Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Sherehe!!!

hariri

Angalia hatua aliyoifikisha Ndugu Riccardo: Matukio ya hivi karibuni. Sherehe!!! --Baba Tabita (majadiliano) 10:13, 17 Machi 2018 (UTC)Reply

Unaombwa kuwasiliana!

hariri

Nafurahi kuona jinsi gani unavyochangia kwetu swwiki. Asante na karibu tena!. Lakini nakuomba sana usiwe haraka kuhamisha makala yaliyopo. Ile ya chansela-kansela labda haikuwa busara. Hujaonyesha sababu kwa nini unataka kuhamisha makala. Hapa lazima kutafakari pamoja, hasa kwa sababu lemma hii imeshatumiwa mara nyingi. Halafu ni LAZIMA uwasiliane na wengine. Uliulizwa swali kuhusu uhamisho huu na mwenzetu. Desturi kwetu ni ya kwamba tunajitahidi kupeana majibu. Kwa hiyo usikae kimya. Hasa ukiwa mgeni bado ni lazima kuwasiliana na wengine ili tupate kushauriana na kusaidiana. Ukiwa mgeni ni vema kuuliza swali kwanza na kutaja pendekezo na kueleza sababu zako. Usipopata jibu kwa siku kadhaa si kosa kuendelea. Kipala (majadiliano) 19:10, 27 Machi 2018 (UTC)Reply

Nakubali ilikuwa makosa kuhamisha kwa haraka. Wakati nilitambua kwamba ukurasa huo ulikuwa umeunganishwa na kurasa nyingine mingi, nilijaribu kusuluhisha kwa kutengeneza ukurasa wa 'maana'. Kuhusu swali, nilieleza sababu ya kuhamisha katika muhtasari. Baadaye nikagundua swali lililokuwa limeulizwa mbeleni katika sehemu ya majadiliano. Nashukuru mawaidha yako. Nitatilia maanani siku zijazo na kutathmini hatua kabla ya kutenda. Unja1234 (majadiliano) 09:12, 28 Machi 2018 (UTC)Reply
Asante kwa jibu. Wakati mwingine inaweza kutosha kutaja sababu kifupi tu kwenye muhtasari. Lakini mara nyingine na safari hii ingekuwa afadhali kusubiri majadiliano, hasa kama lemma imeshatumiwa mara nyingi. Pamoja na haya ukifanya utafiti lemma hii 1) haiko bado katika kamusi sanifu (niliyo nayo), 2) inapatikana kwa google search kwa maumbo yote mawili yaani Chansela na kansela, ingawa kwa sasa "kansela" ziko zaidi. Lakini kwenye maneno yasiyosanifishwa bado matumizi yanaweza kubadilika mwaka baada ya mwaka. Na hasa kama mifano ya google ni chache (kama hapa) hatuna takwimu ya kutegemea. Haya yote si msingi imara wa kubadilisha lemma. Katika wikipedia nyingine hapa kuna mara nyingi chanzo cha "edit war". Sisi tumefaulu kuepukana nayo kwa miaka yote kwa kuwasiliana kati yetu kwa heshima. Karibu kwenye ushirikiano! Kipala (majadiliano) 12:55, 28 Machi 2018 (UTC)Reply
Nashukuru. Nilikuwa najua tu kuhusu neno 'kansela' pekee kwa vile hutumiwa katika DW.
Hi si ajabu. DW ni sauti ya Ujerumani. Maana Wa-TZ na Wa-EAK wanaotunga matini za DW-Kiswahili pale Cologne wamejifunza Kijerumani wakitumia neno "Kanzler" au "Kanzlerin" (kike). Hata "chansela" ni utohoaji tu wa neno la Kiingereza. Asili yake ni Kilatini "cancellarius" kwa lugha zote za Ulaya. Ila labda njia ya kupitia Kiingereza itaeleweka rahisi zaidi kwa wasomaji wetu Afrika ya Mshariki. Ni vema kutaja maumbo yote mawili na kutumia redirect. Ninanakili sehemu ya chini kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala tusikie kama wengine wana neno kama ibaki Kansela caadaye kazi kwako kubadilisha makala zote) au irudishwe Chansela.Kipala (majadiliano) 19:29, 28 Machi 2018 (UTC)Reply

Kaunti za Kenya

hariri

Ndugu, hongera kwa kurasa zako nzuri na kwa maendeleo yako katika kuhariri. Naomba ukiwa Kenya, utuharirie kurasa za kaunti zake zote, kwa kuwa mpaka sasa Wikipedia imeishia katika mikoa na wilaya kama kabla ya katiba mpya. Asante sana na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:32, 29 Machi 2018 (UTC)Reply

Karibu. Nitazipitia. Unja1234 (majadiliano) 12:28, 29 Machi 2018 (UTC)#Reply


Lugard

hariri

Hongera ya makala ya Lugard!197.250.230.173 08:50, 6 Oktoba 2018 (UTC)Reply