Lango:Ulaya/Wasifu uliochaguliwa/1
Karolo Mkuu (Kilatini: Carolus Magnus; Kijer.: Karl der Große; Kifar.: Charlemagne) aliishi kati ya 742 hadi 814 akawa mfalme wa Wafranki akaendele kuwa Kaizari wa Dola takatifu la Roma aliloanzisha. Anakumbukwa kama "baba wa Ulaya" maana milki yake iliunganisha nchi zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya (chanzo cha Umoja wa Ulaya) karne nyingi baadaye.