Lena Headey

Mwigizaji wa Uingereza (Amezaliwa 1973)

Lena Kathren Headey (amezaliwa Oktoba 3, 1973) ni mwigizaji wa Uingereza. Alianza kua maarufu kimataifa baada ya kuigiza kama Cersei Lannister katika tamthilia ya Game of Thrones ambapo alichaguliwa mara 5 kuwania tuzo za Primetime Emmy Award na Golden Globe Award . Na pia alikua maarufu baada ya kuigiza kama Malkia Gorgo kwenye filamu ya 300(2006).

Lena Headey Mwaka 2019

Maisha Ya Zamani hariri

Lena Kathren Headey amezaliwa huko Hamilton nchini Uingereza tarehe 3 Oktoba 1973[1], ni mtoto wakike na wazazi wake wote Sue na John Headey wakiwa ni Waingereza. Babayake alikua ni afisa wa polisi kutoka Yorkshire, alifanya kazi Hamilton wakati Lena anazaliwa katika kituo cha Polisi cha Bermud. Anamdogo wake wakiume anayeitwa Tim[2]. Lena ana asili ya Kiingereza na Ireland. Alipokua na umri wa miaka mitano familia yake ilirudi Uingereza na kuishi Somerset. Alisoma masomo ya ballet akiwa mdogo[3]. Headey alipata uzoefu wake katika kuigiza alipokua mwanafunzi wa Chuo cha Shelley, akiwa na umri wa miaka 17. Akiwa anaigiza katika ukumbi wa Chuo ulioitwa Royal National Theatre, alichaguliwa kuigiza katika tamthilia ya Waterland 1992[4].


Marejeo hariri

  1. https://www.tvguide.com/celebrities/lena-headey/bio/161706
  2. "She's Beautiful When She's Angry". Men's Health (kwa en-US). 2010-10-05. Iliwekwa mnamo 2024-04-30. 
  3. Lena Heady on Letterman (kwa sw-TZ), iliwekwa mnamo 2024-04-30 
  4. YorkshireLive (2008-01-16). "Lena gets ready to terminate TV ratings". Yorkshire Live (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-30. 
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lena Headey kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.