Mwai Kibaki : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 45:
Uchaguzi wa 28 Desemba 2007 ulimrudisha Kibaki kwa kipindi cha pili kama rais. Uchaguzi huu ulipingwa na chama cha upinzani,[[ODM]] , na watazamaji wa kimataifa kuwa matokeo hayo hayakuwakilisha matakwa ya Wakenya. Mpinzani wake mkuu, [[Raila Odinga]] alikuwa mbele katika hesabu za kura hadi Kamati ya Uchaguzi iliposimamisha kuhesabu; baada ya kuendelea na matanganzo Kibaki alionekana kuwa mbele. Kulikuwa na hofu ya kwamba matokeo ya majimbo ya uchaguzi kadhaa yalibadilishwa yakiegemea upande wake kwa kumwongezea kura. Hisia hizi zilisababisha ghasia kuibuka [[Nairobi]], [[Kisumu]], [[Eldoret]], [[Kericho]], [[Mombasa]] na sehemu zinginezo nchini. Kibaki aliapishwa upya kuwa rais wa Kenya masaa machache tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi; hafla ilifanywa katika Bustani ya Ikulu ya Nairobi mbele ya waalikwa wachache walioruhusiwa kushuhudia.
 
Kamati iliyobuniwa tutathmini ukweli wa mambo katika uchaguzi huo wa urais, iliyoongozwa na jaji mstaafu kutoka AfricaAfrika Kusini [[Johann Kriegler]], iliripoti kwamba mshindi katika uchaguzi huo wa urais wa 2007 hangeweza kujulikana. Hii ni kwa sababu wizi wa kura ulifanyika katika sehemu nyingi nchini na ulitekelezwa kule mashinani na wafuasi wa wapinzani wote katika kinyang'anyiro cha Urais. Kriegler pia alielekeza lawama kwa [[Tume ya Uchaguzi ya Kenya]] kwa kutowajibika katika utendakazi, na ripoti hiyo ya Krieger ilipendekeza tume hiyo ivunjwe na ibadilishwe na ingine iliyo huru.
 
Kinyume cha uchaguzi wa rais [[uchaguzi wa Bunge la Kenya 2007]] uliendelea bila matatizo makubwa.