Kolkata
Kolkata (pia: Kalkutta; Kibengali: কলকাতা Kalkāṭa) ni jiji kubwa katika mashariki ya Uhindi na mji mkuu wa jimbo la Bengali ya Magharibi.
Kolkata | |
Mahali pa mji wa Kolkata katika Uhindi | |
Majiranukta: 22°34′N 88°22′E / 22.567°N 88.367°E | |
Nchi | Uhindi |
---|
Mji ulikuwa mji mkuu wa Uhindi wa Kiingereza hadi 1911. Baada ya ugawaji wa Uhindi hali yake ilirudi nyuma kwa sababu ya ugawaji wa Bengali kwa jumla. Baadaye jina limekuwa mashuhuri tena kimataifa kutokana na kazi ya Mama Teresa aliyeishi hapa.