Elimuanga : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 15:
Wataalamu wa kale katika nchi kama [[Uhindi]] au [[Ugiriki ya Kale]] walianza kutambua mwendo wa sayari na kuunda [[nadharia]] yuu ya uhusiano wa dunia, [[jua]] na sayari nyingine. Ndiyo chanzo cha [[imani]] ya kwamba nyota zinaweza kuwa na tabia fulani na athari juu ya [[maisha]] duniani na hasa kama mtu alizaliwa wakati nyota fulani ilionekana, basi tabia zilizoaminiwa kuwa za nyota ziliweza pia kuathiri maisha ya mtu huyo. Hapa kuna asili ya "kupiga falaki" na unajimu wa kisasa. Wakati uleule wataalamu hao walitazama nyota jinsi zilivyo, kuziorodhesha na kupiga hesabu za kalenda. Orodha ya kale iliyoendelea kutumiwa kwa zaidi ya miaka 1,000 ilikuwa ya [[Klaudio Ptolemaio]] kutoka Misri.
 
===Kupanuka kwa elimu tangu kupatikana kwa darubini na kamera===
Kwa [[macho]] matupu mtu mwenye [[afya]] ya macho anaweza kuona takriban nyota 6000 - 7000. Leo hii kuna zaidi za nyota 945,592,683 zilizoorodheshwa katika orodha za kimataifa.
 
Katika [[karne ya 17]] [[darubini]] za kwanza zilibuniwa [[Ulaya]]. Hivyo utazamaji wa nyota uliboreshwa na magimba ya angani mengi yalianza kuonekana. [[Galileo Galilei]] aliweza kuona [[Miezi ya sayari|miezi]] ya [[Mshtarii]] mwaka [[1609]] iliyokuwa haijajulikana hadi siku ile.
 
Katika karne ya 19 kifaa cha [[kamera]] kilileta tena upanuzi wa elimu; [[upigaji picha]] uliwezesha uchunguzi wa picha za nyota wakati wowote. Kamera iliwezesha pia kuona nyota zisizoonekana kwa macho tu. Kuingiza mwanga kwenye kamera kwa masaa kunakusanya nuru hafifu na hivyo kuonyesha lakhi za nyota zisizoonekana kwa macho.
Sehemu kubwa ya kazi ya wanaastronomia ilihama kutoka kwenye darubini kwenda deski ya mtafiti, siku hizi mbele ya kompyuta yenye data.