LUBILOSA ilikuwa jina la mradi wa uchunguzi ambao ulikusudia kuendeleza kibadala cha kibiolojia kwa udhibiti wa kikemikali wa nzige. Jina hili ni akronimi ya jina la mradi kwa Kifaransa: Lutte Biologique contre les Locustes et les Sauteriaux (udhibiti wa kibiolojia wa nzige na panzi). Wakati wa maisha yake ya miaka 13 (novemba 1989 hadi desemba 2002) mradi umetambulisha tenganisho la kuvu Metarhizium ambayo ina maambukizo mazuri dhidi nzige, na umepitia hatua zote zilizo lazima kwa kuendeleza dawa ya kibiolojia “Green Muscle” iliyo na viiniyoga (spora) vya kuvu hii ndani yake[1]. Green Muscle ilizalishwa huko Afrika Kusini, lakini siku hizi inaonekana kama bidhaa hii imepotea kutoka sokoni. Kwa hivyo kampuni Eléphant Vert ya Uswisi [1] imetoa bidhaa nyingine inayoitwa "NOVACRID" na inayozalishwa katika Maroko. Dawa ya kufanana, “Green Guard”, inazalishwa huko Australia.

Marejeo

hariri
  1. Lomer C.J., Bateman R.P., Johnson D.L., Langewald, J. and Thomas, M., 2001. Biological Control of Locusts and Grasshoppers. Annual Review of Entomology 46: 667-702.