Saa ya mkononi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
[[File:Campaign Watch 1915.jpg|thumb|right|Tangazo la saa iliyotengenezwa na [[Mappin & Webb]] mwaka 1898.]]
'''Saa ya mkononi''' ni [[kifaa]] ambacho hubebwa au kuvalishwa [[mkono|mkononi]] ambapo hueleza [[muda]].
 
Kuna saa za [[digitali]] na saa za [[mishale]].
 
Siku hizi matumizi yake yamepungua kwa sababu kuna vifaa vingine, kama [[simu ya mkononi]], ambavyo hufanya kazi ya kuonyesha wakati pia.
 
==Historia==
Dhana ya saa ya mkono ina historia ndefu toka wakati wa uzalishaji wa saa za mwanzo kabisa katika karne ya 16. [[Malkia Elizabeth I]] wa [[Uingereza]] alipokea saa ya mkono kutoka kwa [[Robert Dudley]] mnamo mwaka wa 1571.
 
Mwaka wa 1775 saa ilipatikana yenye uwezo wa kukaza [[kamani]] yake kwa nishati ya msuko suko wa mkono mtu akitembea na mpaka wa leo inatumika na watu wengi. Saa ya mkono ya zamani kabisa iliyopo hadi hivi sasa (iliyokuwa ikiitwa saa ya bangili) ilitengenezwa mwaka 1806. Mwanzoni saa za mkono zilikuwa zikivaliwa na wanawake tu, wakati wanaume walikuwa wakitumia saa za mfukoni hadi karne ya 20.<ref name="Evolu">{{cite web|url=http://www.vintagewatchstraps.com/wristwatches.html|title=The Evolution of the Wristwatch}}</ref>
 
Saa za mkono zilianza kuvaliwa na wanaume wanajeshi mwisho mwa karne ya 19 kwa ajili ya kupanga vyema vita. Kampuni ya Garstin ya London ilipata hati miliki ya "Watch Wristlet" mwaka 1893, lakini walikuwa wakitengeneza saa miundo kama hiyo tangu miaka ya 1880. Maofisa wa Jeshi la Uingereza walianza kutumia saa za mkonononi wakati wa kampeni ya kijeshi ya kikoloni katika miaka ya 1880, kama vile wakati wa [[Vita ya Anglo-Burma]] ya 1885.<ref name="Evolu" /> Wakati wa [[Vita ya kwanza ya Makaburu]], umuhimu wa kuratibu harakati za vikosi na kusawazisha mashambulizi dhidi ya [[Makaburu]] ulikuwa muhimu sana, na matumizi ya saa za mkono ulianza kuenea miongoni mwa maofisa wa kijeshi. Kampuni ya [[Mappin & Webb]] ilianza uzalishaji wa saa za wanajesho wakati huko Sudan mnamo mwaka 1898 na kuongeza kasi ya uzalishaji wakati wa [[Vita ya Pili ya Makaburu]] miaka michache baadaye. Katika bara la Ulaya kampuni ya [[Girard-Perregaux]] na kampuni nyingine za Uswisi zilianza kutengeneza saa za mkono za maofisa wa jeshi la Ujerumani mwaka 1880.
 
Kawaida ubora wa saa unahusishwa na mambo mbalimbali kama vile saa inavyoweza kuzuia maji. Shirika la Kimataifa la Usanifishaji (kwa kifupi ISO) limetoa vipimo maalum vya saa zinavyozuia maji.
 
Saa zaweza kugawiwa katika makundi mawili makuu kuzingatia kizazi; saa za zamani (analog) na saa za kisasa/za [[dijiti]] ambazo ni za [[Elektroni|kielektroni]].<ref>{{Cite Web|url=https://greatwatches.nyc/digital-vs-analog-which-is-better/|title=Digital vs Analog Watch - Which is Better?|author=Great Watches NYC|language=en-US|date=17 March 2018|work=Great Watches NYC|accessdate=10 July 2018}}</ref>
 
Pia zinaweza kugawiwa katika makundi saba kulingana na mtindo na utenda kazi:
 
* saa za kujiendesha (automatiki) - saa zisizo hitaji betri
* saa za kronogilafia ''(chronograph watches) -'' saa zijulikanazo kwa Kingereza kama ''"Stop-Watch"'' za kupimia mda mfupi hasa wakati tendo kama mbio zinafanyika
* saa zisizo na mengi ''(minimalist watches)'' - saa zisizo na marembesho mengi
* saa za quartz - saa zinazo tumia teknolojia ya quartz
* saa za kivazi - saa za kisanaa zinazolenga mvuto wa kipeee
* saa za kifahari - saa zenye bei ghali mno zinazoundwa kwa kulenga matajiri na mara nyingi huendana na vitu vya fahari kama magari na simu
* saa zinazotumia [[nishati ya jua]]
 
==Marejeo==
{{Marejeo}}
 
== Viungo za nje ==
* [https://greatwatches.nyc/digital-vs-analog-which-is-better Tofauti kati ya saa ya dijitali na saa za zamani]
* [https://greatwatches.nyc/atm-water-resistance/ Vipimo vya saa kuzuia maji]
 
* [https://www.nytimes.com/2013/10/23/fashion/wrist-watches-from-battlefield-to-fashion-accessory.html Historia ya saa toka kwenye uwanja wa vita hadi kwenye mitindo]
* [http://www.historyofwatch.com/ Historia ya saa ya mkono na saa ya ukutani]
{{tech-stub}}