Kizizi cha kucheza cha watoto

Kizizi cha kucheza cha watoto ni aina ya samani ambamo mtoto mchanga au mdogo huwekwa ili kumzuia asijidhuru wakati mzazi wake au mlezi hayuko karibu.

Kizizi cha kucheza cha watoto cha mbao

Historia hariri

Kihistoria kizizi hiki kilikuwa kinajengwa kwa mbao kikiwa na muundo wa mraba na fito za mbao ili mtoto aweze kuona nje. Sakafu yake huwa na zulia laini ili kuzuia watoto kujiumiza. Ukuta wake huwa mrefu kuliko urefu wa mtoto, ili kuzuia watoto kuupanda na kupata majeraha; kizizi kinaweza pia kuwa na kifuniko cha muda kinachoweza kuondolewa.

Vizizi vya kisasa vya kisasa vina miundo ya aina mbalimbali na vinabebeka na mara nyingi hujengwa kwa chuma na plastiki na wavu, pande la plastiki au pande za nylon. Aina ya kitanda kidogo huweza kuwekwa juu ya kizizi kwa ajili ya mtoto kulala au kubadilishwa nguo. Aina nyingine huwa na mifuko ya pembeni, taa, kisanduku cha muziki.

Ni muhimu kuhakikisha kuwa kizizi wanachotumia watoto ni salama kwa mtoto. Hii ni muhimu hasa wakati kizizi kilichonunuliwa ni mtumba. Kizizi kisicho salama huweza kuanguka na hivyo kusababisha majeraha (au hata kifo) kwa mtoto. [1]

Marejeo hariri

  1. "B.C. infant dies in playpen under product recall". CBC News. 2007-08-20. Iliwekwa mnamo 2008-06-16. 

Viungo vya nje hariri