Lisa Germaine Gerrard (amezaliwa 12 Aprili 1961) ni mwanamuziki, mwimbaji, na mtunzi kutoka nchini Australia. Alianza kupata umaarufu akiwa moja kati ya kundi la muziki la Dead Can Dance akiwa na mwanamuziki mwenzake wa zamani Brendan Perry.

Lisa Gerrard

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Lisa Gerrard
Amezaliwa 12 Aprili 1961 (1961-04-12) (umri 63)
Asili yake Melbourne, Australia
Aina ya muziki Neoclassical, New Age, Ethereal Wave, Gothic rock
Kazi yake Mwimbaji
Mwanamuziki
Mtunzi
Ala Sauti
Yangqin
Accordion
Aina ya sauti Contralto
Miaka ya kazi 1981–mpaka sasa
Ame/Wameshirikiana na Dead Can Dance
Tovuti Lisa Gerrard

Tangu alivyoanza shughuli zake kunako mwaka wa 1981, amepata kujihusisha katika miradi mikubwa ya kimuziki. Gerrard amepata tuzo ya Golden Globe Award kwa ajili ya kibwagizo cha filamu ya Gladiator, ambayo alishirikiana na Hans Zimmer na and Klaus Badelt. Kwa upande mwingine wa uimbaji, ni mpiga ala kwa kiasi kikubwa katika kazi zake, maarufui kwa kupiga yangqin (hammered dulcimer ya Kichina).

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: