Wazazi

mlezi au mlezi wa watoto katika spishi zao
(Elekezwa kutoka Mzazi)

Wazazi ni wale waliofanya watoto wapatikane katika spishi yao.

Sanamu ya wazazi wawili na mtoto wao huko Bratislava, Slovakia.

Kwa wanadamu, mzazi ndiye mlezi wa mtoto. Inafaa sana uzazi uendelezwe na malezi hadi kumfanya mtoto akomae pande zote na kuwa mtu mzima, tena bora.

Mzazi wa kibiolojia ni mtu ambaye gamete yake imetoa mtoto, mzazi wa kiume kupitia manii, na mwanamke kupitia kijiyai. Wazazi hao, baba na mama, ni jamaa ya kwanza na kuchangia asilimia 50 ya maumbile ya mtoto.

Mwanamke, mbali ya kujifungua, anaweza kuwa mzazi kwa njia ya upasuaji pia, hasa pale ambapo ujauzito una matatizo .

Siku hizi inawezekana kuwa na wazazi wa kibiolojia zaidi ya wawili, pale ambapo mtoto anatengenezwa katika maabara. Jambo hilo linapohusu binadamu, wengine wanalipinga kwa kusema ni kinyume cha maumbile na cha hadhi ya utu, pamoja na kudai mimba nyingi ziangamie au kutunzwa katika jokofu.

Wazazi wengine wanaweza kuwa wazazi kwa kukubaliana, ambao huwalea watoto, lakini si kweli kwamba wanahusiana na mtoto kimaumbile.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wazazi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.