Kizima moto ni chombo kinachotoa kiowevu, gesi au dawa la unga vinavyozuia mwako na kuzima moto. Giligili ndani yake huntunzwa kwa shindikizo inatoka kwa mbio kama vali yake inafunguliwa.

Kizima moto chenye dawa la unga
Kizima moto chenye CO2 chazima TV inayowaka

Madawa ya pekee kwa aina za moto

hariri

Madawa ndani ya kizimamoto hutofautiana kulingana na aina ya moto inayotakiwa kuzimwa.

  • Maji hufaa kwa moto ya ubao, karatasi, makaa, vitambaa, matairi na aina kadhaa za plastiki kwa hiyo kwa moto ya kawaida katika nyumba pasipo na vifaa vikubwa vya umeme. Haifai kwa moto ya vifaa vya umeme au petroli na mafuta.
  • Moto za petroli, mafuta na aina nyingi za plastiki ni hatari kutumia maji kwa hiyo kuna madawa kama pofu, dawa la unga au kaboni dioksidi (CO2).

Siku hizi kuna aina nyingi za moto hasa viwandani au gatika ghala penye kemikali mbalimbali. Walinzi wa moto huwa na vifaa vya pekee kwa aina hizi za moto.

Katika ghala au penye mashine kuna pia mitambo ya kuzima moto yasiyobebwa lakini yametengenezwa mahali penye hatari yakiwaka otomatia kwa kutumia vifaa vya kupima joto, gesi n.k.