Kuuza na kununua hisa nchini Kenya
Hisa zinazouzwa na kununuliwa nchini Kenya huwa ni za kampuni zilizosajiliwa katika Soko la Hisa la Nairobi. Wakati kampuni inaposajiliwa katika soko hilo, asilimia yake fulani huuzwa kwa umma kama hisa. Mtu yeyote aliyenunua hisa za kampuni fulani huwa na haki ya kumiliki asilimia sambamba na hisa alizonunua ya kampuni hiyo. Pia, mtu huyu anaweza kuuzia mtu mwingine hisa hizi katika soko la hisa.
Kuwajibika kuuza na kununua hisa
haririIli kuwajibika kuuza na kununua hisa, inafaa kufungua akaunti na kampuni ya ubroka ambao watahitaji kadi chako cha kitambulisho. Ni vizuri pia kuwa na akaunti ya benki ili kurahisisha ubadilishanaji wa fedha kati yako na kmapuni ya ubroka unapo nunua na kuuza hisa.
Baada ya kufungua akaunti na broka, wao watakufungulia akaunti ya CDSC (Central Depository and Settlement Corporation) ambapo hisa ulizonazo pamoja na rekodi yako ya kuuza na kununua hisa zitarekodiwa. Sasa uko tayari kuanza kununua na kuuza hisa.
Kununua hisa
haririUnapotaka kununua hisa, wafaa kueleza broka wako ni hisa za kampuni gani wataka kununua, wataka kuzinunua kwa bei gani kila hisa na wataka hisa ngapi. Baada ya kumpa mwelekezo huu, broka wako atatafuta anaye hisa unazohitajikatika bei ulilotaja au la chini zaidina kisha, atazinunua chini ya jina yako.
Ubadilishanaji huu wa fedha na hisa utarekodiwa katika CDSC huku hisa ulizonunua zikiwekwa chini ya akaunti yako ya CDSC na zikiondolewa kutoka kwa akaunti ya mmiliki wa hapo awali.
Kuuza hisa
haririUnapotaka kuuza hisa, wafaa kuelezea broka wako ni hisa zipip wataka kuuza na kwa bei gani. Baada ya kumpa mwelekezo huu, broka wako atasajili hiza hizo katika soko ambapo aliyeridhika na bei ya hisa hizo atazinunua.
Ubadilishanaji huu wa fedha na hisa utarekodiwa katika CDSC huku hisa ulizouza zikitolewa chini ya akaunti yako ya CDSC na zikiwekwa katika akaunti ya aliyezinunua.
Angalia pia
haririViungo vya nje
hariri- Soko la Hisa la Nairobi Ilihifadhiwa 3 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
- "Capital Markets Authority"
- CDSC Kenya