Lango hili lipo katika ujenzi

Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia


Jambo!!!
Karibu (Welcome)

WikiLango Kenya

Flag of Kenya
Flag of Kenya
Coat of Arms of Kenya
Coat of Arms of Kenya
Location of Kenya

Jamhuri ya Kenya ni nchi iliyoko Afrika Mashariki katika ikweta, kando ya Bahari ya Hindi. Kenya imepakana na Ethiopia (kaskazini), Somalia (kaskazini mashariki), Tanzania (kusini), Uganda na Ziwa Victoria (magharibi), kisha Sudan Kusini (kaskazini magharibi). Mji mkuu ni Nairobi.

Mji mkuu ni Nairobi. Idadi ya watu imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni na kufikia milioni 50. Kenya ina mbuga mbalimbali wanamoishi maelfu ya wanyama pori wa kila aina.

Jina Kenya linatokana na mlima Kenya, ulio wa pili kwa urefu barani Afrika, Kabla ya mwaka wa 1920, eneo linaloitwa Kenya liliitwa Himaya ya Uingereza Afrika Mashariki, kwa hivyo hapakuwa na haja kutaja neno mlima uliporejelea mlima huo.

Makala iliyochuguliwa

Nairobi

Nairobi ni mji mkuu wa Kenya na vilevile mmojawapo wa mikoa ya Kenya. Ni kati ya miji mikubwa ya Afrika. Kulingana na sensa ya 2009, Nairobi ina wakaaji 3,138,295. Pamoja na vitongoji vyake, Nairobi ni mji wa 12 kwa ukubwa barani Afrika.

Jina Nairobi limetokana na neno la Kimaasai, Enkare nairobi, linalomaanisha "mahali penye maji baridi." Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi, lakini hasa Kiingereza na Kiswahili, pamoja na Sheng. (Soma zaidi...)

Picha iliyochaguliwa

Tea Plantation near Kericho Town
Tea Plantation near Kericho Town
Mashamba ya chai karibu na Kericho, Wilaya ya Kericho.

Je wajua ...

  • ... kwamba wanafunzi katika nchi ya Kenya hufunzwa kwa lugha ya Kiingereza?
  • ... la kwamba jina rasmi la Kenya ni Jamhuri ya Kenya?
  • ... la kwamba Ziwa Turkana ndio ziwa kuu katika jangwa ulimwenguni?
  • ... kwamba Kenya ina upaka na 'ziwa kubwa kwa eneo ya Afrika, Ziwa Victoria' ?
  • ... kwamba Mlima Kenya ni mlima wa pili kwa urefu katika Afrika? Ni metre 5 199 (ft 17 057).
  • ... ya kwamba asilimia thelathini na tatu ya maua katika Umoja wa Ulaya hutoka Kenya?
  • Wasifu uliochaguliwa

    Wangari Maathai

    Wangari Muta Maathai (1 Aprili 1940 – 25 Septemba 2011) alikuwa mwanaharakati wa masuala ya mazingira na haki za wanawake kutoka nchini Kenya. Mwaka wa 2004 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani. Yeye ni mwanamke Mwafrika wa kwanza kupokea tuzo hilo. Pia, aliwahi kuwa mbunge wa Kenya na waziri msaidizi katika serikali ya Mwai Kibaki kati ya Januari 2003 hadi Novemba 2005.

    Katika maandalizi ya uchaguzi wa 2007 Maathai alisimama upande wa rais Kibaki lakini hakuteuliwa na chama cha PNU akagombea kwa chama cha Mazingira Green Party lakini hakurudi bungeni.

    (Soma Zaidi...)

    Jamii

    Masomo inayohusu Kenya

    Milango inayohusiana

    Associated Wikimedia

    Kenya on Wikibooks  Kenya on Wikimedia Commons Kenya on Wikinews  Kenya on Wikiquote  Kenya on Wikisource  Kenya on Wikiversity  Kenya on Wiktionary 
    Manuals and books Images and media News Quotations Texts Learning resources Definitions