Vali au valvu (kutoka Kiingereza valve) ni kifaa kinachoruhusu kufungua, kufunga, kupunguza au kuongeza mwendo wa kimiminiko au gesi katika bomba au kifaa.

Vali ya tairi: upepo unasukumwa ndani kwa shinikizo kubwa (P2) lakini hauwezi kutoka maana shinikizo la ndani (P1) linaifunga.

Kuna aina nyingi za valvu, zikiwa pamoja na

  • bilula (tapu ya maji, koki) kwenye mwisho wa bomba la maji
  • vali ya tairi inayoruhusu kuingiza upepo ndani yake na kuzuia hewa ya ndani isitoke
  • vali ya kudhibiti kumiminika kwa fueli katika injini au kutolewa kwa hewa chafu kutoka injini