Kumar Sanu (pak Kedarnath Bhattacharya Bengali: কেদারনাথ ভট্টাচার্য alizaliwa 23 Septemba 1957 katika Kolkata, ni mwimbaji maarufu India katika Bollywood. Yeye ni mpokeaji wa tuzo la Padma Shri , moja ya tuzo muhimu India. Alishinda Tuzo la mwanamume mwimbaji bora katika nyimbo za filamu kwa miaka 5 mfululizo.

Kumar Sanu
Kumar Sanu

Maisha Yake ya Awali hariri

Baba yake Pashupati Bhattacharjee alikuwa muimbaji na mtunzi wa bora. Alimfunza Sanu kuwa mwimbaji na mchezaji wa tabla. Baada ya kupata shahada ya biashara kutoka Chuo Kikuu cha Calcutta, Sanu alianza kuimba hadharani mwaka wa 1979, Liimba katika maonyesho na ha na mikahawa iliyokuwa Calcutta. Aliunda mtindo wake wa kuimba baada ya mwimbaji maarufu wa sauti Kishore Kumar.Baadaye aliendeleza mtindo wake kuimba.

Kazi hariri

Mwaka wa 1987, mkurugenzi wa muziki na mwimbaji Jagjit Singh alimpa Sanu nafasi ya kuimba katika filamu ya Kihindi Aandhiyan. Sanu kisha alihamiaMumbai, ambapo Kalyanji-Anandji alimpa nafasi ya kuimba katika filamu Jaadugar. Kalyanji-Anandji alipendekeza k kubadili jina lake kutoka Kedar Nath Bhattacharya hadi Kumar Sanu kwa sababu ya upendeleo wa Bollywood na eneo hilo na kumpa umaarufu kutoka watazamaji wa Bengali.

Sanu ilianza kuimba nyimbo za filamu ya Jagjit Singh's , na akaenda kufanya kazi na wanamuziki wa kama Naushad, Ravindra Jain, Hridayanath Mangeshkar, Pt.RK Razdan, Kalyanji Anandji, USHA Khanna nk

Umaarufu wa Sanu ulikuja mwaka wa 1990, katika namna ya filamu Aashiqui. Wakurugenzi wa muziki Nadeem-Shravan alimeuhusu Sanu kuimba nyimbo zote isipokuwa wimbo mmoja. Sanu alipata mafanikio na usiku kucha. Nyimbo za Aashiqui zilizovuma ni pamoja na Sanson ki zaroorat hai jaise, Tu meri Zindagi hain, Nazar ke saamne, Jaane jigar jaaneman, Ab Tere Bin Hum na Lenge Jee Dheere, dheere se mein meri Zindagi aana. Alishinda mara ya kwanza ya rekodi yake ya miaka mitano mfululizo katika tuzo za Filmfare kama mwanamume mwimbaji bora katika nyimbo za filamu. Tuzo zake za FilmFare zilikuja baada ya nyimbo katika filamu ya Saajan (1991), Deewana (1992), Baazigar (1993), na [3] (1994).

Sanu mara nyingi alishirikiana naNadeem-Shravan. Baadhi ya nyimbo zao walizoshirikiana katika sinema ni kama Aashiqi (1990), Manta Ki Dil Tera (1991), Sadak (1991), Saajan (1991), Deewana (1992), Dil Ka Kya Qusoor (1992), Kal Ki Awaz ( 1992), Shreeman Aashique (1993), Salami (1993), Damini: Lightning (1993), dil mile (1994), Agni Sakshi (1996) Raja Hindustani (1996), Jeet (1996) Pardes (1997), miongoni mwa zingine.

Pamoja na Udit Narayanya kisasa, Sanu hupewa heshima kama mwenye sauti bora miongoni mwa waimbaji wa nyimbo za filamu nchini India. Katika Wasifu wake wa miongo ameweza kuimba pamoja na watunzi mbalimbali waliofanikiwa ambao ni RD Burman, Jatin-Lalit, Ismail Darbar, Laxmikant Pyarelal, Naushad, Kalyanji Anandji. Alkivunja Guinness Rekodi ya Dunia kwa kuimba nyimbo 28 katika siku moja mwaka wa 1993.

Nyimbo zake za karibuni zilizovuma ni pamoja na Humraaz, Yeh Dil Aapka Huwa (Pakistan), Karz, Dil Ka Rishta, Indian Babu, Ishq Vishk, Andaaz, Qayamat, Hungama na Footpath. Amegeuza biashara yake katika kutengeneza muziki wa filamu za Indian na pia hivi karibuni kama mtayarishaji wa filamu za Bollywood, Utthaan.

Hivi sasa, Sanu ako katika jopo la majaji katika Sony TV ya Waar Parriwar, Onyesho ambalo linahusisha kuleta pamoja gharana ya kuimba (familia ya waimbaji) anashiriki pamoja u na mwimbaji wenzake Sajan, na Jatin Pandit maarufu wa muziki wa duo Jatin-Lalit katika maamuzi Wakati huo huo, yeye pia ni mmoja wa majaji pamoja na mwimbaji wa Bollywood Shantanu Moitra mtunzi na mwimbwji kuoka zamani Usha Mangeshkar katika zee Bangla TV katika kipindi cha Sa Re Ga Ma Pa - Vishwa Sera.

Tuzo hariri

Filmfare hariri

Tuzo la Filfare la Mwanamume Mwimbaji Boura Zaidi katika Nyimbo za Filamu

Tuzo la Nyota wa Skrini hariri

Tuzo la Nyota wa Skrini la Mwanamume Mwimbaji Boura Zaidi katika Nyimbo za Filamu

Viungo vya nje hariri