Lafarge ni kampuni ya viwanda ya Kifaransa iliyobobea katika vifaa vya ujenzi. Kwa sasa (2008) ni kampuni kubwa zaidi duniani ya kutengeneza saruji na kwa idadi iliyosafirishwa mbele ya Holcim.[2]

Lafarge
Makao MakuuParis, France
Mapato kabla ya riba na kodiincrease €3.362 billion (2008)[1]
Profitincrease €1.598 billion (2008)[1]
Tovutiwww.lafarge.com
Mifuko ya Saruji ya Lafarge

Historia

hariri

Lafarge ilianzishwa mwaka 1833 [3] na Joseph-Auguste Pavin de Lafarge katika mji wa Le Teil (Ardèche), kutumia mawe ya chokaa iliyo katika mji wa Mont Saint-Victor kati Le Teil na Viviers. Mawe ya chokaa ilikuwa nyeupe na 'argillaceous'} na ilitoa kwa kiasi kikubwa chokaa ya aina ya 'hydraulic lime'.

Mwaka 1864 Lafarge ilitia saini mkataba wake wa kwanza wa kimataifa ya utoaji wa tani 110.000 ya chokaa kwa mradi wa ujenzi wa Suez Canal [3] Ilitengeneza saruji za aina ya 'calcium aluminate'. Ilikuwa pia ni mwaanzilishi wa saruji nyeupe ya Portland, ambayo bado hufanywa katika kiwanda cha kwanza cha Le Teil cha kampuni.

Mwaka 1919, kampuni ya umma iliundwa, jina lake "Société anonyme des chaux et ciments de Lafarge et du Teil."

Mwaka 1980, ilijiunga na kampuni ya saruji ya Coppée na kuwa SA Lafarge Coppée.

Lafarge ilinunua kiwanda kutoka Kampuni ya Taifa ya Gypsum mapema-1987.[4] Miaka kumi baadaye, ilinunua Redland plc, kampuni ya marekani iliyoongoza katika kuendesha mashimo ya madini.

 

Mwaka 2001, Lafarge, kama kampuni ya pili kubwa zaidi ya saruji, ilinunua kampuni ya Blue Circle Industries (BCI), ambayo wakati huo ilikuwa kampuni ya sita kubwa zaidi ya saruji duniani, na kuwa kiongozi wa ulimwengu katika viwanda vya saruji [3]

Mwaka 2006, wanahisa wa Lafarge wa Amerika Kaskazini waliitikiaombi la bilioni $3 kutoka Kundi la Lafarge ambalo liliipa kampuni mzazi udhibiti kamili wa biashara ya Amerika ya Kaskazini, kuondoa LNA(Lafarge North America) kutoka Soko la Hisa la New York. Awali, kundi hilo lilimiliki asilimia 53% ya hisa za LNA [5]

Mwaka 2007, waliuza kiungo chao cha paa kwa kampuni ya kibinafsi katika mpango uliosababisha Lafarge kubakia na asilimia 35 ya hisa zake [3]

Mnamo Desemba 2007, Lafarge ilitangaza ununuzi wa kikundi cha saruji cha Orascom, iliyo na makao Misri,na iliyo na shughul Afrika nzima na 'Middle east', kutoka kwa Orascom Construction Industries (OCI) [6]

Tarehe 15 Mei 2008 Lafarge ilinunua Larsen & Turbo Ready Mix-Concrete (RMC) biashara nchini India kwa milioni $ 349.[7].

Wasiwasi wa mazingira

hariri

11 Julai 2008, gazeti la Albany Times Union lilitoa taarifa kwamba kiwanda cha Lafarge cha Ravena, New York "kilikuwa chanzo cha uchafu mwingi zaidi wa zebaki katika mji wa New York kutoka 2004-2006" [8] Kulingana na hadithi, mipango yalikuwa yamefanywa kuboresha kiwanda hicho ili kupunguza uchafu wa zebaki. Hadithi ya pili, iliyochapishwa siku iliyofuata, ilisema kuwa kiwanda hicho kilikuwa kimeto paundi 400 (kilo 181) za zebaki kila mwaka kutoka 2004-2006.[9]

Takwimu

hariri

Ifuatayo ni muhtasari wa takwimu:[1][10]

Takwimu za fedha katika mamilioni ya Euro
Mwaka 2001 2002 2003 2004 2005 2006 2007 2008
Mauzo 13,698 14,610 13,658 14,436 15,969 16,909 17,614 19,033
EBITDA 2,862 3,101 2,820 3,028 2,920 3,610
Matokeo ya Ujumla 750 446 728 868 1,096 1,372 1,909 1,598
Madeni ya Ujumla 9,332 8,544 6,734 7,017 7,221 9,845 8,685 16,884
Wafanyikazi 82,892 77,547 75,733 77,075 80,146 82,734 77,720 83,440

Angalia Pia

hariri

Washindani wakuu wa Lafage ni:

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named AR2008
  2. Kiasi kilichosafirishwa mwaka 2008 (2007 katika mabano), tani milioni: Lafarge 155 (136.4); Holcim 143.4 (149.6). Kutoka: 2008 ripoti za kampuni.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 [4] ^ Historia ya Lafarge Ilihifadhiwa 26 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.
  4. Wharton, George."Great Lakes Fleet Page Vessel Feature - J. A. W. Iglehart," Boatnerd.com.
  5. Kampuni mzazi ya Kifaransa yalenga shabaha kwa kampuni kubwa lakini isiyojulikana Lafarge North America
  6. Lafarge yanunua Orascom Cement kwa Euro bilioni 10
  7. Lafarge yaingia katika biashara ya kampuni ya India ya RMC kwa kununua L & T
  8. |title=Update at Ravena Cement Plant to Clean Air |accessdate=2008-07-29 |publisher=Albany Times Union
  9. "Update at Ravena Cement Plant to Clean Air". Albany Times Union. Iliwekwa mnamo 2008-07-29.
  10. OpesC

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lafarge kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.