio Bongo Records
Mtunzi Professor Jay
Mtayarishaji P. Funk
Mwenendo wa single za Professor Jay akiwa na Diamond Platnumz
"Chafu Tatu"
(2014)
"Kipi Sijasikia"
(2014)
"Sauti ya Ghetto"
(2014)
Kiwambo cha Kipi Sijasikia ikimuonesha Diamond Platnum aliyecheza kama wakili wa Jay katika video hii. Seti hii ilikuwa ya mahakamani.

Ubunifu pekee katika wimbo huu ni kwenye video. Inaanza anakamatwa, anapelekwa mahakani, anashinda na mwishoni anaonekana akiwa na marafiki zake wanakula raha za dunia kwa raha mustarehe kabisa licha ya magumu aliyopitia hapo awali.

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-09. Iliwekwa mnamo 2017-11-10.  "Professor Jay Ft Diamond- Kipi Sijasikia (GetMziki Exclusive)".

Viungo vya Nje hariri

Sijasikia Video katika YouTube