Kumbikumbi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d #WPWP,#WPWPTZ
I read from an article in social networks
Tags: Reverted Mobile edit Mobile web edit
Mstari 7:
[[Jamii:Mchwa]]
[[Jamii:Chakula]]
 
 
 
 
Katika kujibu maswali kutokana na Kibali cha kuuliza nilichotoa hapo kabla naomba nijibu Swali la Mwenzetu Lydia Rogath aliyeuliza;
 
Mchwa anageukaje kuwa Kumbikumbi?
 
Majibu:
 
Nitaanza na maelezo mafupi ambayo nayaanza kwa kuwauliza ninyi.
 
Baada ya mvua kunyesha na Kumbikumbi kuonekana,Je umewahi kuona KUMBIKUMBI WAWILI wamekatika mbawa halafu wanafuatana kwa karibu kabisa mmoja akiwa mbele na mwingine akiwa nyuma?
 
Kama umeona tukio hilo basi yule wa mbele ni Jike na wa nyuma ni Dume.Wameungana pamoja kama Couple.Vile wanavyozurura wanatafuta sehemu yenye udongo mzuri unaofaa kwa ajili ya kuanzisha makazi mapya.Kama hawatodhuriwa na maadui,wakifanikiwa kupata sehemu hiyo yule wa mbele ambaye ni jike atasimama na kuanza kuchimba ka shimo kadogo na kujifukia ndani huku dume akimsaidia.
 
Watafanya hivyo kwa kwenda chini hadi sehemu ambayo watajiridhisha kwamba ni salama kwao angalau wanaweza kujisitiri.Wakishafika eneo hilo,watasaidiana kupanua chumba kidogo ili kuwa na nafasi ya kutosha halafu jukumu la kuanza kumlisha yule jike ili anenepe litaanza kutekelezwa na dume peke yake.
 
Kwa maana nyingine ni kwamba Dume anamuandaa Malkia.Ataendelea na zoezi hilo mpaka pale jike atakaponenepa kabisa na kushindwa kujisogeza na wakati sahihi utakapofika basi yule Malkia atapandwa na dume kisha mayai yatatagwa.
 
Nakukumbusha kwamba familia ya kumbikumbi kwenye kichuguu kimoja imegawanyika kama ifuatavyo
 
1.Malkia na Mume wake....wale waliokuwa wamefuatana.
2.Watenda kazi...workers
3.Askari...Soldiers.Hawa ni wale wenye mikasi mikubwa na vichwa vikubwa
 
4.Kumbikumbi....uzao mpya unaanzishwa na hawa.
 
Jambo la kushangaza hapa ni kwamba Malkia ana uwezo wa kuamua mayai atakayotaga yawe ya kundi gani kati ya hayo niliyotaja.
 
Kwa mfano:
 
Kwa kuwa hawa wawili wamekutana na wameandaa chumba kidogo tu cha kuishi uzao wa kwanza utakuwa ni wa kundi la wafanyakazi zaidi ili waongeze vyumba na kupanua ngome .Hawa watatengeneza kichuguu imara lakini kikianzia chini ardhini ili iwe kama msingi imara wa kichuguu tutakachokuja kukiona kikimea huku juu ya uso wa dunia.
 
Kutoka pale malkia alipo na mume wake watamsogeza chini zaidi kwa sababu za kiusalama kwa kuwa bado hawana jeshi lolote imara la kumlinda.Kule kutakuwa na chumba kikubwa zaidi na Baba Mchwa ataacha kabisa shughuli za utafutaji kwa kuwa kazi hiyo itafanywa na uzao wa kwanza wa wafanyakazi.
 
Wote wawili wataendelea kutunzwa mpaka wakati ufaao wa malkia kupandwa na kutaga tena.
 
Awamu hii mayai karibu yote yatakuwa ni Askari watupu ili kuimarisha ulinzi.
 
Kwa hiyo mpaka hapo kunakuwa na vitengo viwili muhimu.
-Ulinzi
-Ujenzi na Chakula
 
Malkia akiwa anataga atazingatia upungufu wa kikosi kimojawapo kwa kila msimu na wakati huo huo shughuli zitakuwa zinaendelea kwa kasi kubwa wajakazi na askari wakijituma usiku na mchana mpaka kichuguu kinakuwa kikubwa na kirefu kama ambavyo tumekuwa tukiona maeneo mbalimbali.
 
Uimara wa jeshi na ukubwa wa kichuguu utapelekea siku moja Jeshi na wajakazi wamuhamishe Malkia kutoka kule chini walipomuandalia Ikulu ndogo na kumleta upande wa juu wa kichuguu sehemu hii tunayoiona sisi ila ni pale katikati kabisa na eneo la kukaribia ardhi ambapo wanakuwa wameshaandaa Ikulu kubwa zaidi.
 
Sehemu hii ni nzuri zaidi kwa kuwa wakati wa joto ni rahisi wajakazi kufungua njia za upande ule unaopokea upepo na upande wa juu ili hewa safi iingie vizuri na kutokea juu au upande wa pili.
 
Sehemu hii ni nzuri pia kwa kuwa hata mvua ikinyesha wajakazi wanafunga tu vent zote hivyo mvua haitoingia ndani na hata kama itazidi na kutafuta upenyo basi maji yakifika kule kwenye ikulu ndogo ya chini yatakuta malkia kahamishwa yuko sehemu salama huku katikati mwa kichuguu....wana akili na hesabu kubwa mno.
 
Wakati haya yote yakiendelea nakukumbusha kwamba zoezi la kutaga nalo litakuwa linaendelea kwa majira yake na Malkia ataamua aongeze idara ipi kulingana na mahitaji.
 
Kwa kuwa Malkia anajua yeye ni zao la Kumbikumbi basi ndio kuna wakati ambao hahitaji kuongeza Jeshi wala wajakazi ila ataongeza Kumbikumbi ili wakitoka waweze kuruka mbali na kusambaa ili kuanzisha uzao wao na kuongeza falme za mchwa popote pale inapowezekana.
 
Kumbikumbi hao wataruka na baadae mbawa zitakatika watatafutana na kukutana wenye jinsia tofauti ambao wataanza harakati kama nilivyoeleza kwa hawa wawili waliofanikiwa kutengeneza kichuguu kikubwa kabisa.
 
Nakukumbusha!
 
Kundi la wajakazi na Askari hawana jinsia.Si madume si majike.Ni Sexless
 
Kwa nini iwe hivyo?
 
Huu si ukatili bali ukiona kichuguu kinavyojengwa kwa ushirikiano usiku na mchana ni kwamba hawana muda wala hisia za kuwaza mapenzi wala hakuna atakayetumwa udongo wa kujengea yeye akapitiaGuest kwanza kisa ana hamu zake.Hapa kazi ni kazi na Ulinzi ni Ulinzi.Hakuna kulinda na kuweka silaha chini kisa demu mkali kapita.
 
Kundi pekee lenye uzao na jinsia ni kutoka kundi la kumbikumbi tu.
 
Asante.
 
By Mr.Frank Mbowe