Waiyaki wa Hinga : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
kuanzisha ukurasa
 
No edit summary
Mstari 1:
'''Waiyaki wa Hinga''' alikuwa [[mpiganaji]] na kiongozi wa [[Wakikuyu]] (''mũthamaki'') katika [[Kaunti ya Kiambu|Kabete ya kale]]<ref name=":2">{{Cite web|url=https://www.nation.co.ke/lifestyle/dn2/Andrew-Kuria-Waiyaki-wa-Hinga/957860-2441040-daot43z/index.html|title=122 years later, family seeks hero’s burial for Waiyaki wa Hinga|language=en|work=nation.co.ke|accessdate=2018-10-17}}</ref>. Aliongoza vita dhidi ya [[Wamasai]] na uasi dhidi ya [[wakoloni]]<ref name=":0">{{Cite book|url=https://books.google.co.ke/books?id=H5cQH17-HnMC&pg=PA905&dq=waiyaki+wa+hinga&hl=sw&sa=X&ved=0ahUKEwig1YLEio3eAhVlx4UKHcyFDhgQ6AEIJDAA#v=onepage&q=waiyaki%20wa%20hinga&f=false|title=Holy People of the World: A Cross-cultural Encyclopedia|last=Jestice|first=Phyllis G.|date=2004|publisher=ABC-CLIO|year=|isbn=9781576073551|location=|pages=905-906|language=en}}</ref>. Alikufa mwaka 1982, akiwa mikononi mwa wakoloni.
 
== Maisha ==
Hijulikani bayana mahali alipotoka au wakati alipozaliwa. Baadhi ya vizazi vyake husema kuwa alikuwa wa nasaba ya Wakikuyu ilhali baadhi ya wanahistoria wanaamini kuwa alikuwa Mmasai kutoka [[Ngong, Kenya|Ngong]] aliyekuwa amehama hadi [[Dagoretti]] kwa sababu ya [[maafa asilia]]<ref name=":1">{{Citation|last=Standard|first=The|title=How legend was buried alive for resisting takeover|url=https://www.standardmedia.co.ke/article/2000036058/how-legend-was-buried-alive-for-resisting-takeover|work=The Standard|language=en|access-date=2018-10-17}}</ref>. Waiyaki alipewa jina ''Hinga'', maana yake ikiwa [[Unafiki|mnafiki]], kwa sababu hakuwa na uwazi na alikisiwa kuwa [[jasusi]] kutoka kwa Wamasai. Wamasai pia hawakumwamini kwa kuwa alikuwa ameongoza vita dhidi yao na kuteka ng'ombe wengi. Jina Waiyaki linaaminika kutokana na neno Koiyaki kutoka Kimaasai<ref>{{Cite web|url=https://www.pressreader.com/kenya/daily-nation-kenya/20171028/282153586534540|title=PressReader.com - Connecting People Through News|work=www.pressreader.com|accessdate=2018-10-17}}</ref>.
 
Alikuwa tajiri aliyekuwa ameoa wanawake kumi. Kama kiongozi, alikuwa [[kabaila]] mwenye ushawishi mkuu. Makazi pake palikuwa na vijumba tofauti, vya bibi zake na kimoja cha wageni. Hapo ndipo walipatana na [[Frederick Lugard]] Oktoba 10, Mwaka 1890<ref name=":1" /><ref name=":0" />.
 
== Uasi na kifo ==
Lugard alikuwa na jukumu la kuhakikisha ushawishi wa [[Milki ya Uingereza|Uingereza]] na usalama wa [[Msafara|misafara]] ya wafanyabiashara katika [[Afrika ya Mashariki]]. Kwa sababu hiyo, alikuwa akitengeneza [[Mkataba|mikataba]] na makabila tofauti katika ziara ya kwenda [[Uganda]]. Kampuni aliyokuwa akifanyia kazi, [[IBEAC]], ilikuwa ikiasisi [[ngome]] njiani<ref name=":3">{{Cite web|url=https://www.businessdailyafrica.com/lifestyle/society/Oldest-edifice-of-colonial--era-left-to-rot-in-Kibwezi--/3405664-4363826-ralmoi/index.html|title=Oldest edifice of colonial era left to rot in Kikuyu|work=www.businessdailyafrica.com|accessdate=2018-10-17|}}</ref>. Waiyaki alikubali ngome, ambayo pia ilikuwa kituo cha misafara ya Waingereza, ijengwe katika ardhi aliyoitoa. Lugard alijenga ngome, mahali ambapo Kanisa la P.C.E.A la Kihumo limejengwa<ref>{{cite web|url=https://www.nakala.fr/data/11280/f0c7cbab|title=How pioneers set the pace|author=Wanjohi Mutunga|format=PDF|publisher=The Torch bearer|access-date=17 October 2018}}</ref><ref name=":1" />. Ili apatiwe shamba, Lugard alifanya mkataba na Waiyaki kwa njia ya [[uchale]]. Walikubaliana kwamba wazungu hawangenyakua ardhi au mali yoyote kutoka kwa Wakikuyu<ref name=":0" />.
 
Mwezi mmoja baada ya Lugard kuendelea na safari yake, [[askari]] na [[Mchukuzi|wachukuzi]] walioachwa chini ya usimamizi wa [[George Wilson]] walianza kuvamia mashamba ya wenyeji na kuiba mazao ya shamba, [[mifugo]] na hata kuwanyanyasa[[Dhuluma|kuwadhulumu]] wanawake<ref name=":1" /><ref name=":3" />. Matukio hayo yaliwakasirisha sana wenyeji. Waiyaki aliongoza shambulizi katika ngome hiyo, mwaka [[1891]]. Walipofika katika ngome, walipata kuwa George na wadogo wake walikuwa wametoroka kwa kuwa walikuwa wameonywa kuhusu shambulio hilo. Washambuliaji waliichoma ngome<ref name=":3" /><ref name=":1" />.
 
Mwaka [[1892]], msafara uliokuwa umeongozwa na [[Erick Smith]] ulitumwa [[Kabete]]. Smith alijenga ngome nyingine ambayo iliitwa [[Ngome ya Smith]] ([[Ing.|ing]]: ''Fort Smith'') bila idhini. Kulikuwa na vuta nikuvute kati ya wageni na wenyeji. Waingereza walikuwa wametumwa kulipiza kisasi kwa kushambulia kijiji cha [[Riuki]], [[Githunguri]]. Waiyaki aliwaonya wanakijiji, na wakaweza kuondoka pamoja na mifugo yao kabla ya shambulizi kutendwa. Waingereza walichoma vijiji 30 na kuharibu mazao ya mashamba<ref name=":2" />. Waiyaki alipoenda kulalamikia Waingereza katika Ngome ya Smith, alipatana na [[W. P. Purkis]]. Purkis alidai kuwa Waiyaki alikuwa amejaribu kumvamia kutumia kisu na kwa hivyo, Waiyaki akakamatwa<ref name=":4">{{Cite book|url=https://books.google.co.ke/books?id=XVPM53_gPP4C&pg=PA53&dq=fort+smith+waiyaki+wa+hinga&hl=sw&sa=X&ved=0ahUKEwjx4s2kso3eAhUkDsAKHX96C74Q6AEIJDAA#v=onepage&q=fort%20smith%20waiyaki%20wa%20hinga&f=false|title=History and Government Form 2|last=|first=|publisher=East African Publishers|year=|isbn=9789966253330|location=|pages=53|language=en}}</ref>. Baada ya kuteswa, alipelekwa katika [[mahakama]] ya muda, iliyokuwa kando ya ngome<ref name=":2" />. Mahakama ilimpata kuwa na kosa na akahukumiwa kuhamishiwa [[Mkoa wa Pwani (Kenya)|Pwani]].
 
=== Kuzikwa ===
Haijulikani bayana kilichomfanyikia alipokuwa katika msafara, ila tu hakuweza kuendelea na safari alipofika [[Kibwezi]]. Baadhi ya vyanzo husema kuwa msafara ulipofika Kibwezi, Waiyaki hangeweza kuendelea kwa kuwa alikuwa na majeraha mabaya kichwani<ref name=":4" />. Wengine husema kuwa alipigwa risasi. Rekodi rasmi zinaonyesha kuwa aliachwa katika hospitali ya misheni ambapo alifariki na akazikwa makaburini ya hospitali hiyo<ref name=":3" /><ref name=":2" />. Vyanzo vingine husema kuwa alizikwa hai, Agosti 17, mwaka 1891<ref name=":1" /><ref name=":4" /><ref>{{Cite book|url=https://books.google.co.ke/books?id=G0lBfbmYRf0C&pg=PA119&dq=waiyaki+wa+hinga+buried+alive&hl=en&sa=X&ved=0ahUKEwiH8NO_zI3eAhXMFsAKHSjcBuQQ6AEILTAB#v=onepage&q=waiyaki%20wa%20hinga%20buried%20alive&f=false|title=Africa and the West: From colonialism to independence, 1875 to the present|last=Worger|first=William H.|last2=Clark|first2=Nancy L.|last3=Alpers|first3=Edward A.|date=2010|publisher=Oxford University Press|year=|isbn=9780195373134|location=|pages=119|language=en}}</ref>.
 
== Marejeo ==
<references />
[[Jamii:Historia ya Kenya]]
[[Jamii:Wakikuyu]]