Lango:Kenya/Wasifu uliochaguliwa/1
Wangari Muta Maathai (1 Aprili 1940 – 25 Septemba 2011) alikuwa mwanaharakati wa masuala ya mazingira na haki za wanawake kutoka nchini Kenya. Mwaka wa 2004 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani. Yeye ni mwanamke Mwafrika wa kwanza kupokea tuzo hilo. Pia, aliwahi kuwa mbunge wa Kenya na waziri msaidizi katika serikali ya Mwai Kibaki kati ya Januari 2003 hadi Novemba 2005.
Katika maandalizi ya uchaguzi wa 2007 Maathai alisimama upande wa rais Kibaki lakini hakuteuliwa na chama cha PNU akagombea kwa chama cha Mazingira Green Party lakini hakurudi bungeni.