Luangwa ni mji wa Zambia kwenye pembetatu ya mpakani kati ya Zambia, Msumbiji na Zimbabwe mahali panapoishia mto Luangwa katika Zambezi si mbali na ziwa la lambo la Cabora Bassa. Ng'ambo ya Zambezi upande wa Zimbabwe iko Kanyembe na ng'ambo ya mto Luangwa iko Zumbo (Msumbiji).

Location Luangwa in Zambia coordinates 15°37'S 30°23'ELuangwa
Luangwa is located in Zambia
Luangwa
Luangwa

Mahali pa mji wa Luangwa katika Zambia

Majiranukta: 15°37′0″S 30°23′0″E / 15.61667°S 30.38333°E / -15.61667; 30.38333
Nchi Zambia
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 3 400

Luangwa iko kwa kimo cha mita 347 juu ya UB ni makao makuu ya wilaya yenye wakazi 18,948 (sensa 2000).

Kabla ya uhuru mji ukaitwa Feira kwa sababu iliundwa na Wareno kutoka Msumbiji.

Kuna barabara moja tu inayounganisha Luangwa na barabara kuu ya Zambia iliyoko takriban kilomita 100 upande wa kaskazini. Hakuna feri za mara kwa mara lakini watu huvukizwa kwa maboti madogo.

Makala hii kuhusu maeneo ya Zambia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Luangwa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.