Lango:Hip hop/Intro
Hip hop hutaja vitu viwili kwa pamoja, yaani, utamadauni wa hip hop na muziki wake. Mtindo huu wa muziki ulianza kunako miaka ya 1970 huko mjini New York City na uvumbuzi uliofanywa na baadhi ya waanzilishi kama vile Kool DJ Herc, Grandmaster Flash, Grandwizard Theodore, Afrika Bambaataa, na DJ Hollywood. Elementi maarufu ya utamaduni huu ni kurap, U-DJ/utayarishaji wake, graffiti, breakdancing, na beatboxing. Utamaduni huu umechumbukia katika jamii za Wamarekani Weusi, Wakaribi-Waafrika na Walatino Amerika wa mjini New York City (na South Bronx kukiwa kama ndiyo kitovu kikuu cha utamaduni huu) mwishoni mwa miaka ya 1970.
Ilikuwa DJ Afrika Bambaataa ambaye alitaja nguzo tano za utamaduni wa hip-hop: U-MC, U-DJ, breaking, kuandika graffiti, na ufahamu. Elementi zingine ni pamoja na beatboxing, mtindo wa hip hop, na lugha za mitaani. Tangu kuanzishwa kwake huko mjini Bronx, staili ya maisha ya utamaduni wa hip hop siku hadi siku na kuenea dunia nzima. Wakati muziki wa hip hop unaanza kuchipukia, ilikuwa hasa unategemea na mzunguko wa ma-diski jockey waliotengeneza wizani na midundo kwa kurudia-rudia na kusimamisha (hasa sehemu ndogo ya wimbo alioutaka uwekewe au uwe na maudhui ya kingoma-ngoma) kwenye turntable mbili, ambapo hasa kwa sasa huitwa kusampo wimbo.
Hii baadaye ikaja kusindikizwa na "rap", mtindo wa wizani unaotoa maneno au mashairi yaliyo kwenye vipimo vya mstari ulalo wa nota 16 katika fremu ya muda, ikiwa sambamba na beatboxing, maujanja ya sauti hutumika hasa katika kugezea mfumo wa midundo na elementi za muziki mbalimbali na mautundu na vionjo kadhaa kutoka kwa Ma-DJ wa hip hop.
Muundo kamili wa kudansi na staili kadha wa kadha za mavazi zimezua mashabiki miongoni mwao katika muziki mpya. Elementi hizi zimeonesha mabadiliko ya na maendeleo kadha wa kadha katika historia ya utamaduni huu. Baadhi ya miziki ya hip-Hop hutoa maelezo ya kisiasa.