Kuuza na kununua Hisa (Kenya)

Hisa zinazouzwa na kununuliwa nchini Kenya huwa ni za makampuni yaliyosajiliwa katika Soko la Hisa la Nairobi. Hivyo basi, wakati kampuni inaposajiliwa katika soko la hisa, asilimia yake fulani huuzwa kwa umma kama hisa. Mtu yeyote aliyenunua hisa za kampuni fulani huwa basi na haki ya kumiliki asilimia sambamba na hisa alizonunua ya kampuni hiyo. Pia, mtu huyu anaweza kuuzia mtu mwingine hisa hizi katika soko la hisa.

Broka katika soko la hisa la Nairobi

Kuajibika Kuuza na Kununua HisaEdit

Ili kuajibika kuuza na kununua hisa, wafaa kufungua akaunti na kampuni ya ubroka ambao watahitaji kadi chako cha kitambulisho. Ni vizuri pia kuwa na akaunti ya benki ili kurahisisha ubadilishanaji wa fedha kati yako na kmapuni ya ubroka unapo nunua na kuuza hisa.

Baada ya kufungua akaunti na broka, wao watakufungulia akaunti ya CDSC (Central Depository and Settlement Corporation) ambapo hisa ulizonazo pamoja na rekodi yako ya kuuza na kununua hisa zitarekodiwa. Sasa uko tayari kuanza kununua na kuuza hisa.

Kununua HisaEdit

Unapotaka kununua hisa, wafaa kueleza broka wako ni hisa za kampuni gani wataka kununua, wataka kuzinunua kwa bei gani kila hisa na wataka hisa ngapi. Baada ya kumpa mwelekezo huu, broka wako atatafuta anaye hisa unazohitajikatika bei ulilotaja au la chini zaidina kisha, atazinunua chini ya jina yako.

Ubadilishanaji huu wa fedha na hisa utarekodiwa katika CDSC huku hisa ulizonunua zikiwekwa chini ya akaunti yako ya CDSC na zikiondolewa kutoka kwa akaunti ya mmiliki wa hapo awali.

Kuuza HisaEdit

Unapotaka kuuza hisa, wafaa kuelezea broka wako ni hisa zipip wataka kuuza na kwa bei gani. Baada ya kumpa mwelekezo huu, broka wako atasajili hiza hizo katika soko ambapo aliyeridhika na bei ya hisa hizo atazinunua.

Ubadilishanaji huu wa fedha na hisa utarekodiwa katika CDSC huku hisa ulizouza zikitolewa chini ya akaunti yako ya CDSC na zikiwekwa katika akaunti ya aliyezinunua.

Angalia piaEdit

Viungo vya njeEdit