Nzige
Nzige | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nzige mwekundu, Nomadacris septemfasciata
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Jenasi 12, spishi 16 za nzige:
|
Nzige ni jamii ya panzi wenye uwezo wa kujikusanya kwenye makundi makubwa na kuruka umbali mrefu kwa pamoja. Wanao huitwa tunutu. Nzige wanapokuwa wametawanyika mmojammoja huishi kama panzi wa kawaida. Wanapozaliana na kuongezeka idadi hujikusanya katika makundi. Makundi ya tunutu husafiri kuelekea upande mmoja na kula majani wanakopitia. Makundi ya nzige waliokomaa huweza kufikia idadi ya zaidi ya bilioni na huruka umbali mrefu na kuharibu mazao wanakotua.
Udhibiti wa nzige
haririNzige hudhibitiwa kwa dawa za kikemikali. Ni vema nzige wadhibitiwe wanapokuwa wadogo au tunutu kabla hawajaingia mashamba na kuharibu mazao. Tunutu wanaweza kudhibitiwa kwa mashine zinazobebwa mikononi au mgongoni, au zilizopachikwa juu ya gari la pickup. Makundi ya nzige waliokomaa ni lazima yadhibitiwe kwa ndege.
Hivi karibuni dawa ya kibiolojia imeendelezwa na mradi wa kimataifa LUBILOSA. Dawa hiyo ina spora za kuvu Metarhizium acridum ndani yake. Siku hizi kuna vifundiro vya kibiashara vitatu sokoni: "Green Muscle" na "Green Guard" vya kampuni BASF na "NOVACRID" cha kampuni ÉLÉPHANT VERT. Vifundiro hivi vinaweza kupulizwa katika mafuta ya diseli kwa mashine za kiwango kidogo sana (g 50 katika L 0.5-2 kwa ha).
Katika Biblia
haririNzige wanatajwa mara nyingi katika Biblia kati ya vitisho vikubwa kwa binadamu kutokana na njaa wanayoweza kusababisha.
Pia wanatajwa kama chakula maalumu cha Yohane Mbatizaji, mtangulizi wa Yesu.
Spishi za Afrika
hariri- Anacridium aegyptium, Nzige-miti wa Misri (Egyptian Locust)
- Anacridium melanorhodon
- Anacridium m. melanorhodon, Nzige-miti wa Saheli (Sahelian Tree Locust)
- Anacridium m. arabafrum, Nzige-miti Arabu (Arabian Tree Locust)
- Anacridium wernerellum, Nzige-miti Mabawa-meusi (Sudanian Tree Locust)
- Dociostaurus maroccanus, Nzige wa Maroko (Moroccan Locust)
- Locusta migratoria, Nzige Msafiri (Migratory Locust)
- Locusta m. migratorioides, Nzige Msafiri wa Afrika (African Migratory Locust)
- Locusta m. capito, Nzige Msafiri wa Madagaska (Malagasy Migratory Locust)
- Locustana pardalina, Nzige Kahawia (Brown Locust)
- Nomadacris septemfasciata Nzige Mwekundu (Red Locust)
- Schistocerca gregaria, Nzige-jangwa (Desert Locust)
Spishi za mabara mengine
hariri- Austracris guttulosa (Spur-throated locust)
- Calliptamus italicus (Italian locust)
- Ceracris kiangsu (Yellow-spined bamboo locust)
- Chortoicetes terminifera (Australian plague locust)
- Locusta migratoria (Migratory locust)
- Locusta m. manilensis (Oriental migratory locust)
- Locusta m. migratoria (Asiatic migratory locust)
- Patanga succincta (Bombay locust)
- Rhammatocerus schistocercoides (Mato Grosso locust)
- Schistocerca cancellata (South American locust)
- Schistocerca piceifrons (Central American locust)
Picha
hariri-
Nzige-miti Arabu
-
Nzige-miti wa Saheli
-
Nzige wa Maroko
-
Nzige msafiri wa Afrika
-
Nzige kahawia
-
Nzige-jangwa akitaga mayai
-
Udhibiti wa nzige wekundu kwa "Green Muscle" huko Tanzania
-
Spur-throated locust
-
Italian locust
-
Australian plague locust
-
Bombay locust
-
South American locust
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nzige kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |