Kituo cha sanaa cha Pakare Paye

Kituo cha sanaa cha Pakare Paye (Pakare Paye Arts Centre) ni mojawapo ya mipango ya marehemu mwanamuziki nguli wa Zimbabwe Oliver Mtukudzi [1] [2] [3] ambaye pia alijulikana kama Tuku. [4] [5] [6]

Kituo hicho cha sanaa kilifunguliwa mwaka wa 2004 tarehe 3 Oktoba na kinapatikana mji wa Norton ambao uko umbali wa kilomita 45 kutoka mji mkuu wa Harare. Mahali hapo hapo awali palitumika kama ghala.

Sifa kuu ya kituo ni pamoja na Kituo cha Mikutano cha Sam Mtukudzi kilichopewa jina la mtoto wake marehemu Sam (aliyefariki mwaka 2011 kwa ajali ya gari). Kuna mikahawa, nyumba za kulala wageni, ofisi, na pia jukwaa la wazi ambalo linaweza kuchukua watu 3,000. Ukumbi kuu ni viti 200. [7]

Marejeo

hariri
  1. "Tuku leaving Pakare Paye for the last time". 26 Januari 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-07. Iliwekwa mnamo 2022-03-19.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Tribute to an icon". 27 Januari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Chronicle, The. "Farewell humble giant". The Chronicle.
  4. newsday (31 Oktoba 2011). "Tuku, a serious business person".{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Tuku unveils free Sunday show at Pakare Paye". 5 Machi 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. H-Metro. "Pakare Paye's Valentine's gig without Tuku". H-Metro.
  7. Mail, The Sunday. "'Dzvamu Tsvamu' at Pakare Paye". The Sunday Mail.