Rosebud Kurwijila : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ' '''Rosebud Violet Kurwijila''', wa Tanzania, ni mkuu wa idara ya maendeleo ya kiuchumi vijijini na kilimo ya Umoja wa Afrika. Kabla alikua ni mrati...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 11:51, 20 Juni 2018

Rosebud Violet Kurwijila, wa Tanzania, ni mkuu wa idara ya maendeleo ya kiuchumi vijijini na kilimo ya Umoja wa Afrika. Kabla alikua ni mratibu wa programu ya maendeleo ya ACTIONAID iliyopo Tanzania.

Wasifu

Rosebud Kurwijila, ni mtanzania na ni mkuu wa idara ya uchumi wa vijijini na kilimo. Rosebud alipata shahada ya kwanza ya kilimo kutoka katika chuo cha kilimo cha Sokoine Sokoine University of Agriculture, kilichopo Tanzania mnamo mwaka 1976, mwaka 1983 alipata shahada ya uzamili ya uchumi wa kilimo kutoka chuo kikuu cha London University of London na pia shahada ya uzamili ya falsafa katika uchumi na maendeleo mwaka 1994 kutoka katika chuo cha East Anglia University of East Anglia (UK) (1994).

Katika kipindi chake cha ajira ameshawahi kutumika kama mshauri katika sehemu tofauti zinazohusiana na mambo ya kilimo, uchumi wa vijijini na usalama wa chakula. Mwaka 1995 – 1997, alikua ni mshauri mwandamizi kutoka katika kampuni inayohusika na huduma ya ushauri, alihusika na upatikanaji na ufanyaji wa miradi.

Rosebud amechapisha makala nyingi katika majarida ya kimataifa kuhusu usalama wa chakula, uchumi wa vijijini, teknolojia ya kilimo na mambo mengine yanayohusiana na hayo.

Maeneo yake ya ufanisi ni pamoja na usimamizi wa mipango, utungaji wa sera na usimamizi wa wafanyakazi.

Ameolewa na pia ana watoto wanne (4).[1]

Marejeo

Viungo vya nnje

Kigezo:Mwanasiasa-wa-Tanzania-mbegu