Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)

Chuo kikuu kilichopo Tanzania

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Sokoine Universityof Agriculture (SUA)) kipo katika manisipaa ya Morogoro nchini Tanzania. Ni chuo kikuu pekee cha kilimo nchini. Kilipewa jina kwa heshima ya mwanasiasa marehemu Edward Sokoine.

Chuo hicho kilianzishwa mwaka 1984; kabla ya hapo kilikuwa chuo kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu mwaka 1970.

Mwaka 1984 chuo kilianza na vitivo vitatu:

  • Kitivo cha kilimo
  • Kitivo cha misitu pamoja na
  • Kitivo cha tiba za mifugo

na hivi karibuni kimeanzishwa

  • Kitivo cha sayansi.

Chuo kinadahili wanafunzi wa shahada za kwanza na za uzamili katika vitivo vyote isipokuwa kitivo cha sayansi ambacho hakitoi shahada za uzamili. Chuo kina wanataaluma zaidi ya mia tatu na kwa mwaka wa mwisho wa masomo kimedahili wanafunzi wa shahada za kwanza wapatao 2400 na wale wa shahada za juu zaidi ya mia mbili.

SUA ilikua na chuo kishiriki cha MUCCoBS (Moshi University College Of Cooperatives and Business Studies) katika mkoa wa Kilimanjaro ambacho kwa sasa kinaitwa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.