Kitenduli
Kitenduli mashavu-mekundu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea
Familia: Estrildidae (Ndege walio na mnasaba na mishigi)
Jenasi: Uraeginthus (Vitenduli na tunguhina)
Cabanis, 1851
Ngazi za chini

Spishi 3:

Vitenduli ni ndege wadogo wa jenasi Uraeginthus katika familia ya Estrildidae ambao wana rangi buluu. Kuna spishi mbili zingine kwa jenasi hii ambazo zinaitwa tunguhina na zina rangi kahawianyekundu, lakini wataalamu wengine wanaziweka katika jenasi Granatina. Vitenduli wanatokea Afrika chini ya Sahara tu. Hupenda kuwa karibu na makazi ya watu. Tago lao hutengenezwa na manyasi juu ya mti au ndani ya paa; limefunikika juu na mwingilio kando.

Spishi hariri

Picha hariri