Angahewa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Protected "Angahewa" ([Kuhariri=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho) [Kuhamisha=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho))
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Angahewa_tabaka.png|thumb|300px|right|Tabaka za angahewa ya dunia]]
'''Angahewa''' ni [[Tabaka|matabaka]] ya [[gesi]] za [[hewa]] yanayozingira [[sayari]] au [[Gimba la angani|gimba lingine la angani]] yakishikwa na [[Graviti]] ya gimba hilihusika.
 
==Angahewa ya Dunia==
Angahewa inakinga [[uhai]] [[duniani]] kwa kupunguza [[mnururisho]] wa [[urujianimno]] wa [[jua]], kutunza halijota[[halijoto]] duniani kwa kuakisisha [[mawimbi]] [[infraredi]], kupunguza tofauti kati ya [[baridi]] na [[joto]] na kuwapa [[wanyama]] na [[mimea]] viwango vya [[oksijeni]] na [[nitrojeni]] wanayohitajiwanavyohitaji.
 
Magimba ya angani mengine kama [[sayari]] au [[jua]] huwa pia na aina za angahewa ingawa gesi zake ni tofauti na za duniani.
 
Gesi zilizopo katika angahewa ya dunia ni hasa [[nitrojeni]] (78 [[%]]) na [[oksijeni]] (21 %) pamoja na viwango vidogo lakini muhimu vya [[arigoni]] (0.9 %), [[kaboni dioksidi]] (0.035 %), [[mvuke]] wa [[maji]] na gesi nyingine mbalimbali.
 
Angahewa haina mwisho kamili, ila inazidi kuwa hafifu jinsi inavyofikia juu. [[Asilimia]] 75 ya [[masi]] ya hewa yake iko katika [[tabakatropo]] hadi [[kilomita]] 11 juu ya uso wa dunia. [[Uzito]] wa hewa hupimwa kama [[mkandamizo hewa]].
 
== Halijoto na tabaka za angahewa ==
Sehemu za angahewa zina baridi au joto zaidi kutegemeana na [[kimo]]. Tukipaa juu ya uso wa dunia halijoto inazidi kuwa baridi, baadaye joto tena, kadiri jinsi tunavyopaa. Mabadiliko ya halijoto yanafuata muundo wa tabaka zinazootofautishwazinazotofautishwa na kiwango cha joto au baridi kinachopimwa.
 
Kwa jumla inawezekana kutofautisha tabakamatabaka 5 ambazoambayo ni
* [[Tabakatropo]] (troposphere) - inaanza kwenye uso wa dunia na kuishia mnamo kilomita 7 (juu ya ncha za dunia) - 15 (juu ya sehemu za [[tropiki]]) juu yake; baridi inazidi jinsi unavyopaa juu (kwa hiyo ni baridi mlimani kushinda chini); mawingu yako hapa na hii ni tabaka ambako [[halihewa]] inatokea.
* [[Tabakastrato]] (stratosphere) - inaishia kwenyi kimo cha 50 [[km]]; hapa joto linaanza kuzidi tena. [[Eropleni]] kubwa zinapita hapa kwa sababu hakuna upepo mwenye nguvu inayosumbua mwendo
Mstari 21:
* [[Tabakanje]] (exosphere) - ni tabaka la nje inayoanza kati ya 500- 1000 km na kuwa hafifu kadri unayopaa juu zaidi; inafikia kilomita maelfu hadi kwa kimo cha takriban 10,000 km ambako hewa haipimiki tena
 
TabakaMatabaka zaya juu, yaani tabakajoto na tabakanje, huitwa pia [[tabakaioni]] kwa sababu [[atomi]] za gesi zake zinapatikana katika hali ya [[ioni]] zilizopoteza [[elektroni]] kutokana na kupigwa na miale ya jua iliyo bado kali sana hapo nje.
 
==Angahewa kwenye sayari==
Nje ya dunia yetu angahewa imetambuliwa pia kwenye [[sayari]] nyingine. Katika [[mfumo wa jua na sayari zake]] kuna sayari 4 za ndani zinazofanana kiasi, ni [[Utaridi]] (Mercury), [[Zuhura]] (Venus), Dunia na [[Mirihi]] (Mars). Zote nne ni sayari zinazofanywa na [[mwamba]].
 
*Kati ya hizi Utaridi haina angahewa, ikiaminiwa yote imepotea kutokana na kupigwa vikali na [[upepo wa jua]] lililo karibu na sayari hii.
*Zuhura ina angahewa nzito, hasa ya [[dioksidi kabonia]] (CO<sup>2</sup>)
*[[Mirihi]] na angahewa hafifu sana ya dioksidi kabonia (CO<sup>2</sup>). Inaaminiwa kuwa imepotea asilimia kubwa ya angahewa yake. Mirihi haina [[uga sumaku]] na hivyo upepo wa jua unapiga sayari hii moja kwa moja na kusukuma [[molekyuli]] za angahewa mbali kwenda [[anga-nje]].
Sayari kubwa za nje kama [[Mshtarii]] (Jupiter) na [[Zohari]] (Saturn) si rahisi vile kuofautisha kati ya sayari yenyewe na angahewa yake. Sayari hizi huitwa pia "jitu za gesi" kwa sababu asilimia kubwa ya sayari yote ni elementi kama [[hidrojeni]] na [[heli]] ambazo kwetu duniani zinapatikana kama gesi. Kutokana na umbali mkubwa na jua ni baridi zaidi hadi gesi hizi kupitia katika hali mango. Vilevile hidrojeni katika kiini cha Mshtarii inaaminiwa kuwa katika hali metalia kutokana na shinikizo kubwa ya masi yake.