Kundi la kijeshi ni jeshi lisilo rasmi na wala si sehemu ya jeshi ambalo linatambulika na sheria za nchi husika.[1] Kwa mujibu wa uchunguzi juu ya historia ya makundi haya, wataalam wamebaini kuwa makundi haya yamekuwepo tangia mwaka 1934.[2]

Jeshi kuu la wapambanaji wa mstari wa mbele, Kamandi ya Edmonton, 1915 – kundi la jeshi la kizalendo lisilo na uhusiano rasmi na Jeshi la Taifa la Canada

Ingawa kifasili kundi la kijeshi huonekana si jeshi, kwa kawaida huwa sawa na jeshi la askari wa miguu wasio na zana nzito au vikosi maalum kwa mujibu wa nguvu, stadi (kama za uteguaji wa mabomu), mbinu (kama za mapambano ya msituni au kwenye miji), ukali wa mapambano na hata muundo wake wa kamandi.[3]

Tanbihi

hariri