Welcome!

hariri

Habari, Ndesanjo. We are working on improving the site (you too, I think!). Don't forget to visit Wikipedia:Jumuia, and check out Recentchanges from time to time. Don't hesitate to correct bad Swahili you find here. Sj 01:53, 24 Septemba 2005 (UTC)Reply

Jina la makala

hariri

Habari Ndesanjo? Nataka kukujulisha kwamba ukiandika makala, uhakikishe jina lake likitamkwa mara ya kwanza (kwa kawaida mwanzoni kabisa) liwe nene kama hili. Kwa mfano, angalia nilivyobadilisha makala Ellen Johnson-Sirleaf. Ili neno liwe nene, una weka ''' kabla na baada yake. Ahsante sana. Marcos 11:42, 21 Novemba 2005 (UTC)Reply

Marcos, asante kwa kunijulisha. Hongera kwa kazi ufanyanyo!

Naomba angalia utoe shauri

hariri

Ndesanjo: nimeweka swali kwa ukurasa wa Marcos [[1]] akiwa mratibu - wewe ukiwa Mswahili kabisa uangalie utoe shauri. Naomba sana. Ukiona vema labda kuna wataalamu ambao wangejua jibu tukibaki na wasiwasi kati yetu. --Kipala 21:03, 17 Januari 2006 (UTC)Reply

Swahili help

hariri

Hi, I have a Swahili question for you. w:Span (unit) lists a Swahili term "unguru" as a unit of measurement. I believe this is a hoax, based on this Slashdot post. Also: w:Fungu'lu. Could you help? Cheers and thanks, w:User:AxelBoldt

Hi Boldt, I've never heard the two terms before. I am not sure if they are swahili terms. I will ask some people around the swahili term for that unit of measurement.

Hi, I just did a search of my own after noticing this, and looks like the correct Swahili word for that unit of measurement is futuri. I just now added that correct word to the English article too. 70.105.38.244 22:58, 17 Desemba 2005 (UTC)Reply

Thanks a lot. Now I know what "futuri" means.

Hi, my "Kamusi ya Kiswahili Sanifu" says: futuri is another word for shubiri which means urefu kutoka kidole gumba hadi cha kati (=a "span", isn´t it? from thumb to middle finger) kiasi cha inchi tisa (=9"); same as "shibiri". But then I am not sure if to absolutely trust the Kamusi in this detail because my two other dics say:

Madan-Johnson: futuri,a short span, as a measure, from the tip of the thumb to the tip of the forefinger; as distinct from shibiri, a full span from thumb to little finger; > arab. ftr / shbr

Velten (1910) has the same as Madan-Johnson on futuri and on shibiri / shubiri;

so even if the two are Wazungu my guess would be that they noted a difference of measures well aware among the Waswahili themselves which may have been lost later - and that the recent kamusi either reflects that the two are mixed up or they had the wrong reference people. --Kipala 19:15, 5 Januari 2006 (UTC)Reply

I have also checked my Arabic dics; one says shibr ﺷﺒﺮ is the span of the hand and futra ﻓﺘﺮﻩ is the span of time; the other one gives futr ﻓﺘﺮ as the span between extended thumb and index finger.I guess as both Swahili words are of Arab origin then older dics are probably right. --Kipala 20:23, 5 Januari 2006 (UTC)Reply

alf lela

hariri

Ndesanjo, hujambo? Hongera na makala mapya ya alf lela.. Nimeongeza maneno mawili kuhusu Baghdadi - wakati wa kukusanyika kwa hadithi hizi ilikuwa makao makuu ya Khalifa na hivyo kituvo cha Uislamu duniani. --Kipala 22:06, 17 Desemba 2005 (UTC)Reply

Kipala, asante sana. Hongera kwa kazi zako. Tuendelee hivi hivi iko siku watakuja wengi zaidi kusaidia. Safi kwa nyongeza yako kwenye Alfu Lela U Lela. Bado nitaipitia tena kuiboresha.

Abu Nuwas

hariri

Ndesanjo, hujambo? Umefika vizuri mwaka mpya? Safari hii naona tatizo na mabadiliko yako Abu Nuwas > Abunuwasi.

Kwa sababu mbili: kwanza nimeshaweka viungo mbalimbali vya Abu Nuwas.

Pili - hapa tunahitaja maelewano kati ya watu wanaochangia kuhusu maswali jinsi ya kutaja vitu. Jina la mtu huyu mshairi mwarabu ni Abu Nuwas - Abunuwasi inaweza kuchukuliwa kwa namna mbili: AMA (ninavyoona) ndiye huyu jamaa wa kifasihi wa "Riwaya" aliye tofauti na Abu Nuwas wa Kihistoria AU ni jina la Kiswahili kwa ajili ya mshairi mwarabu Abu Nuwas; lakini hata kama mimi si mtaalamu katika mambo haya sidhani ni hivyo.

Unaonaje? Sipendi kabisa tupate hivi "vita vya wahariri" jinsi ilivyo katika wikipedia nyingine --Kipala 19:15, 5 Januari 2006 (UTC)Reply

Mimi sijui sana Unguja lakini hata huko naona watu wanaweza kutumia ile "Abu" kuwa sehemu ya jina lao wakiiandika pekee; kwa mfano Sheikh Sayyid bin Omar bin Abdullah bin Abu Bakr bin Salim (1917-1988) aliyekuwa mkuu wa Chuo cha Kiislamu Zanzibar; ninavyoona jina la "Abu Bakr" hutumiwa na Waswahili Waislamu wengi bila kuibadilisha kuwa "Abubakri" au "Abubekri". Unaonaje, si kweli?? --Kipala 19:33, 5 Januari 2006 (UTC)Reply

Ndio Kipala. Asante, mwaka mpya salama kabisa. Hongera sana kwa kazi zako. Umeichangamsha kamusi elezo yetu. Sasa kwenye Abu Nuwas/Abunuwasi. Ni kweli hakuna haja ya kuingia kwenye vita wanavyofanya wengine. Nakubaliana nawe kuhusu jina lake halisi. Nadhani kuna majina ambayo yanapoingia kwenye Kiswahili yanabadilika kama vile Yesu. Jina lake hasa la kule alikotokea halitumiki. Au nabii Musa. Lakini kuna mengine yanabaki vile vile. Sasa katika vitabu kadhaa vya Kiswahili ambavyo nimewahi kuvipitia, nimeona jina lake limechukua kanuni fulani za Kiswahili (kwa mfano badala ya kuishia na "s" pekee ikaongezwa "i" kuwa Abunuwasi). Lakini hii inafanya jina hilo kuwa moja wakati ambapo katika maelezo yako ni kuwa haya ni majina mawili (sio?). Sasa tunaweza kuchukua vile Waswahili walivyotamka na kuandika jina lake au tukachukua jina lake halisi, ambapo itakuwa ni majina mawili kama ulivyoandika. Tunachoweza kufanya naona ni kuandika jina lake hasa (yaani lake na la ubini) kisha tukaeleza kuwa Waswahili wamekuwa wakimwita Abunuwasi. Unasemaje?

Asante kwa jibu la haraka. Kimsingi mimi naona Abunuwasi (jamaa wa kifasihi) wa "Riwaya" na mshairi Abu Nuwas (mtu wa kihistoria) si yeye yule.

Abu Nuwas alitoa jina lake kwa Abunuwasi (au labda zaidi: jina lake limechukuliwa) - hadithi zile za Abunuwasi zimesimuliwa kati ya Waturuki juu ya Nasreddin na kati ya Waarabu wengine juu ya Guha (ninaandaa makala nyingine kuhusu Riwaya nitakapoeleza uhusiano huo).

Lakini hadithi za Riwaya hazina uhusiano na Abu Nuwas wa kihistoria. Hapo sababu yangu ya kuwataja pekee.

>> Ninahamisha majidiliano yetu kwenye ukurasa ya Abu Nuwas - sawa? ----Kipala 13:07, 6 Januari 2006 (UTC)Reply

Kipala, nimekupata sawasawa sasa. Nashukuru. Nilichanganya mambo. Nakupa pongezi tena kwa kazi zako. Tuendelee.


Maajabu ya Kwanzaa

hariri

Ndesanjo hujambo! Baada ya kusoma makala kuhusu Kwanzaa ninegependa kukuuliza kuhusu Kwanzaa jinsi unavyoiona ukiwa Mwafrika na Mwsahili. Nimetazama desturi hii kwa miaka kadhaa nikiwa mbali nikashangaa. Kwangu ilikuwa wazi ya kwamba sherehe hii haina kitu cha kiafrika ndani yake. Wala Afrika ya mashariki wa magharibi nimesikia ya kwamba kuna sikukuu ya mavuno wakati wa Disemba.

Kiswahili wanachotumia - basi naiona mtandaoni tu. Lakini kama ningemjibu mtu anayenisalimu "Habari gani" kwa maneno kama "kuumba" sijui angeniangalia namna gani.. Ama ataona nimesahau lugha au atajiuliza kama nimelewa. Wanaweka mahindi wakiita "muhindi" (sina neno kuhusu mahindi - imekuwa kiafrika sawa jinsi kiazi imekuwa kiingereza au kijerumani ingawa zote zimetoka Amerika ya Kusini, hata kama Wachagga na Waganda wasingekubali kamwe :-)) - ila tu lugha bovu). Unajua wewe mahali Afrika penye sherehe ya "matunda ya kwanza"???

Kwangu imeonekana kama sherehe ya kisintetiki yaani isiyo ya asili kabisa. Ni kama ndoto nyingine tena juu ya Afrika: Waingereza wanaota ndoto zao za "Out of Africa", karne zilizopita wataalamu wa Ulaya walikuwa na ndoto hizi za "Washenzi watukufu". Afrika ilikuwa na bado ni mara nyingi kama skrini ya filamu watu wanapotupa picha zilizomo kichwani mwao. Lakini si Afrika yenyewe.

Kwa upande mwingine nimefikiri basi si kitu kibaya kama watu wanatafuta habari za Kiswahili hata kama njia ni potovu. Ikisaidia kueneza kwa lugha ya Kiswahili nifunge macho? (Juzi nimepita mahali mtandaoni wanapotaja majina kwa ajili ya watoto wakidai ni ya Kiswahili - taz. http://www.babynology.com/swahili-boynames-m100.html - natumaini ya kwamba kuna matokeo mazuri zaidi ya upendo ule wa Kiamerika wa lugha kuliko orodha hii!)

Juzi tu nimeona mara ya kwanza habari za huyu Karenga kuwa jina lake ni Ron Everett amekuwa na historia mbaya asiyopenda kukubali. Umewahi kukutana naye? Ameanza kujifunza Kiswahili siku hizi? Kujiita "Maulana" ili watu wote Marekani wanaamini ni neno la Kiswahili kwa ajili ya "mwalimu" ni ajabu nyingine kwangu.

Kwa hiyo - ningependa kusikia mawazo yako kweli! --Kipala 17:05, 8 Januari 2006 (UTC) (Nanakili haya kwenye majidiliano ya "Kwanzaa" - labda wenzetu wengine wana neno pia)Reply

Kalenda ya Juliasi

hariri

Ndesanjo, nimeona matatizo na makala ya Kalenda.. Tafadhali angalia: http://sw.wikipedia.org/wiki/Talk:Kalenda_ya_Juliasi --Kipala 21:05, 19 Aprili 2006 (UTC)Reply

Tuzo ya Nobel/Nobel

hariri

Ndesanjo, hujambo? Vema kukuona tena ulipotea kweli. Ombi: wakati wa kusahihisha tukumbuke viungo! "Tuzo ya Nobel" ilikuwa kiungo - "Nobeli" imekata kiungo. Ingekuwa vema kama ama unasahihisha viungo vyote au kukirudisha. --Kipala 12:21, 24 Juni 2006 (UTC)Reply

Narudia ombi la Kipala: Kwa vile umebadilisha herufi za viungo, umekata viungo hivyo. Sasa nimeongeza viungo vitano kwa tuzo za Nobel. Ukumbuke mara ijayo kuongeza viungo ambavyo herufi zake umevibadilisha. Asante! -- Oliver Stegen 08:47, 14 Agosti 2006 (UTC)Reply

jambo

hariri

hujambo bwana? habari gani? it's mike/gozar from Wikimania 2006 checking in (apparently i had an account registered on here already). anyways, i may at some point add images to existing articles or make basic starts for others. probably country pages or those from the "articles every wikipedia should have" list...if i can find it! are you still in boston or have you moved on? kwa heri na asante.--Gozar 00:42, 10 Agosti 2006 (UTC)Reply

mawasiliano na anwani

hariri

Ndesanjo, habari yako? Uliniomba nikutumie anwani yangu kupitia baruapepe. Je, umeipata? Sijasikia kutoka kwako. Wasalaam, Oliver Stegen 10:54, 2 Septemba 2006 (UTC)Reply

Kutafuta maneno - Kuunda templeti

hariri

Ndesanjo, naomba msaada wako pamoja na Waswahili wengine. Niko kwenye makala za kijiografia / jiolojia nikiona tatizo la kuchagua maneno.

Kwa sasa nahitaji maneno kwa kutaja tabaka mbalimbali ya muundo wa dunia. Tatizo ni ya kwamba Kamusi ya KAST haionyeshi maneno ya kutosha. Je una ushauri kwa yafuatayo:

  • crust - gamba la nje ? (KAST inataja "ganda" - lakini haina neno la "mantle")
  • mantle (inner & outer) - ganda la dunia? (ya nje na ya ndani)
  • core (inner & outer) - KAST inataja "masoka" (niliweka "kiini" kabla ya kuangalia kwenye KAST - natumaini Mswahili wa kawaida ameshasahau maana ya masoko=pepo mbaya) - nifuate KAST

Kwa hiyo nisaidie kati ya "gamba" na "ganda". Nikitumia ganda kwa sehemu ya nje kabisa ambayo ni imara imepoa (ile tunapoishi) nitumiaje kwa "mantle"? (KAST hawana kitu kile)

Lugha nyingi hutumia neno lilelile "mantle" - Warusi, Wapoland n.k. wameitafsiri tu - je nikichukua "johoo" ?? au "koti" ?? Waturuki wamepokea neno la Kiitalia/Kifaransa "manto" (nijaribu ile?? Kuazima kutoka nje si aibu)

Naona vema kuwa na templeti ya kuonyesha: "Makala hii inatumia neno ambalo matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotaja. Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao."

Je, unaonaje?? --Kipala 21:02, 2 Septemba 2006 (UTC)Reply

Maswali magumu Kipala. Unaonaje nikiweka maswali haya pale kwenye kamusi hai mtandaoni? Binafsi ninapendelea "gamba" zaidi ya "ganda." Na "kiini" zaidi ya "masoka". Sioni ubaya kwenye kuazima neno na hivyo kutumia "manto." Unaonaje tukiuliza? --Ndesanjo

Ni vizuri ukiuliza. Labda itawavuta wengine katika mradi huu. "Koti" unaonaje? Vipi wazo la Templeti na maneno yake? --Kipala 21:53, 2 Septemba 2006 (UTC)Reply

Nilisahau kuhusu templeti. Ni wazo zuri sana. Tafadhali fanya.Itasaidia kwa kazi nyingine zinazoendana na hii unayoandika sasa. -Ndesanjo 2 Septemba 2006

Kumasi

hariri

Ndesanjo, asante kwa kunyosha Kiswahili changu! Miaka ya Nairobi imeniharibu!!! Kubaya mingi!! Lakini kiti kile cha Asantehene: je siyo "kigoda" huwa na miguu mitatu?? Muundo wa viti vya Ghana ni tofauti! Sina uhakika kinaitwa nini kwa Kiswahili hivyo nimetumia "kikalio". Angalia picha hapa: [[2]] --Kipala 20:40, 3 Septemba 2006 (UTC)Reply

Nilisahau kuwa kile hakina miguu kama ile ya kigoda, ni sawa tuiite kikalio. Ngoja nibadili.--Ndesanjo

Misitu na jangwa

hariri

Ndesanjo, umependekeza jamii: Vita vya msituni Afrika. Labda utafute jina nzuri zaidi. Nisipokosei vita ya POLISARIO au vita za Watuareg katika Sahara ni jambo lilelile - ila tu wanapigana jangwani pasipo na msitu kabisa. (Kwa Savimbi na Kony/LRA pekee ingekuwa sawa.) --Kipala 11:23, 11 Septemba 2006 (UTC)Reply

Ombi la ufutaji wa makala

hariri

Ndesanjo, hujambo? Naomba ufute makala hii: Insert text. Haieleweki inarejea nini, na jina lake ni Kiingereza. Asante, --Oliver Stegen 08:53, 22 Januari 2007 (UTC)Reply

Greetings from the Midwest

hariri

Ndesanjo, warm greetings from Dr A and me. It's beautiful to see you name and then (Sysop). Can you Email me? katewill at umich.edu -- I want to know if you will speak in my class of library school students about Wikipedia. They are in training to be wikipedian-librarians. Of course there is much more to say, so let's talk. 69.211.15.179 02:27, 6 Februari 2007 (UTC) (oh my, i just learned that my english wikipedia ID katewill doesn't log me in here.)Reply


Tufunge uhariri kwa wale waliojiandikisha?

hariri

Napendekeza kufungs uharitri wa makala kwa watumiaji waliojiandikisha. Uhalifu wote hadi sasa ilikuwa ya watu bila jina. Leo nilirudisha "Msaada wa kuanzisha makala" baada ya uhalifu. Hatujakuwa na matatizo mengi bado lakini ilhali tuko wachache inasumbua hata hivyo. Wasimamizi wenzangu: Je kuna tatizo lolote tukitaka kuruhusu uhariri wote kwa waliojiandikisha tu? (Naomba jibu kwenye ukurasa Wikipedia:Jumuia) --Kipala 21:00, 27 Februari 2007 (UTC)Reply

Tovuti

hariri

Ndesanjo, karibu tena. Umepotea sana. Naomba uangalie swali la lugha katika mambo ya kompyuta. Makala yetu ni "tarakishi"; wewe umetumia "tarakilishi". Je ni sawa kutumia yote miwili? Kama ndiyo naombe uweke redirect. Na tuongeze kamusi ya Yale. --Kipala 19:40, 1 Julai 2007 (UTC)Reply

Muziki ya Bongo

hariri

Ndesanjo, asante kwa kuangalia makala hizi za wanamuziki, naomba unendelee. Kwa upande mmoja nimefurahia ya kwamba tumepata wimbi ya watu wa TZ walioamua kujiandikisha - ingawa kwa upande mwingine yaonekana sababu muhimu ni wameona safi kujitangaza. Sehemu ya makala hizi zingefutwa moja kwa moja katika wikipedia nyingine - hapo kwetu naona ni vizuri kama wenyeji wa EA washiriki hivyo tusiangalie makala kwa ukali mno. Lakini mimi mwenyewe sina ujuzi sana katika ambo ya Hiphop n.k. hivyo nimefurahia ya kwamba wewe umechukua hatua. Naomba uendelee! --Kipala 22:49, 23 Agosti 2007 (UTC) )Reply

Kimya Kingi Mufti

hariri

Habari Ndugu Ndesanjo, Mbona kimya mkubwa hata kwenye majadiliano sikuoni vipi Sheikh au majukumu. tafadhali naomba uangalie sehemu ya kurasa mpya uangalie makala nilitengeneza kisha unifamishe kama zipo sahihi, ni hayo sina mengi nipo na mzee User:Kipala ananizidi kunipa Darasa zaidi. Muddyb Blast Producer 16:25, 17 September 2007 (UTC)


Uchaguzi

hariri

Kuna mapendekezo mapya kwa Wakabidhi na bureaucrat. Naomba angalia ukurasa http://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Wakabidhi --User_talk:Kipala 08:35, 1 Februari 2008 (UTC)Reply

Uteuzi mpya

hariri

Kuna pendekezo jipya kwa bureaucrat. Naomba uangalie ukurasa wa wakabidhi. --Oliver Stegen 09:15, 1 Machi 2008 (UTC)Reply

Karibu tena

hariri

Ndesanjo naona umepatwa na ufufuo hapa sw-wiki. Karibu tena na ukae tu kidogo! Ni vizuri kama Mswahili anafagilia makala. --Kipala (majadiliano) 13:23, 27 Mei 2008 (UTC)Reply

Mwanaharakati awe bureaucrat

hariri

Nimemteua Mwanaharakati achaguliwe kuwa msimamizi mkuu pamoja nasi (b'crat). Naomba upige kura kwenye ukurasa wa wakabidhi. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 07:17, 28 Mei 2009 (UTC)Reply

Kuondoa haki za usimamizi kwa baadhi ya watumiaji

hariri

Ndesanjo, salam! Unatakiwa utoe mawazo yako juu ya kuondoshwa kwa haki za usimamizi kwa baadhi ya watumiaji wasionekana kwa kipindi kirefu sana. Orodha hiyo unaweza kuipata hapa. Ahsante na kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 16:15, 10 Julai 2009 (UTC)Reply

mradi wa Google kwa ajili ya wikipedia yetu

hariri

Bwana Ndesanjo, salaam!
Nimepata mawasiliano kutoka Christine Moon huko Palo Alto, California. Yeye anafanya kazi kwa shirika la Google, nao wameanza kupanga mradi au huduma kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania na Kenya ili waelimishwe kuandika makala kwa wikipedia ya Kiswahili. Kumbe!
Christine sasa ametualika kumwandikia maoni yetu, angalia tovuti hiyo:
http://docs.google.com/Doc?docid=0AbIPJ9Nv6udZZGd6MndwcGdfMzFkODNzOG0zYw&hl=en
Bahati mbaya yeye haelewi Kiswahili, kwa hiyo itakuwa lazima kumwandikia kwa Kiingereza. Ukihitaji msaada wangu upande wa kumwandikia, karibu unijulishe. Asante kwa michango yako!
Ni wako katika ujenzi wa lugha yetu, --Baba Tabita (majadiliano) 07:58, 10 Oktoba 2009 (UTC)Reply

mkutano wa Skype kesho kutwa

hariri

Ndugu Ndesanjo, salaam! Jumatatu tarehe 19, saa kuminamoja za mchana/jioni (yaani saa za Nairobi) tutajaribu kukutana kwenye Skype kwa ajili ya majadiliano kuhusu kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Kenya na Tanzania kutumia na kuichangia makala wikipedia ya Kiswahili. Mpaka sasa tupo wanne: Christine wa Google (mooncheech), Sj (metasj), Muddyb (mohammed.lupinga) nami (stegling). Ni tumaini langu kuwa utakuwepo. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 18:58, 17 Oktoba 2009 (UTC)Reply

majadiliano kuhusu utafsiri wa istilahi

hariri

Ndugu Ndesanjo, salaam! Nimeanzisha majadiliano mapya kuhusu utafsiri wa istilahi ya wikipedia yetu hapa. Naomba uyaangalie na kuchangia maoni yako. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 09:40, 23 Oktoba 2009 (UTC)Reply

Semina ya Google katika UDSM

hariri

Ndesanjo, salam! Eti, nimepata ujumbe unaoelezea kwamba kutakuwa hakuna intaneti katika eneo tutakalokuwa tunatoa dahwa hizo. Je, hiyo unadhani itakuwa msaada zaidi kwa wale tutakaokuwa tunawaeleza?--  MwanaharakatiLonga 08:01, 21 Novemba 2009 (UTC)Reply

Uchaguzi Mpya

hariri

Salam, Ndesanjo. Unaombwa upige kura katika ukurasa wa wakabidhi wa Wikipedia. Mmoja kati ya wachangiaji wenzetu (Mr Accountable amejiteua kuwa mkabidhi! Ili kumpgia kura, tafadhali fungua hapa. Ahsante sana.--  MwanaharakatiLonga 18:34, 28 Novemba 2009 (UTC)Reply


Kura ya kuamua juu ya wakabidhi waliopotea

hariri

Karibu kutembelea ukurasa wa wakabidhi na kuamua juu ya wenzetu waliopewa haki za wakabidhi lakini hawakuonekana tangu miezi mingi: Wikipedia:Wakabidhi#Kura_ya_kuondoa_wakabidhi_waliopotea. Tuliwahi kujadili swali hili mwaka uliopita (tazama kwenye ukurasa unaotajwa, juu ya pendekezo) ; sasa njia imeonekana. Kipala (majadiliano) 05:31, 1 Oktoba 2010 (UTC)Reply


Pendekezo kuhusu utaratibu wa kuanzisha makala kwa watumiaji waliojiandisha pekee

hariri

naomba usome hapa na fanya uamuzi wako: Wikipedia:Jumuia#Pendekezo:_Utaratibu_wa_kuanzisha_makala Kipala (majadiliano) 14:58, 26 Novemba 2012 (UTC)Reply

Kupakia mafaili, Sogora ya kupakia?

hariri
 

Hello! Sorry for writing in English. As you're an administrator here, please check the message I left on MediaWiki talk:Licenses and the village pump. Thanks, Nemo 19:22, 18 Septemba 2014 (UTC)Reply

furaha kubwa

hariri

Naona umerudi, Ndugu - karibu sana tena! Tumefurahi tukisonga mbele pamoja. Salaam nyingi, --Baba Tabita (majadiliano) 09:26, 27 Aprili 2015 (UTC)Reply


Tafadhali uangalie jamii kuhusu mfumo wa kuanzisha makala

hariri

Mpendwa, nakuomba kuaangalia ukurasa wa Jumuiya. Tuliomba wikimedia ya kutpa mfumo wa kuzuia watumiaji wasiojiandikisha wasianzise makala mapya. Kusudi lilikuwa kupunguza idadi ya makala mabaya yasiyotosheleza masharti ya wikipedia ilhali tuko wachache mno kuziangalia. Wikipedia kubwa kadhaa zinatumia utaratibu huu (kama en:wikipedia) lakini sisi tunapaswa kupeleka ombi kwa kamati fulani. Kamati hii wametupa nafasi kwa kipindi ha miezi 6 tu inayokwisha karibuni. Sasa wanakamati wamekuja wanadai tujieleza au watarudisha mfumo huu nyuma. Mimi nikiwa 1 kati ya wachache wanaochugulia makala mapya naona itaturudisha nyuma. Naomba mchangie! Sanaaaaa!! Kipala (majadiliano) 23:40, 10 Septemba 2015 (UTC)Reply

Famouse Ukrainian People or maarufu Kiukreni

hariri
Hello Ndesanjo! Sorry for writing in English. I don`t understand Swahili. I ask you to contribute with translation into the Swahili language. Could you or other users of your wikipedia translate some articles, that dedicated for prominent figures in Ukraine. The list shown on the page Wikipedia:Makala zilizoombwa. It is equipped interlanguage links and given pronunciation on Latin alphabet.--Yasnodark (majadiliano) 11:36, 10 Aprili 2016 (UTC)Reply

Karibu tena!

hariri

Hatimaye! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:47, 29 Agosti 2017 (UTC)Reply

Karibu tena!

hariri

Ndugu Ndesanjo, habari? Karibu sana kwa kurudi baada ya muda mrefu. Tumefurahi kukuona humo kwetu. Tukazane kusonga mbele pamoja katika kukuza wikipedia ya Kiswahili (na matumizi yake mtandaoni). Wasalaam,--Baba Tabita (majadiliano) 08:19, 29 Septemba 2017 (UTC)Reply

Karibu tena!

hariri

Nisijekuonekana mwanga bure! Karibu sana, ndugu. Ukimya wako umekithili.. Lakini ni miongoni mwa waanzilishi na waendelezi bora kabisa wa Wikipedia hii! Karibu tena na tena!--MwanaharakatiLonga 08:31, 3 Oktoba 2017 (UTC) Reply

Kweli ndugu Mwanaharakati. Ukimya ulikolea sana. Sasa tumerudi kwa nguvu mpya. Ni kazi tu kama Magufuli! Muziki unaendaje?--Ndesanjo (majadiliano) 07:32, 18 Oktoba 2017 (UTC)Reply
Mzee wangu salaam. Unisamehe kwa ukimya wangu. Nilikuwa sijaona kama umejibu. Eh, kweli, umerudi kwa kasi. Labda usemi wa hapa kazi tu, unafaa kwa sasa. Kuhusu muziki, unaendelea vizuri. Siandiki mengi kuhusu siasa na mengineyo isipokuwa muziki! Umenitupa sana, kaka. Sasa naona heri tuongee kwenye simu. Unaonaje ukinitafuta humu: 0713538427. Miaka 10 sasa bila maongezi ya sauti itakuwa haifai isitoshe sisi sote wa nyumbani!--MwanaharakatiLonga 12:03, 4 Novemba 2017 (UTC)Reply

Vipi! (jibu)

hariri

Tupo! Asante kwa ujumbe. Kwa mabaki ya mwaka huu natumai kuwa na raha baada ya miezi saba ya kusafiri duniani: Uhabeshi, Uskoti, miji mbalimbali Ujerumani, Tanzania, Uholanzi na hatimaye Marekani. Tena tulikuwa na ndoa, binti ameolewa mwezi uliopita. Raha tele! :) Ukae salama! --Baba Tabita (majadiliano) 10:04, 6 Oktoba 2017 (UTC)Reply

Umekuwa Baba Tabita Mtembezi. Kweli umetembea. Hongera sana sana kwa ndoa ya binti!--Ndesanjo (majadiliano) 07:34, 18 Oktoba 2017 (UTC)Reply
Asante! Bila shaka hujatimiza matembezi yako mwenyewe. Au vipi? --Baba Tabita (majadiliano) 11:13, 18 Oktoba 2017 (UTC)Reply

Makala mapya - jamii na interwiki

hariri

Salaam Ndesanjo, naona umeanzisha makala kadhaa. Karibu! Naomba usisahau kupanga kila makala katika jamii (category) zake halafu ongeza "lugha - add links" (kushoto chini dirishani). Nimefanya hii kwa makala kadhaa lakini "Kunyanyua vyuma‎" inanishinda. Hii ni muhimu, kwanza utaona mwenyewe kama mada yako iko tayari kwa jina nyingine, tena inawasaidia wasomaji wanaopenda kupata habari za nyongeza kupitia lugha nyingine kama Kiingereza. Kipala (majadiliano) 21:49, 16 Oktoba 2017 (UTC)Reply

Asante ndugu. Najaribu kidogo, wakati mwingine haraka haraka, muda kidogo. Polepole ndio mwendo. Asante kwa kunikumbusha mambo haya muhimu. Muda unajua ulipita kidogo. Nikumbushe kidogo tena juu ya hii unayosema chini ya dirisha. Halafu unatumia Skype? --Ndesanjo (majadiliano) 05:00, 17 Oktoba 2017 (UTC)Reply
Naomba uangalie hapa: Wikipedia:Mwongozo_(Viungo_vya_Wikipedia). Skype niko kwa jina Ingo Koll Kipala (majadiliano) 08:16, 17 Oktoba 2017 (UTC)Reply

Kamafleji

hariri

Ndesanjo salaam! Hatujaongeana nafikiri. Ninafurahi kuona kama umerudi kuchangia makala mpya. Na asante kwa masahihisho na maboreshaji yako ya makala zangu. Lakini kwa nini uliandika "mabakamabaka ya kijani" katika makala ya nondo (mdudu) nyuma ya neno kamufleji? Nondo si vifaru au magari ya deraya. ChriKo (majadiliano) 20:11, 21 Novemba 2017 (UTC)Reply

Umenichekesha asubuhi hii. Eti nondo sio magari ya derayaǃ Ni kweli. Unajua nilidhani kuwa mabakamabaka linatumika hata kwa wanyama, wadudu au zile nguo za kijeshi. Sina kamusi ya karibuni. Neno kamafleji ndio linatumika? Ngoja nitabadili. --Ndesanjo (majadiliano) 06:29, 22 Novemba 2017 (UTC)Reply
Asante Ndesanjo. Ndiyo, kamafleji iko katika kamusi ya TUKI. ChriKo (majadiliano) 15:22, 22 Novemba 2017 (UTC)Reply
Asante kwa elimu. Nilishabadilisha asubuhiǃ --Ndesanjo (majadiliano) 15:40, 22 Novemba 2017 (UTC)Reply

Jenga Wikipedia ya Kiswahili

hariri

Salaam, je unapenda kushiriki katika kundi letu la meta:Jenga Wikipedia ya Kiswahili?? Karibu! Kipala (majadiliano) 11:36, 21 Februari 2018 (UTC)Reply

Sherehe!!!

hariri

Angalia hatua aliyoifikisha Ndugu Riccardo: Matukio ya hivi karibuni. Sherehe!!! --Baba Tabita (majadiliano) 10:03, 17 Machi 2018 (UTC)Reply


Amboseli

hariri

Ndugu, mradi umechangia makala juu ya hifadhi hiyo, nakuuliza kama ziwa Amboseli na ziwa Ambussel ni lilelile au mawili tofauti. Asante na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:33, 6 Juni 2018 (UTC)Reply

Mimi mzima. Ninajua tu ziwa Amboseli. Ziwa Ambussel liko wapi?Ndesanjo (majadiliano) 07:32, 10 Juni 2018 (UTC)Reply

Jenga Wikipedia

hariri

Naone umerudi tena kidogo. Sasa nimekukaribisha kujiandiksha ktk kundi letu la meta:Jenga Wikipedia ya Kiswahili. Unaonaje? Hili ni kundi la kupanga na kushauriana kuhusu mielekeo ktk Wikipedia ya Kiswahili. Kipala (majadiliano) 09:55, 20 Juni 2018 (UTC)Reply


Mkabidhi mpya. pendekezo

hariri

Naomba angalia hapa Wikipedia:Jumuia#Mkabidhi_kwa_Jadnapac. (Halafu: je ungekuwa na nafasi ya kuja Dar mwisho wa Novemba Ijumaa-Jpili kwa warsha ya hapa? basi niandikie email) Kipala (majadiliano) 21:37, 30 Oktoba 2018 (UTC)Reply

Nimekujibu ndugu kwenye email. Umeipata?--Ndesanjo (majadiliano) 01:33, 13 Novemba 2018 (UTC)Reply

Jumiya

hariri

Habari Ndesanjo, naona ulitunga makala ya Amazon (kampuni). Je unaweza kutunga makala ya en:Jumia ambayo imekuwa no.1 katika Afrika? Nimeona leo makala za magazaeti kwa sababu Fatouma Ba (mwanzilishaji wa Jumiya huko Cote d'Ivoire alipata sasa tuzo fulani pia atahubiria pale Davos. Wako pia Tanzania sina uhakika muhimu kiasi gani lakini mimi napitilia mara nyingi kabla ya kununua kitu ili nipate picha ya bei yake. Naona kama umeshaanza msamiati wa mambo haya afadhali uendelee. Kipala (majadiliano) 06:44, 22 Januari 2019 (UTC)Reply

Ni kweli ni kampuni kubwa sana Afrika sasa. Basi nitafanya hivyo.--Ndesanjo (majadiliano) 15
48, 24 Januari 2019 (UTC)
Just a minor correction: it's Jumia, not Jumiya. I thought it best to clarify this now so that if indeed its article is to be created, it'd be with the correct spelling :-) --Abbasjnr (majadiliano) 16:59, 24 Januari 2019 (UTC)Reply

Document your culture with Wiki Loves Love 2019 and win exciting prizes!

hariri
 

Please help translate to your language

Africa has many beautiful festivals, ceremonies and celebrations of love and we need your help to document these! They are the core part of African culture and in order to make sure this way of life followed by our ancestors remain among us, we need to have them online to make sure they are preserved. Join hands with Wiki Loves Love that aims to document and spread how love is expressed in all cultures via different rituals, celebrations and festivals and have a chance to win exciting prizes!! While uploading, please add your country code in the Wikimedia Commons upload wizard. If you want to organize an on-site Wiki Loves Love event, then contact our international team! For more information, check out our project page on Wikimedia Commons.

There are several prizes to grab. Hope to see you spreading love this February with Wiki Loves Love!

Imagine...The sum of all love!

Wiki Loves Love team 07:34, 4 Februari 2019 (UTC)

Email

hariri

Habari, nilipotaja email nilimaanisha: unaweza kubadilisha settings za akaunti yako ya mtumiaji hapa wikipedia na kuruhusu mawasiliano kwa baruapepe. Ukitazama ukurasa wangu utaona upande wa kushoto chini ya "Vifaa" pa mstari "Email this user". Hapa sionyeshi anwani yangu kwa watu wote lakini kila mtu anaweza kuniandikia. LAbda na wewe ubadilishe settings hizi kwako? Kipala (majadiliano) 09:47, 29 Juni 2019 (UTC)Reply

Asante. Kumbe sikukuelewa. Ngoja basi nitafanya. Na kamusi nimeipata. Nashukuru. --Ndesanjo (majadiliano) 03:10, 30 Juni 2019 (UTC)Reply

Community Insights Survey

hariri

RMaung (WMF) 00:47, 7 Septemba 2019 (UTC) Reply

Reminder: Community Insights Survey

hariri

RMaung (WMF) 18:56, 20 Septemba 2019 (UTC) Reply

Reminder: Community Insights Survey

hariri

RMaung (WMF) 15:11, 4 Oktoba 2019 (UTC) Reply


Ukaguzi wa orodha ya wakabidhi

hariri

Mpendwa, jina lako linapatikana kwenye orodha ya wakabidhi wa Wikipedia ya Kiswahili. Ilhali tutakagua orodha hiyo karibuni, nataka kukuuliza kama uko tayari kufanya kazi hii pia wakati ujao, pamoja na kushiriki katika shughuli za kuwa mkabidhi / admin. Naomba jibu lako ama kwa baruapepe kwangu au kwenye ukurasa https://sw.wikipedia.org/wiki/Majadiliano_ya_Wikipedia:Wakabidhi. Ndimi wako Kipala


Wakabidhi wenzangu,

tunahitaji kupeleka ukaguzi wa orodha ya wakabidhi tena mbele ya jumuiya. Kabla ya kuitagangaza hatua hii naomba tuelewane kwanza kati yetu kuhusu mambo mawili

1. Nani atapiga kura kati ya wanawikipedia? Pendekezo langu:

   a) Mwenye kura awe aliyewahi kuandikishwa tangu mwezi 1 (hatutaki waliojiandikisha jana kwa kumpiga kura rafiki leo)
   b) aliyewahi kuhariri makala 3 kwenye swwiki (nje ya ukurasa wake mwenyewe; hatukubali watu walioingia kwa kutunga/kusahihisha makala 1 pekee)
   c) aliyehariri katika miezi 12 kabla ya kura yetu

Zamani tulikuwa wachache sana lakini siku hizi idadi ya waliojiandikisha imeongezeka ingawa wengi hawafanyi kitu tena, kwa hiyo tuelewane.

2. Kuhusu orodha ya wakabidhi kuna matatizo mawili: a) tunaendelea kutunza majina ya wengine ambao ama hawakushiriki kabisa tangu miaka, au hawakushiriki katika shughuli za usimamizi. (hapa nitamwandikia kila mmoja na kumwuliza kama yuko tayari kutekeleza shughuli za admin: kupitia mara kwa mara ukurasa wa Mabadiliko ya Karibuni, kuangalia makala mpya na mabadiliko, kufuta spam dhahiri, kupeleka makala zisizofaa kwenye ukurasa wa ufutaji, kushiriki katika ufutaji, kukaribisha wageni) LAKINI tunahitaji watu zaidi walio tayari kufanya kazi hii

b) tuelewane nipeleke swali namna gani:

   ama tufute tu wale wasioshiriki tena na kuchagua wapya wa nyongeza (wale wanaofanya kazi waendelee tu)
   AU tufanye uchaguzi mpya kwa wote . Jambo hili si dhahiri na miradi ya wikipedia ziko tofauti hapa.

Naomba majibu kwenye ukurasa wa majadiliano ya wakabidhi. https://sw.wikipedia.org/wiki/Majadiliano_ya_Wikipedia:Wakabidhi

Ndimi wenu Kipala

kuhusiana lugha yangu

hariri

mimi ni mwongeaji mzuri wa kiswahili lakini nina shida, ni kama mimi naonewa kama mtu ambaye naongea lunga nyingine tafadhali nisaidie na suluhisho

Email

hariri

Habari zako, tafadhali uwezeshe Email katika mpangilio wa akaunti yako (angalia https://meta.wikimedia.org/wiki/Help:Preferences jinsi ya kuiwezesha). Ni muhimu wakabidhi wapatikane kwa njia hiyo pia kwa watumiaji wetu.

Kipala (majadiliano) 06:31, 1 Desemba 2020 (UTC)Reply

How we will see unregistered users

hariri

Hi!

You get this message because you are an admin on a Wikimedia wiki.

When someone edits a Wikimedia wiki without being logged in today, we show their IP address. As you may already know, we will not be able to do this in the future. This is a decision by the Wikimedia Foundation Legal department, because norms and regulations for privacy online have changed.

Instead of the IP we will show a masked identity. You as an admin will still be able to access the IP. There will also be a new user right for those who need to see the full IPs of unregistered users to fight vandalism, harassment and spam without being admins. Patrollers will also see part of the IP even without this user right. We are also working on better tools to help.

If you have not seen it before, you can read more on Meta. If you want to make sure you don’t miss technical changes on the Wikimedia wikis, you can subscribe to the weekly technical newsletter.

We have two suggested ways this identity could work. We would appreciate your feedback on which way you think would work best for you and your wiki, now and in the future. You can let us know on the talk page. You can write in your language. The suggestions were posted in October and we will decide after 17 January.

Thank you. /Johan (WMF)

18:19, 4 Januari 2022 (UTC)

Have you voted in the UCoC enforcement guidelines ratification?

hariri

Hi! @Ndesanjo:

The ratification voting process for the revised enforcement guidelines of the Universal Code of Conduct (UCoC) is now open! Voting commenced on SecurePoll on 7 March 2022 and will conclude on 21 March 2022. Please read more on the voter information and eligibility details.

Please vote and encourage other editors of Swahili Wikipedia to also vote.

Regards, Zuz (WMF) (majadiliano) 12:05, 11 Machi 2022 (UTC)Reply

Hali yako ya mkabidhi

hariri

Habari yako, katika orodha yetu ulikuwa mkabidhi wa swwiki. Tunashukuru sana kwa michango yako yote tangu kuingia hapa. Lakini hujaonekana tena tangu zaidi ya mwaka mmoja. Kufuatana na mapatano tuliyofanya mwaka jana, tumeamua kufuta hali ya mkabidhi kama yuko kimya kwa mwaka 1 au zaidi. Unakaribishwa kujibu kama kuna jambo. Kipala (majadiliano) 19:26, 5 Septemba 2022 (UTC)Reply

 

You have been a medical translators within Wikipedia. We have recently relaunched our efforts and invite you to join the new process. Let me know if you have questions. Best Doc James (talk · contribs · email) 12:34, 13 August 2023 (UTC)