Nzi-matunda Mdogo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Sahihisho
dNo edit summary
Mstari 21:
'''Nzi-matunda wadogo''' ni [[nzi]] wa [[familia (biolojia)|familia]] [[Drosophilidae]] katika [[oda]] [[Diptera]] wanaotaga [[yai|mayai]] katika [[tunda|matunda]], yale yaliyoanza kuoza ama yaliyopata madhara hasa, na katika maada nyingine ya mimea inayooza. Nzi-matunda wa familia [[Tephritidae]] ni wakubwa zaidi na hutaga mayai yao katika matunda yasiyooza.
 
Nzi hawa ni wadogo sana ([[mm]] 2-4) kwa kawaida lakini kuna spishi zilizo kubwa kuliko [[nzi-nyumbani]] (mm 15). Rangi yao ni njano, kahawianyekundu, kijivu au nyeusi na macho yao ni mekundu. Mara nyingi [[bawa|mabawa]] yana mabaka meusi.
 
Majike hutaga [[yai|mayai]] katika maada inayooza ya [[mmea|mimea]] na [[kuvu]], inayojumuisha matunda, [[ua|maua]], [[gome|magome]] na [[kiyoga|viyoga]]. [[Buu|Mabuu]] ya [[spishi]] kadhaa, kama ''Drosophila suzukii'', wanaweza kuharibu matunda kabla ya mavuno na kuletea [[mkulima|wakulima]] hasara kubwa, lakini kwa kawaida nzi hao ni wasumbufu tu.