Lango:Hip hop/Wasifu uliochaguliwa/Ice Cube


Ice Cube akitumbuiza mjini Toronto, Kanada, 2006.
Ice Cube akitumbuiza mjini Toronto, Kanada, 2006.

O'Shea Jackson (amezaliwa tar. 15 Juni, 1969), anajulikana sana kwa jina lake la kisanii kama Ice Cube, ni rapa wa Kimarekani, mwigizaji na pia mwongozaji wa filamu. Anatazamika kama ni msanii mkubwa duniani wa muziki aina ya hip hop.

Ice Cube alianza shughuli zake za kimuziki kama mmoja wa waanzilishi wa kundi la muziki aina ya hip hop maarufu kama N.W.A., baadae akaanza shughuli za kuimba muziki akiwa peke yake bila ushirika wowote ule huku kwa mbali anaigiza filamu, kitu ambacho kilimpa mafanikio makubwa sana. Mnamo mwaka wa 1992, akamuoa Kimberly Woodruff, kwa pamoja wamezaa watoto wanne.

Mwaka huo huo wa 1992, Ice Cube akabadili dini na kuwa mwislam. Kuanzia kati kati mwa miaka ya 1990 na kuendelea, Cube aliegemea sana katika shughuli za uigizaji, na shughuli zake za kimuziki zikawa zinafiriwa kama zina fifia kwakuwa hakuwa anaangaikia sana muziki kama alivyokuwa mwanzo.

Cube akabaki kuwa kama mmoja wa waonekanao kuwa ni marapa wa West Coast rappers, kwa kuwa alikuwa akitoa msaada mkubwa sana katika vikundi vya rap. Anafahamika hasa kwa uimbaji wake vile akizungumzia siasa na sela za kibaguzi, kwasababu nyimbo nyingi za Ice zilikuwa zikifiriwa kama tiba kwa watu weusi wa Marekani.

Soma zaidi....