Oliver Mtukudzi
Oliver "Tuku" Mtukudzi (Highfield, Harare, Zimbabwe, 22 Septemba 1952 - The Avenues Clinic, Harare, 23 Januari 2019) alikuwa mwanamuziki wa Kizimbabwe. Oliver ni miongoni mwa wanamuziki walio maarufu kwa muda mrefu sana katika nchi hiyo. Alianza shughuli za muziki kunako 1977 pale alipojiunga na bendi ya Wagon Wheels, ambayo pia alikuwemo na mwanamuziki wa zamani Thomas Mapfumo.
Oliver Mtukudzi | |
---|---|
| |
Jina Kamili | {{{jina kamili}}} |
Jina la kisanii | Oliver Mtukudzi |
Nchi | Zimbabwe |
Alizaliwa | 22 Septemba 1952 |
Alikufa | 23 Januari 2019 |
Aina ya muziki | Aina zote |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Miaka ya kazi | 1977-hadi leo |
Ala | Sauti Gitaa |
Kampuni | Putumayo World Music Tuku Music ZMC Sheer Sound |
Wimbo wa kwanza ulikuwa "Dzandimomotera" ulioheshimika sana, na hapo ndipo Tuku alipotoa albamu yake ya kwanza, nayo pia ilileta mafanikio makubwa kabisa. Mtukudzi nae pia ni mmoja wa wanakundi la Mahube, kundi la muziki la nchi za Afrika ya Kusini.
Oliver alikuwa baba wa watoto watano na babu wa wajukuu wawili, wawili hao pia ni wanamuziki. Alikuwa na dada zake wanne na kaka mmoja ambaye alimtangulia kufariki.
Alifurahia kuogelea katika bwawa lake la kuogelea (swimming pool) ambalo lina umbo la gitaa. Oliver alitoa zaidi ya albamu 40 na amepata kushinda tuzo nyingi mno na hata nyingine hawezi kuzikumbuka.
Nyimbo
haririAlbamu alizotoa
hariri- 1978 Ndipeiwo Zano (Re-released 2000)
- 1979 Chokwadi Chichabuda
- 1979 Muroi Ndiani?
- 1980 Africa (Re-released 2000)
- 1981 Shanje
- 1981 Pfambi
- 1982 Maungira
- 1982 Please Ndapota
- 1983 Nzara
- 1983 Oliver's Greatest Hits
- 1984 Hwema Handirase
- 1985 Mhaka
- 1986 Gona
- 1986 Zvauya Sei?
- 1987 Wawona
- 1988 Nyanga Yenzou
- 1988 Strange, Isn't It?
- 1988 Sugar Pie
- 1989 Grandpa Story
- 1990 Chikonzi
- 1990 Pss Pss Hallo!
- 1990 Shoko
- 1991 Mutorwa
- 1992 Rombe
- 1992 Rumbidzai Jehova
- 1992 Neria Soundtrack
- 1993 Son of Africa
- 1994 Ziwere MuKobenhavn
- 1995 Was My Child
- 1995 The Other Side: Live in Switzerland
- 1997 Ndega Zvangu (Re-released 2001)
- 1998 Dzangu Dziye
- 1999 Tuku Music
- 2000 Paivepo
- 2001 Neria
- 2001 Bvuma (Tolerance)
- 2002 Shanda sountrack
- 2002 Vhunze Moto
- 2003 Shanda
- 2003 Tsivo (Revenge)
- 2004 Greatest Hits Tuku Years
- 2004 Mtukudzi Collection 1991-1997
- 2004 Mtukudzi Collection 1984-1991
- 2005 Nhava
- 2006 Wonai
- 2007 Tsimba Itsoka
Filamu alizoshiriki
hariri- Jit (mwong. Michael Raeburn , [[1990]])
- Neria (mwong. Goodwin Mawuru, imetungwa na Tsitsi Dangarembga, [[1993]]). Mtukudzi ndiyo alikuwa nyota wa [[filamu]] na yeye ndiye aliyetengeneza nyimbo ya filamu.
- Shanda (mwong. John na Louise Riber, [[2002]], rev. [[2004]])
Tuzo
hariri- Tuzo ya KORA kwa ajili ya matayarisho mazuri ya nyimbo yake ya Ndakuwara mnamo mwaka wa [[2002]]
- Tuzo ya National Arts Merit (NAMA) mnamo mwaka wa [[2002 ]]na [[2004]]kama kundi bora la muziki/ mwanamuziki bora wa kiume
- Tuzo ya KORA kama mwanamuziki bora wa kiume wa [[Africa]] na tuzo ya Lifetime Achievement mnamo mwezi Agosti wa mwaka wa [[2003]]
- Tuzo ya Reel kama lugha bora ya Kiafrica mnamo wamaka wa [[2003]]
- An honorary degree from the University of Zimbabwe in Desemba [[2003]]
- Tuzo za M-Net Best kama nyimbo bora ya filamu mnamo [[1992]] kwa ajili ya [[filamu]] ya Neria.
Marejeo
hariri- Oliver Mtukudzi and the Black Spirits, Zimbabwe Music Guide
- Internet movie database
- Internet movie database
- Review of Shanda movie at Dandamutande
- Mtukudzi, Ringo expected for UK concerts, New Zimbabwe.com, 11 Oktoba 2006
- Oliver Mtukudzi:Biography, Sheer Sound
Viungo vya nje
hariri- Oliver Mtukudzi in the film business Ilihifadhiwa 30 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Biography Ilihifadhiwa 17 Oktoba 2016 kwenye Wayback Machine.
- Official Website Ilihifadhiwa 21 Februari 2008 kwenye Wayback Machine.