Tazama pia kurasa za muda: Viungo vya mwili na makala 100!

Majadiliano ya awali yamehamishwa kwenye kurasa za Hifadhi ya Nyaraka

Ongeza chako chini kabisa!

Kuhusu Wikipedia kwa simu

Watu wengi wako Afrika wanasoma wikipedia kwa simu. Wanaweza kuhusu kwa simu pia?

https://www.mediawiki.org/wiki/Wikimedia_Apps

https://translatewiki.net/wiki/Translating:WikimediaMobile

Benson Muite (majadiliano) 12:35, 28 Januari 2020 (UTC)

Asante kwa swali, Ndugu Benson. Tuna watumiaji wengi wanaochangia kwa simu. Inawezekana, pia kwa matokeo mazuri. Historia ya makala inaionyesha kwa "tag:Mobile edit". Kwa upande mwingine tuna tatizo hasa kwa watumiaji wapya wakiamua mara moja kubadilisha kitu kidogo au kuongeza hosa, sentensi au neno kwamba hariri zao zina makosa (au:hazina maana) kwa hiyo tunasafisha mara kwa mara. Si rahisi kuunda makala marefu kidogo kwa simu ya mkononi. Lakini uwezekano upo. Kipala (majadiliano) 12:55, 28 Januari 2020 (UTC)
Kutafsiri kwa kutumia msaada kama translatewiki inawezakana pia, mimi mwenyewe ninaitumia siku hizi mara kwa mara. Hata hivyo, watumiaji wapya wanaonywa dhidi yake. Maana inahitaji maarifa na umakini. Ni rahisi kuingiza makala marefu ya Kiingereza katika programu ya aina hii, kusahihisha kidogo makosa ya kwanza na kuihifadhi. Ila tu mara nyingi (hasa kwenye skrini ndogo ya simu) watumiaji wanachoka au hawaoni tena makosa mengine - yanayobaki. Ni kidogo kama samaki hizi zenye sumu zinazopendwa na Wajapani en:fugu - tamu sana, lakini ole ukisahau kukata sehemu za sumu! Kipala (majadiliano) 13:04, 28 Januari 2020 (UTC)

Kazi nzuri ya uhariri

Habari!

Umefanya vyema kuweka kielelezo kwenda Mapatano ya Kimataifa dhidi ya Utesaji.

BlessNathan (majadiliano) 13:56, 1 Februari 2020 (UTC)

Kuhusu kubadili jina la mtumiaji

Mimi Simon waziri msika naomba kubadili jina la mtumiaji na liwe 20_savage.Asante amani kwako--Simon waziri msika (majadiliano) 12:23, 7 Februari 2020 (UTC)kipala.

Mashindano ya Uhariri Alfagems

Ndugu, nipo na Magotech kwa ajili ya mashindano yetu. Afadhali usihariri makala zinazoundwa mpaka tutoe tuzo kwa washindi. Asante. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:28, 16 Februari 2020 (UTC)

Usiwe na wasiwasi, naona hiyo baada ya tukio.Kipala (majadiliano) 18:53, 16 Februari 2020 (UTC)

Ugatuzi Burundi

Ndugu, naona nchi hiyo ndogo imegawiwa sehemu 16 (provinces) ambazo tungeziita wilaya, si mikoa. Hasa kwa sababu kuna ngazi ya juu zaidi ambayo inafaa iitwe mkoa. Unasemaje? Kuhusu masahihisho yangu, nimekuelewa. Nitasubiri zaidi. Hofu yangu ni kusahau baadaye... Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 05:43, 17 Machi 2020 (UTC)

Asante, kama wenzetu wa enwiki wako sawa https://en.wikipedia.org/wiki/Burundi#Subdivisions, zile provinces za Burundi ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi wa nchi. Je umeona ngazi ya juu? Menginevyo fanya unavyoona. Nadhani tu ni busara tukianza kutaja kwa kila nchi makala yetu husika, ambayo ni Eneo la utawala; tafadhali uiangalie, unatumia neno hili zuri "ugatuzi", labda uhamishe lemma kwenda kule. Sasa naona tuktaja mfano "wilaya/mikoa ya Burundi", tuwe na makala fupi inayosema "Wilaya/mikoa ya Burundi" inayoeleza kwa sentensi moja "Wilaya/Mikoa ya Burundi ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi wa nchi. Nchi hiyo imegwanywa kwa wilaya/mikoa 17. Wil/Mkoa unagawanywa kwa ....." Kipala (majadiliano) 06:23, 17 Machi 2020 (UTC)

Tafsiri

Habari! naomba msaada wa tafsriri ya maneno haya : Performance of biofilm carriers in anaerobic digestion of sisal leaf waste leachate Czeus25 Masele (majadiliano) 15:41, 2 Aprili 2020 (UTC)

Kwa nini unataka kuitafsiri? ni jina la makala kuhusu utafiti fulani, haihitaji tafsiri. Ukitaka kuieleza usitafsiri utumie maneno yako. Kipala (majadiliano) 16:25, 2 Aprili 2020 (UTC)
Labda kitu kama "ufanisi wa (kipagazi ?) cha ukoga hai katika mmeng'enyo anerobi wa kichujuaji cha mikonge" - siridhiki kipagazi (carrier).Kipala (majadiliano) 18:13, 2 Aprili 2020 (UTC)

Masanja

Nmeondoa picha ya Masanja kwa sababu ya mlalamikaji mmoja akisema anaomba kuondolewa kwa picha hiyo. Natafuta picha nyingine. Czeus25 Masele (majadiliano) 03:15, 11 Aprili 2020 (UTC)

Sawa si picha ya kupendeza sana. Basi kumbuka kufuta faili ya picha yenyewe, maana bado iko. Kipala (majadiliano) 05:57, 11 Aprili 2020 (UTC)
Naomba maelekezo namna ya kufuta picha. Czeus25 Masele (majadiliano) 06:51, 11 Aprili 2020 (UTC)
Unafungua picha, utaipata kwa kuingia katika historia ya makala. Katika historia fungua nakala yenye picha, bofya picha, utapata ukurasa wa faili yake. Hapa ukihariri unaweza kufuta nisipokosei. Kipala (majadiliano) 08:28, 11 Aprili 2020 (UTC)
Ahsante. Czeus25 Masele (majadiliano) 14:06, 11 Aprili 2020 (UTC)

Programmu ya kusafishia sw.wikipedia

Kuna programmu en:Wikipedia:CLEANER, nafikiri inaweza kusaida na Wikipedia ya Kiswahili. Programmu ingine ni en:Wikipedia:Typo_Team/moss. Au tunaweza kuandika yetu. Benson Muite (majadiliano) 12:34, 29 Aprili 2020 (UTC)