Bongo Flava : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 16:
|madanyingine =
}}
'''Bongo Flava''' ni [[jina]] badala la [[muziki]] wa [[Hip hop ya Tanzania]]. Mtindo huu ulianzishwa kwenye [[miaka ya 1990]], hasa ukiwa kama mwigo au utokanaji wa [[hip hop]] kutoka [[Marekani]], ikiwa na ongezeko la athira ya muziki wa [[reggae]], [[rhythm and blues|R&B]], [[afrobeat]], [[dancehall]], na mitindo ya asili ya Kitanzania kama vile [[taarab]] na [[muziki wa dansi|dansi]], muunganiko ambao umeunda mtindo wa pekee wa muziki.<ref name="ReferenceA">Mueller, Gavin. "Bongoflava: The Primer." Stylus Magazine, 12 May 2005</ref> [[Mashairi]] kwa kawaida huwa kwa [[lugha]] ya [[Kiswahili]] au [[Kiingereza]].
 
Jina la "bongoBongo flavaFlava" ni tokeo la matini yaliyoharibiwa kutoka "bongo flavour", ambapo "bongo" ni wingi wa neno ''[[wikt:ubongo|ubongo]]'', ambapo mara nyingi huchukua nafasi ya kutaja jina la utani la [[Dar es Salaam]], jiji ambalo aina ya mtindo huu inatokea na wakati mwingine humaanisha pia nchi ya Tanzania. Katika bongo flava, sitiari ya "bongo" inaweza kutaja zaidi maana ya ujanjaujanja wa mtaani, ya ''msela'' au masela wingi wake.<ref>{{cite journal|last=Stroeken|first=Koen|title=Immunizing Strategies: Hip-Hop and Critique in Tanzania|journal=[[Africa (journal)|Africa]]|volume=75|issue=4|pages=488–509|date=Winter 2005|doi=10.3366/afr.2005.75.4.488}}</ref>
 
Istilahi ya "bongoBongo flavaFlava" ilitajwa kwa mara ya kwanza mnamo 1996 na Radio One 99.6 FM (moja kati ya redio za kwanza kabisa za binafsi nchini Tanzania) DR wa Redio [[Mike Mhagama]] ambaye alikuwa akijaribu kutofautisha kati ya muziki wa R & B na hip hop wa Marekani kupitia lipindi chake maarufu cha redio - 'DJ Show' ambapo enzi hizo vijana chipukizi walikuwa hawajaanza kutamba kwa mitindo yao wenyewe. DJ Show kilikuwa kipindi cha kwanza cha redio kukubali wanamuziki vijana wa Kitanzania wenye athira ya muziki wa Marekani - wakijieleza wenyewe kupitia uimbaji wa rap. Alisema hewani, "Baada ya kusikiliza kibao cha "R & B Flava" kilichoitwa 'No Diggity' kutoka Marekani, sasa inakuja "Bongo Flava" kutoka kwa [[Unique Sisters]], kutoka hapa nyumbani." Baada ya kusema hivyo katika kipindi, istilahi hii ya "Bongo Flava" ikanasa hadi leo hii.
 
Asili ya mwanzo kabisa na jinsi "Bongo flava" ilivyoanzishwa nchini Tanzania ni kutokana na [[Taji Liundi]] akiwa kama kiini cha hadithi hii. Kifupi hakuna asili bila yeye. Taji Liundi pia anajulikana kama Master T, mwasisi, mwanzilishi na vilevile mtayarishaji wa kipindi cha Dj Show alishaanza kupiga nyimbo za wasanii wa ndani tangu mwishoni mwa miaka ya 1994. Mike Mhagama baadaye akajiunga na kipindi akiwa chini ya ukufunzi wa Master T. Aliendelea na kutangaza kipindi hicho peke yake hata baada ya Master T kuondoka Radio One mnamo 1996.
Taji Liundi pia anajulikana kama Master T, mwasisi, mwanzilishi na vilevile mtayarishaji wa kipindi cha Dj Show alishaanza kupiga nyimbo za wasanii wa ndani tangu mwishoni mwa miaka ya 1994. Mike Mhagama baadaye akajiunga na kipindi akiwa chini ya ukufunzi wa Master T. Aliendelea na kutangaza kipindi hicho peke yake hata baada ya Master T kuondoka Radio One mnamo 1996.
 
"Bongo flava" ilikaa vizuri sana hata kabla ya rekodi za video au sauti. Vijana mjini Dar es salaam walikuwa wakirap ufukweni mwa bahari kupitia matamasha mbalimbali (yameandaliwa na [[Joseph Kusaga]] ambaye anamiliki Mawingu Discothèque, baadaye Mawingu Studios na sasa ni [[Clouds Media Group]]), matamasha ya ndani yaliyochukua sura mpya rasmi baada ya kuanzisha mfululozo wa shindano la Yo!Rap Bonanza ambalo lilikuwa likichochewa na DJ Kim "And the Boyz" Magomelo.
Line 38 ⟶ 37:
 
Miongoni mwa wasanii maarufu wa Bongo Flava kwa sasa ni pamoja na [[Ali Kiba]], [[Juma Nature]], [[Lady Jaydee]], [[Mzungu Kichaa]], [[Geezy Mabovu]], [[Q Chillah]], [[TID]], [[Diamond Platnumz]], [[Dknob]] na wasanii wapya wa Bongo Flava kama vile [[Nay wa Mitego]], [[Ben Pol]], [[Dogo Fani]] na wengine wengi. Majina mengine maarufu ni pamoja na [[Gangwe Mobb]], [[Dully Sykes]], na [[Daz Baba]].
 
==Picha==
<gallery class="center" widths="195px" style="text-align:center">
Mstari 65:
* [http://www.africanizers.i8.com/ Tovuti ya Africanizers Music]
 
{{mbegu-mwanamuzikimuziki-Afrika}}
 
{{DEFAULTSORT:Bongo, Flava}}
[[Jamii:Muziki wa Kizazikizazi Kipyakipya]]
[[Jamii:Hip hop]]
[[Jamii:Muziki wa Tanzania]]