Liputa ni mtindo wa uvaaji wa mavazi ya kisasa kwa wanawake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mtindo wa kuvaa liputa ulikuja baada ya athari za ukoloni.[1] Liputa maana yake ni uvaaji wa nguo za rangi lakini katika mtindo[2]. Kawaida wanawake wa Kongo huvaa mavazi ya rangi ya kuvutia sana. Kitamaduni ni muhimu sana kuvaa vizuri. Wanawake wa Kongo huvaa mavazi ya Liputa kwenye sherehe ya ndoa, sokoni, kwenye mkusanyiko au kwenye karamu rasmi kwa. Akina mama pia hubeba watoto wao kwa kutumia malighafi za Liputa.

Mwaname wa Kiafrika akiwa ndani ya vazi la Liputa

Njia ya kutengeneza

hariri

Bidhaa ina vipande vinne vilivyotengenezwa na malighafi ya aina moja . Kipande kimoja huvaliwa kama blauzi, kimoja cha kanga, kimoja kiunoni, na kingine cha kufunga kichwani kama kilemba.Blauzi ya ina shingo kubwa iliyokatwa na mkono mkubwa. Kipande kimoja hufungwa kuanzia kiunoni hadi miguuni ili kufunika miguu. Kipande kingine kinafungwa kiunoni ili kusaidia kitambaa na kitambaa kikae mahali pake.Pia huashiria kama mwanamke ameolewa au hajaolewa. Kipande hiki kinafungwa kwa njia ambayo fundo inaonekana kama upinde mkubwa mzuri kwenye kiuno. Kipande cha mwisho hutumika ichwani kama kilemba cha kufunika nywele. Siku hizi hawafungi nywele zao na kilemba au kuacha nywele wazi hata kama wamefunga kilemba. Blauzi kawaida huwa na nyuzi nyuzi za rangi na shanga za mapambo karibu na shingo. Shingo ni kubwa zaidi, ili kichwa kiweze kuingia kwa urahisi. Vifungo vya jadi hazitumiwi, hata hivyo wakati mwingine vifungo vinaweza kutumika.

Marejeo

hariri
  1. "Culture". Democratic Republic of Congo. Iliwekwa mnamo 2022-03-17.
  2. "Culture". Democratic Republic of Congo. Iliwekwa mnamo 2022-03-17.