Hongera ya makala ya Uholanzi. Kuna msaada mmoja: sanduku la habari za nchi - njia rahisi ni kuinakili kutoka en.wikipedia (nakili katika hali ya "edit" ) na kuibandika tu kwa sw.wiki. Halafu ukibonyeza "Mandhari ya mabadilisho" utaona ya kwamba sehemu kubwa ni Kiswahili tayari. Unatafsiri maneno machache tu. Matt ameandaa templeti hii, mimi naona ni msaada mkubwa - --Kipala 19:20, 25 May 2006 (UTC)

Kweli, ni rahisi sana. ChriKo 12:53, 26 May 2006 (UTC)

Hongera kwa makala ya yule ndege ( Muddyb Blast )

hariri

Kimtazamo unaonekana umezama sana kiwikipedia, mimi binafsi nimependezewa sana ile Template ulioitumia kwenye makala ya kuelezea majopu ya ndege, ni mda mrefu sana nilikuwa nikiona zile Template kwenye wikipdeia ya kingereza lakini nikijaribu kunakili zile Template zinakuwa lemavu yaani hazina uwezo kuonekana katika sw.wiki hivyo juhudi zangu zikagonga mwamba kwa upande wa zile Template nikawa nasubiria siku nimfahamishe bwana kipala kuhusiana na ile Template kwa bahti nzuri nikiwa naangalia zile kurasa mpya katika Special Pages nikaona kurasa yako inayohusu ndege hivyo mpango wangu utafanikiwa Hongrea bwana chriko na kila lakheri katika maisha yako huko uliko Ahksante.

--Muddyb Producer 07:09, 6 Septemba 2007 (UTC)Muddyb Blast Producer

Aksante Bwana ChriKo

hariri

Habari yako ndugu ChriKo, natumai humzima wa afya pole nakazi. kwanza ahsante kwa jibu la haraka ulionigea kuhusiana na ile Template nilkuwa na mpango wa kujaribu tena nikishindwa nitamtafuta ndugu marco kwa msaada zaidi, hata hivyo nilijitahidi mpaka kuiona zile html zake na kujaribu kuhariri baadhi yake ikakubali baadhi zikakataa na pia nashukuru kwa jibu lako la haraka kazi njema na tuendelee hivi hivi kuchangia Wikipedia. --Muddyb Producer 11:06, 7 Septemba 2007 (UTC)Muddyb Blast Producer

Okapi

hariri

Nimetunga makala nilipoona habari za BBC [[1]]. Naomba uangelie jinsi nilivyojaza sanduku ya uainishaji kama ni sawa. --Kipala 15:17, 10 Juni 2006 (UTC)Reply

Mwarobaini

hariri

Salaam, nimejaribu kutunga sanduku la uainishaji kwa makala ya Mwarobaini - naomba uangalie na kusahihisha. --Kipala 13:18, 25 Juni 2006 (UTC) Ukipata nafasi - naomba angalia pia Biolojia; nilikuwa nimechoka mito na miji halafu ilikuwa kama pengo kwenye ukurasa wa Mwanzo. --Kipala 16:14, 25 Juni 2006 (UTC) (Pole, nimesafiri, niko Senegal sasa. Nikirudi nitaangalia kurasa hizi. ChriKo 13:00, 30 Juni 2006 (UTC))Reply

Nimesahau kusema: Asante! --Kipala 20:00, 13 Julai 2006 (UTC)Reply

Congratutalions, and some questions

hariri

Hi ChriKo. I hope you understand English. Congratulations with the 1000 articles in Swahili! It's just great! It's probably the first encyclopedia in an original African language with more than 1000 articles, or?

I have been involved in Wikipedias in several other African languages, such as Bambara. I will be speaking about the Wikipedias I have been involved in. And I would be grateful if you could answer some questions. Also, any other remarks are welcome.

1. Where are you from? Where did you learn Swahili?

2. When did you hear about Wikipedia? And when about the Swahili Wikipedia? When did you start to contribute?

3. What do you think about the future of this project?

thanks, Guaka 20:37, 3 Agosti 2006 (UTC)Reply

Hi Guaka, thanks for the congrats, which I will have to share with the other regular contributors. It's indeed wonderful that the Swahili Wikipedia has breached the 1000 mark. It could well be the first in an African language, I have not checked. Reading your questions, I am again reminded that it is high time I introduced myself on the various Wikipedias to which I contribute. My answers to your questions are a start:
1. I was born in the Netherlands like yourself but left the country after my studies at Wageningen University in 1979. I have been back only occasionally since then. I learned Swahili in Kenya during a study period in 1976/7. Later, I have lived and worked in that country twice for a total of more than 10 years. I have regularly visited Tanzania as well. In addition, I have lived in Niger, Nigeria and Sudan, and travelled extensively throughout the continent. Though I now work in Benin, my Kenyan wife still lives in the highland town of Nanyuki where I visit her twice a year.
2. I learned about Wikipedia in 2004 and it did not take me long to discover the Swahili one. I started to contribute last year.
3. I assume that with "this project" you mean the Swahili Wikipedia. I have to admit that initially I was a bit pessimistic about the future of the project, especially since I had the impression that few native Africans contributed. It was partly the reason for me to start contributing. I am now more optimistic, though cautiously so. I think we need many more Africans to contribute. ChriKo 22:27, 7 Agosti 2006 (UTC)Reply
1) I'm from the UK. I lived in Kenya for six few years when I was growing up, and still manage to visit East Africa about once a year. I picked up a little Swahili when I lived in Kenya, but I've been trying to learn properly for the last couple of years. My Swahili isn't anywhere near good enough to write fresh articles, but I've got a fair bit of experience with MediaWiki and Wikipedia, and when I have time I try and help out here with more technical wiki aspects like templates, categories, translating the user interface etc.
2) I got involved in the English Wikipedia in March 2004, and the Swahili Wikipedia from 2005. I probably first heard about it from the Swahili article in en:.
3) It's very encouraging to have reached 1,000 articles. For a long time it was stuck with around a dozen actual articles of mediocre quality. We really need to have more African Swahili speakers involved with the project, but that may be a matter of waiting for more people to get online and to get faster connections. A Wikipedia edition needs a community of editors actively working and maintaining the project, but for that, a contributor needs a fairly decent connection to the Internet. Matt Crypto 17:35, 8 Agosti 2006 (UTC)Reply
Thats some interesting contributions here, I just came across them today (because I spent August once more in EAK and EAT and did not check very often). I have also had my thoughts about the African share among the authors. At the monent Ndesanjo looks a bit alone holding up the African flag in this wikipedia from the other side of the Atlantic, although he seems to be a tough guy and won´t be scared by all the wazungu invading here. On the other hand we probably have similar motivations for contributing here.
Surely it makes a difference if its all Africans contributing or if most contributions come from "guest-workers". Especially with articles on history, culture and society. A critical mind may call for some "decolonizing of the sw-wiki-mind" after some time from now.
On the other hand I think that it is not so grave with this open concept of wikipedia. Once an encyclopedia worthwhile to be called so is in place it will be used. And it is open to everybody to change and correct. So whatever "harm" I may do with my contributions - it's open for change.
I really find this much more worthwhile than a wikipedia say in English - German - French because this may be the only chance in a nearer future for Kiswahili to have an encyclopedia -I dont see it coming in print from any East African publisher. So lets go. Pecca fortiter! (thats Martin Luther about necessary sins ...) --Kipala 20:48, 13 Septemba 2006 (UTC)Reply

Areas of habitat

hariri

ChriKo, could it be possible to mention countries and places where the species you describe occur? Would be helpful for interlinking. Just an idea, what do you think? --Kipala 20:48, 13 Septemba 2006 (UTC)Reply

Hi Kipala, welcome back! Yes, countries and places will have to be mentioned when I get down to describing species. For the moment, I am listing groups that have single Swahili names, and providing short descriptions. Describing the individual species will be a lot of work, which I do not have much of at the moment. As a matter of fact, I am thinking of requesting the help of my friends of the Nature Kenya bird group. I may also contact some Tanzanian birders. ChriKo 21:32, 13 Septemba 2006 (UTC)Reply

Nahitajii jina

hariri

Chriko, naomba nisaidie jina la "Goshawk" (kijer. Habicht). Naiihitaji kwa makala ya Azori. Jina ni lile la ndege. Naweka kwa sasa "tai" lakini si yenyewe. Ukijua naomba sahihisha neno lile moja tu. --Kipala 23:59, 15 Septemba 2006 (UTC)Reply

Jina la "goshawk" ni "kipanga". Nimekwisha kuhariri makala yako. ChriKo 18:41, 16 Septemba 2006 (UTC)Reply


mpungate (kakati)??

hariri

Chriko, naomba tena msaada ikiwezekana. Nahitaji neno la "cactus" - angalia makala ya "Nembo ya Mexiko". Nimetumia neno "mpungate (kakati)" lakini sina uhakika kama ni sahihi. Ukijua nashukuru ukisahisha. --Kipala 16:34, 27 Septemba 2006 (UTC)Reply

Salamu Kipala. Mpungate ni sawa. "Cacti" haitokei Afrika kwa asili. Spishi chache zimeingizwa na ile iliyotapakaa ni "prickly pear" au mpungate. Ni spishi hii inayoonyeshwa kwa nembo ya Mexiko. ChriKo 10:35, 1 Oktoba 2006 (UTC)Reply

Problem of lines inside taxoboxes

hariri

Chriko, youa sked me about a problem with line getting into taxoboxes. Does it persist? It could be something with the settings on your screen. I have seen it, too, but it is not consistent and sometimes off again. --Kipala 18:57, 8 Oktoba 2006 (UTC)Reply

Majina za nchi

hariri
ChriKo, asante kwa ushauri wako kwenye ukurasa wa majidiliano / Afrika. Ushauri wangu ni tofauti kidogo: tusivutane mno kuhusu tahijia ya maneno au kutumia majina namna gani. Tutapoteza muda wetu tu.Tuongeze maumbo mengine kwa kuongeza makala za "Redirect".
Sababu zangu
  • hali halisi hakuna orodha ya majina inayokubaliwa. Hatuna budi kuendelea na maumbo mbalimbali lakini tuweke viungo! Tujitahadhari tukibadilisha kitu ili tusiharibu viungo vilivyopo!
  • orodha za TUKI na BAKITA ya majina ya nchi haifuatwi mara nyingi wala Tanzania wala Kenya. Jinsi inavyoonekana kwangu sehemu yake ni kazi bure. Kama orodha ya Kamusi Hai ni sawa zote mbili hazikubaliani kati yao.
  • Nimejipatia "Atlasi kwa Shule za Msingi Tanzania" (ISBN 9976950403, chapa ya tatu 2005) ambayo ni Atlasi ya pekee kwa Kiswahili ninayofahamu. Haifuati orodha ya TUKI. Lakini hii ni namna ya majina ambayo wanafunzi wanafundishwa nchini Tanzania.
  • inaonekana kuna nchi yenye majina ya pekee kwa Kiswahili yenye uzoefu ya miaka mingi (kwa mfano Misri, Uingereza, Marekani, Shelisheli). Haya tutetee.
    • Nchi nyingine ina majina ya kimapokeo (kama vile Uhabeshi, Uajemi) lakini kuna matumizi sawasawa ya majina ya kimataifa kama vile Ethiopia na Iran. Hatuna budi kuonyesha yote.
    • Kuna nchi nyingine ambazo hazijadiliwi mara nyingi kwa Kiswahili. Hapo matatizo yanaonekana ya orodha zilizotungwa kwenye deski ya TUKI au BAKITA lakini hazitumiki au hutumiwa mara chache sana lakini majina ya kimataifa hutumiwa zaidi. Mifano ni Guinea, Cote d'Ivoire, Nigeria (TUKI: Gini, Kodivaa, Nijeria) na mengi mengine. Nashauri tuongeze Redirect na kuongeza kwa mabano majina haya katika makala ya nchi.
  • Mtindo wa TUKI na BAKITA mara nyingi ni kufuata matamshi ya Kiingereza. Ila tu si rahisi kuelewana kwa sababu katika Kiingereza kuna tofauti katika matamshi (Kiingereza ya kisiwani au ya Marekani auya wapi..). Wameanza tu kwa orodha ya majina machache ya nchi. Baada ya kuandika makala mengi ya nchi naona matata katika mtindo huo. Pamoja na sababu nilizotaja hapo juu inaongeza ugumu wa kuoandika makala upande wa historia, kwa mfano ukieleza asili ya jina la nchi (etimolojia). Kwa mfano Guyana ilipatikana kama jina la koloni tatu za Uingereza, Ufaransa na Uholanzi katika Amerika ya Kusini. Kwa nini tuandike nchi moja "Guyana" lakini nchi nyingine "Gwiyana" (TUKI)?? Kwa nini San Marino iwe "Samarino"?? Hizi ni fikra tupu za deski lakini si matumizi ya lugha.
Nitaandika makala kuhusu tatizo na kutoa orodha ya majina ya nchi kandokando. Nimeshandaa orodha ya TUKI/BAKITA kwa bara na nitaongeza umbo la Atlasi kwa Shule za Msingi.
Naona heri tufuate umbo la Atlasi kwa sababu hii ni kitabu kinachotumiwa, tofauti na orodha zile zilizotajwa. Unaonaje ? --Kipala 18:32, 8 Oktoba 2006 (UTC)Reply
Kipala, nimefahamu sababu zako za kupea nchi majina fulani. Lakini nafikiri si mzuri kutumia kitabu kimoja ili kuchagua majina haya. Ni kweli kama wanaisimu hawakubali kuhusu utumiaji wa majina ya nchi. Hata mimi sipendi majina kadhaa, kama Gine na Kotivaa (hata Samarino). Wala sipendi mtindo wa kufuata matamshi ya Kiingereza. Lakini nani atachagua? Ni sisi wazungu au wazungumzaji wa kienyeji? Inaonekana kwangu kama ni lazima tuhakikishe utumiaji wa majina ya nchi miongoni mwa wananchi na kwa magazeti.
Tusipotumia majina ambayo yanafuata matamshi ya Kiingereza, tutafuata matamshi gani? Kama hakuna jina ambalo linatumika sana, labda tungetumia jina rasmi linalotumika nchini, k.m. Guyana au San Marino. Pengine tunaweza kufuata majina yanayotumika kwa lugha zingine za Bantu. K.m., “Kameruni” hutumika kwa Kinyarwanda. Nafikiri afadhali tutie –i nyuma ya majina rasmi ambayo mwisho yao ni konsonanti, kwa sababu hii haipatikani kwa maneno ya lugha za Bantu.
Kwa kila hali haya ni majadiliano baina ya wazungu wawili. Afadhali tukaribishe wananchi. ChriKo 21:34, 9 Oktoba 2006 (UTC)Reply

Karibu tena!

hariri

ChriKo, nimefurahi kuona bata yako! Niliogopa umepotea lakini umerudi. Karibu tena! --172.173.207.46 06:00, 9 May 2007 (UTC)

Asante! Nimefanya kazi katika Sudan na Senegal. Kupata mtandao kwa nchi hizi ni ngumu isipokuwa mjini kuu.ChriKo 08:32, 9 May 2007 (UTC)

Nimefudhu

hariri

Salam Nyiingi Nd. ChriKo, Ni baada ya kimya kingi natafakari nyingi zilizonijaa juu ya sanduku za habari. Ni siku hizi nimeamua kuwa naziumba mwenye kisha naomba msaada wa marekebisho kutoka kwa mkab. Hilo ni baada ya wewe ndugu chriKo kunifahamisha hivyo nimefaulu ahsante. ---Muddyb Blast Producer 05:44, 22 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Salamu nyingi ndugu Muddyb. Ninafurahi sana kuona kama umeweza kuandikia wikipedia yetu makala mengi. Kusaidia ni furaha yangu. ChriKo 16:21, 25 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Uchaguzi

hariri

Kuna mapendekezo mapya kwa Wakabidhi na bureaucrat. Naomba angalia ukurasa http://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Wakabidhi --User_talk:Kipala 08:35, 1 Februari 2008 (UTC)Reply

Uteuzi mpya

hariri

Kuna pendekezo jipya kwa bureaucrat. Naomba uangalie ukurasa wa wakabidhi. --Oliver Stegen 09:16, 1 Machi 2008 (UTC)Reply

Sooty Chat

hariri

ChriKo, salam. Ndugu ChriKo, unaweza kunieleza mawili matatu kuhusiana na Sooty Chat? Ikiwezekana umwandikie hata makala inayomhusu huyu ndege! Natumai nitakubaliwa ombi langu!! Ubarikiwe.--Mwanaharakati (majadiliano) 07:43, 5 Septemba 2008 (UTC)Reply

Muddyb, salama nyingi. Pole, niko porini. Nitajibu baadaye. ChriKo (majadiliano) 23:41, 11 Septemba 2008 (UTC)Reply
ChriKo, salam. Ahksante kwa ukurasa wa ndege Chati. Lakini labda nikusumbue kidogo (samahani sana). Huyu ndege kweli ni yule, lakini yule niliyemtaka mimi ni yule anayesemekana kuwa yeye anaimba (songbird), ambaye makala yake waweza kuifikia kwa kutumia ukurasa huu! Natumai umenipata, basi ukipata muda tena, naomba ujaribu!! Kazi njema.--Mwanaharakati (Longa) 06:09, 24 Septemba 2008 (UTC)Reply
Salaaam! Sijui kwa Kiswahili anaitwaje. Ila nimeona katika Wikipedia kwa Kiingereza wakimwita Sooty Chat! Ila kwa Kiswahili sijui. Lakini ni Sooty Chat. Kila lakheri...--Mwanaharakati (Longa) 09:05, 26 Septemba 2008 (UTC)Reply
ChriKo, salam. Nashukuru kwa makala nzuri ya ndege mwimbaji!! Pia nakutakia kila lakheri huko uliko, ahsante.--Mwanaharakati (Longa) 05:41, 6 Oktoba 2008 (UTC)Reply

Hi ChriKo ;)

hariri

Hi! How are you? Could you please help me add a couple of sentences to the Kiswahili version of this interesting article?

Thanks so much! -Ivana Icana (majadiliano) 22:35, 6 Septemba 2008 (UTC)Reply

Hi Ivana, I'll try to find some time. ChriKo (majadiliano) 23:46, 11 Septemba 2008 (UTC)Reply
Salaam, huyu mama ni msumbufu. Angalia majadiliano kwenye ukurasa wa makala. --91.96.107.243 08:33, 12 Septemba 2008 (UTC)Reply
Kweli, nimeona. Asante sana! ChriKo (majadiliano) 20:53, 14 Septemba 2008 (UTC)Reply

Familia

hariri

ChriKo, salaam. Nafurahia kuona insi unavyoendelea na makala za ndege. Sasa nimegundua jambo. Unaweka Kiungo kwa familia kama kitengo cha uainishaji. Je unaonaje ikibadilishwa kuwa familia (biolojia)? Maana yake neno familia pekee yake itakuwa ni zaidi jumuiya ya kibinadamu. Je, bado inawezakana kubadilisha kiungo hiki? --Kipala (majadiliano) 19:00, 29 Novemba 2008 (UTC)Reply

Salaam, umesema kweli. Nitavibadilisha baadhi kwa kila wakati mmoja. ChriKo (majadiliano) 21:53, 29 Novemba 2008 (UTC)Reply

Pole na kazi!

hariri

ChriKo,salaaaam! Mzee wangu, nimeona umefanya kazi siyo ya kitoto kiasi hata kustahili kupewa pongezi - HONGERA! Ni baada ya kimya kirefu almanusura tukukatie tamaa kama jinsi ilivyo kwa Nino, Matt, Sj, na wengine weeeengi! Ningependa kusema karibu tena na ninafurahia kuona Waswahili tunazidi kupata makala nyingi za ndege. Na kwa hili, sidhani kama kuna Wikipedia yeyote ya Kiafrika inafikia Wikipedia yetu kwa makala za ndege. Basi tusemaje? Labda hongera zaidi na kila la kheri liwe juu yako! Nikiwa natokea Dar es Salaam, Tanzania, niite Muddyb au--Mwanaharakati (Longa) 08:35, 23 Machi 2009 (UTC)Reply

Muddyb, salaam na asante kwa pongezi zako. Mara kwa mara ninasafiri kwa ajili ya kasi yangu na wakati huu siwezi kuandika makala. Napenda sana kufanya kazi hii na ninafurahi kama kuna watu ambao wanapenda vile ninafanya. Utaona makala mpya nyingi za ndege. ChriKo (majadiliano) 11:30, 24 Machi 2009 (UTC)Reply
Basi tunazikaribisha!!!!!!--Mwanaharakati (Longa) 13:02, 24 Machi 2009 (UTC)Reply

11,000

hariri

ChriKo, salaaaaam! Wikipedia yetu imefikisha makala 11,000! Ni furaha iliyoje? Basi tu, niseme tujitahidi kuendeleza na kushauriana kwa kila jambo litakalosaidia Wikipedia yetu kuwa juu! Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 15:54, 9 Aprili 2009 (UTC)Reply

Oyeeee!!! Hongera Muddyb, hongera kila mtu aliyechangia. Ninafurahi sana. Nasema tufikishe 20,000 sasa.ChriKo (majadiliano) 21:47, 11 Aprili 2009 (UTC)Reply

Swala na wengine

hariri

Salaam ChriKo Je unajua kama kuna njia ya kutofautisha kwa Kiswahili kati ya akina swala na wale wanaoitwa "antelope" kwa Kiingereza? --91.62.33.152 11:11, 16 Aprili 2009 (UTC)Reply

Ndiyo, najua. Nitaweka orodha ya spishi katika makala ya swala. Nikipata nafasi nitaandika kurasa za spishi.ChriKo (majadiliano) 12:56, 16 Aprili 2009 (UTC)Reply

Mwanaharakati awe bureaucrat

hariri

Nimemteua Mwanaharakati achaguliwe kuwa msimamizi mkuu pamoja nasi (b'crat). Naomba upige kura kwenye ukurasa wa wakabidhi. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 07:20, 28 Mei 2009 (UTC)Reply

Flowerparty awe mkabidhi

hariri

Nimemteua Flowerparty achaguliwe kuwa mkabidhi pamoja nasi. Naomba upige kura kwenye ukurasa wa Wakabidhi. Ahsante! --Mwanaharakati (Longa) 10:36, 9 Julai 2009 (UTC)Reply

mradi wa Google kwa ajili ya wikipedia yetu

hariri

Bwana ChriKo, salaam!
Nimepata mawasiliano kutoka Christine Moon begin_of_the_skype_highlighting     end_of_the_skype_highlighting huko Palo Alto, California. Yeye anafanya kazi kwa shirika la Google, nao wameanza kupanga mradi au huduma kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania na Kenya ili waelimishwe kuandika makala kwa wikipedia ya Kiswahili. Kumbe!
Christine sasa ametualika kumwandikia maoni yetu, angalia tovuti hiyo:
http://docs.google.com/Doc?docid=0AbIPJ9Nv6udZZGd6MndwcGdfMzFkODNzOG0zYw&hl=en
Bahati mbaya yeye haelewi Kiswahili, kwa hiyo itakuwa lazima kumwandikia kwa Kiingereza. Asante kwa michango yako!
Ni wako katika ujenzi wa lugha yetu, --Baba Tabita (majadiliano) 08:04, 10 Oktoba 2009 (UTC)Reply

Baba Tabita, salamu sana. Ni sawasawa, nitamwandikia nikiwa nimerudi safari yangu. Nipo kusini kwa Senegali sasa. ChriKo (majadiliano) 22:54, 12 Oktoba 2009 (UTC)Reply

majadiliano kuhusu utafsiri wa istilahi

hariri

Bwana ChriKo, salaam! Nimeanzisha majadiliano mapya kuhusu utafsiri wa istilahi ya wikipedia yetu hapa. Naomba uyaangalie na kuchangia maoni yako. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 09:39, 23 Oktoba 2009 (UTC)Reply

Miti

hariri

Salaam nafurahia kuona ya kwamba siku hizi umeangalia hata mahali ambako ndege hulala au kutafuta kivuli! --Kipala (majadiliano) 07:31, 10 Desemba 2009 (UTC)Reply

Salaam. Nafurahi kama unapenda vile ninafanya. Nafikiri mimi ni mwanabiolojia wa pekee ambaye anaandikia wikipedia ya Kiswahili makala. Kwa hivyo lazima niandike kuhusu mada yoyote ya biolojia. ChriKo (majadiliano) 21:53, 10 Desemba 2009 (UTC)Reply

Hongera ya makala 18,000

hariri

Salam, ChriKo! Hongera ya makala 18,000! Kumbe tumefika - japokuwa kuna mengi ya kusahihisha na kufuta pia. Lakini si mbaya tukipongezana! Tuendeleeni jamani.--MwanaharakatiLonga 09:13, 31 Mei 2010 (UTC) Reply

Sanduku la uainishaji kwa ng'ombe

hariri

Naomba angalia mabadiliko ya sanduku kwa ng'ombe. Nimeongeza elezo kwa Ruminantia na kuweka maelezo yote maandishi madogo. Unaonaje? Ukipenda, tumia - usipopenda - rudisha ukurasa nyuma. (91.98.113.164 21:03, 7 Juni 2010 (UTC)) ni mimi Kipala (majadiliano) 05:32, 8 Juni 2010 (UTC)Reply

Nimeona, asante. Nitaitumia, lakini nimeibadilika vidogo. ChriKo (majadiliano) 16:10, 8 Juni 2010 (UTC)Reply

Questionnaire

hariri

Nadhani labda wewe umepata pia maswali yale ya Rachel - hapa majibu yangu: Mtumiaji:Kipala/questionnaire - Kipala (majadiliano) 19:07, 30 Juni 2010 (UTC)Reply

Jimbo Wales' Wikimania questionnaire

hariri

Hi, how are you; I received a message from Jimbo Wales' office, asking if I would like to participate in a questionnaire. As I am not so proficient in Kiswahili, I wonder if you would be interested? /// Hi, mimi nilipokea ujumbe kutoka kwa ofisi ya jimbo Wales ', kuuliza kama napenda kushiriki katika maswali ya. Kama mimi si hivyo magari katika Kiswahili, mimi ajabu kama ingekuwa nia? Kama wewe ni, nami nitawapa ujumbe kwamba una nia. /// Please see: User talk:Mr Accountable#Hello! --Mr Accountable (majadiliano) 18:27, 1 Julai 2010 (UTC)Reply

Msaada wa tasfiri

hariri

Salam mzee ChriKo. Kumradhi ndugu, unaweza kutoa maoni kwenye ukurusa wa jumuia? Tafadhali tembelea:

Wikipedia:Jumuia#Tafsiri_ya_.22Wikipedia_Usability_Initiative.22_kwa_Kiswahili

Kila la kheri.--MwanaharakatiLonga 13:49, 3 Julai 2010 (UTC) Reply

Kura ya kuamua juu ya wakabidhi waliopotea

hariri

Karibu kutembelea ukurasa wa wakabidhi na kuamua juu ya wenzetu waliopewa haki za wakabidhi lakini hawakuonekana tangu miezi mingi: Wikipedia:Wakabidhi#Kura_ya_kuondoa_wakabidhi_waliopotea. Tuliwahi kujadili swali hili mwaka uliopita (tazama kwenye ukurasa unaotajwa, juu ya pendekezo) ; sasa njia imeonekana. Kipala (majadiliano) 05:28, 1 Oktoba 2010 (UTC)Reply

Chipmunks

hariri

Salam, ChriKo! Eti umeona huo ukurasa huo hapo juu? Unaenda katika Wikipedia ya Kiingereza, huruma - sijui hao Chipmunks ni panya au namna gani. Je, unaweza kuumba ukurasa wa Chipmunk japo kwa Kiswahili? Au hata ukielezea namna uonavyo kwa kitaalamu zaidi? Haya, ni hilo ombi langu. Wako Muddyb au,--MwanaharakatiLonga 09:07, 11 Oktoba 2010 (UTC) Reply

Muddyb, salaam. Ndiyo, nimeona ukurasa huo. Chipmunk ni aina ya kindi ambaye anaishi ardhini. Nikipata nafasi ningeweza kuumba ukurasa wa chipmunk, lakini isingekuwa mzuri zaidi niumbe ukurasa wa kindi kwanza? Wako, Christiaan. ChriKo (majadiliano) 13:31, 14 Oktoba 2010 (UTC)Reply
Jamani? Miye sijui lolote kuhusu wanyama! Kwa vile wewe ni mtaalamu wa masuala ya viumbe hai, tafadhali fanya vile ipasavyo! Ikiwa safi, basi nitakuwa mwenye kushukuru. Kila la kheri.--MwanaharakatiLonga 16:55, 14 Oktoba 2010 (UTC)Reply

Makala za mamalia

hariri

Kipala na Muddyb, salaam. Nawaandikia tena kuhusu rafiki yetu Mjanja. Ameanzisha makala nyingi kuhusu mamalia ambao hawatokei Afrika. Pengine naweza kukubali majina anayotumia, lakini kuna mengine ambayo ameyabuni kabisa au anayatumia kwa njia mbaya. Sidhani ni mzuri kama msemaji asiye mwenyeji anabuni majina mapya. Tafadhali hii ifanywe na wataalamu wa kienyeji. Majina nisiyoyakubali ni yafuatayo:

Mnajua wataalamu (wanazoolojia) ambao watakubali kubuni majina ya wanyama haya kwa Kiswahili? Zamani nimeandikia wanazoolojia katika Tanzania na Kenya, lakini hakuna mtu aliyejibu. ChriKo (majadiliano) 23:02, 20 Julai 2011 (UTC)Reply

Nakubali - asianzishe. Je tufute zote? Menginevyo: nimempata mtaalamu 1 anayejibu mara kadhaa lakiní yeye mwalimu wa astrologia. Wengine: maaraida swa na yako. Kipala (majadiliano) 22:35, 21 Julai 2011 (UTC)Reply
Kwa maoni yangu unaweza kuzifuta. Nitaendelea kutafuta wanazoolojia walio tayari kutafsiri majina ya wanyama wasiotokea Afrika. Itakuwa ngumu kwa sababu siishi katika Afrika ya Mashariki sikuhizi.ChriKo (majadiliano) 23:27, 22 Julai 2011 (UTC)Reply

Salaam

hariri

ChriKo, nataka kukuambia tu nafurahia kila safari ninapokuona jinsi unavyoendelea kujenga msingi wa wikipedia yetu kazika habari za biolojia. Asante. 91.98.113.164 18:44, 9 Oktoba 2011 (UTC)Reply

Karibu! Furaha ni yangu. (Ulisahau kutia sahihi yako, kwa hivyo sikuweza kukuhutubia kwa jina lako). ChriKo (majadiliano) 20:31, 9 Oktoba 2011 (UTC)Reply

Désolé

hariri

Hello ChriKo,
I'm afraid I don't speak a single word of swahili, so I could not even read your message of Decembre 4th. If you could have it translated into english, I would be able to read and most probably understand it, and then answer it if needed. Anyway, I thank you very much for the attention you paid to my humble person. Hop [[Utilisateur:Kikuyu3|Kikuyu3]] [[Discussion utilisateur:Kikuyu3|Sous l'Arbre à palabres]] (majadiliano) 20:15, 10 Desemba 2011 (UTC)Reply

Bonjour, Chriko,
Merci de ton intercession sur la page de discussion de l'article "swahili" sur SW:. Ta traduction de ma question a engendré rapidement une réponse d'un contributeur plein de bon sens. J'ai transposé sa réponse sur la page de discussion de l'article. Je viens de faire de même avec ta propre réponse, ainsi nos spécialistes du sujet sauront comment s'orienter.
Asante sana, je crois qu'on dit comme ça. Merci beaucoup et Hop ! [[Utilisateur:Kikuyu3|Kikuyu3]] [[Discussion utilisateur:Kikuyu3|Sous l'Arbre à palabres]] (majadiliano) 11:37, 11 Desemba 2011 (UTC)Reply

Bioanuwai

hariri

Nisipokosei unatafuta neno "bioanuwai". Ujaribu kuiweka katika google nadhani utaridhika. Wasalaam! 91.98.113.164 11:41, 27 Desemba 2011 (UTC)Reply

Nadhani jibu umepata, mzee wangu. Kama alivyosema ndivyo-iitwavyo!--MwanaharakatiLonga 12:31, 27 Desemba 2011 (UTC)Reply
Asante sana!! ChriKo (majadiliano) 13:42, 27 Desemba 2011 (UTC)Reply

Jamii:Mitishamba

hariri

Nimekuta leo jamii hii nikashangaa kidogo. Sijaangalia yote lakini ninahisi ni zaidi miti ya matunda ambayo si "mitishamba" - yaani dawa (la kienyeji) kutokana na mimea inayopatikana katika mazingira. Lakini haimaanisha "Miti inayokua shambani". Kama nimekosea naomba maelezo zaidi. Kipala (majadiliano) 13:35, 11 Februari 2012 (UTC)Reply

Ndiyo, uko sahihi. Sikufikiria vizuri. Nikikuta jamii hii, niliangalia ndani yake nikaona miti ya matunda. Kwa hivyo nimeongeza miti ya matunda mingine. Lakini kweli, “mitishamba” ni dawa litokalo shambani au msituni. Nitaondoa miti ya matunda. ChriKo (majadiliano) 19:06, 11 Februari 2012 (UTC)Reply

Pendekezo kuhusu utaratibu wa kuanzisha makala kwa watumiaji waliojiandisha pekee

hariri

naomba usome hapa na fanya uamuzi wako: Wikipedia:Jumuia#Pendekezo:_Utaratibu_wa_kuanzisha_makala Kipala (majadiliano) 14:57, 26 Novemba 2012 (UTC)Reply

Article requests in Swahili

hariri

Hi! I know you are sw-2. Are you interested in writing short stubs for the Swahili Wikipedia? Thanks WhisperToMe (majadiliano) 01:18, 24 Julai 2013 (UTC)Reply

Hello. I am already writing plenty of articles, stubs and otherwise, for the Swahili Wikipedia. What kind of stubs would you want me to write? ChriKo (majadiliano) 12:20, 24 Julai 2013 (UTC)Reply
The stubs I had in mind are mainly government agencies, including radio producers, public school systems, and an aviation authority. The list includes:
Please let me know if you are interested in writing articles about these subjects
WhisperToMe (majadiliano) 17:31, 24 Julai 2013 (UTC)Reply
Being a biologist, these subjects don't particularly interest me, but when I have some time, I'll see what I can do. ChriKo (majadiliano) 19:35, 24 Julai 2013 (UTC)Reply
Thank you :) - All I need are small stubs. I'll let you know if I find anything biology or science related that I think should have a Swahili translation WhisperToMe (majadiliano) 05:05, 25 Julai 2013 (UTC)Reply
Have you had a chance to start some of these stubs? WhisperToMe (majadiliano) 19:18, 31 Agosti 2013 (UTC)Reply
I'm afraid that I've had little time to spend on Wikipedia lately. Maybe in the next few weeks.ChriKo (majadiliano) 20:41, 31 Agosti 2013 (UTC)Reply
Ok. If you do get a chance to do it, please let me know. Thank you WhisperToMe (majadiliano) 16:01, 10 Septemba 2013 (UTC)Reply
First one: https://sw.wikipedia.org/wiki/Radio_France_Internationale. ChriKo (majadiliano) 21:01, 10 Septemba 2013 (UTC)Reply
Thank you so much! 108.243.10.234 07:14, 28 Septemba 2013 (UTC)Reply

Viungo vya interwiki katika makala mpya

hariri

Salaam tele Nd. ChriKo kutoka mjini Dar es Salaam, Tanzania! Baada ya salaam, ninapenda kukumbusha kuhusu uwekaji wa viungo vya interwiki katika makala mpya. Hivi karibuni nimeona ukiandika makala bila viungo vya Wikipedia zingine. Wamebadili utaratibu wa kuunganisha Wikipedia moja kwenda nyingine - je, ushajua namna ya kuunganisha? Binafsi nimeunga ya "Lemuri-spoti" kwenda ENWIKI. Tafadhali nijuze kama unaona kuna kikwazo katika hilo. Wako,--MwanaharakatiLonga 06:00, 19 Agosti 2013 (UTC) Reply

Salaam kwako Muddyb. Uko sahihi. Tangu njia hii mpya kuweka viungo imetekeleza, ninasahau kuviweka mara kwa mara. Nitaisahihisha. Asante kwa kunikumbusha. ChriKo (majadiliano) 21:34, 19 Agosti 2013 (UTC)Reply

Wiki Indaba conference

hariri

Salaam, ChriKo. Kuna mpango wa mkutano mjini Johannesburg mwezi wa pili mwakani, angalia http://wikiindaba.net/index.php?title=Main_Page - pia, umeombwa kujibu maswali yao kwenye tovuti la Google docs: https://docs.google.com/forms/d/1zEk6hw4IiQYVrdJGYphPhQHOQFi4wdOIXvzVj9vy_gU/viewform Asante kwa msaada wako. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 12:28, 4 Novemba 2013 (UTC)Reply

Salaam Baba Tabita. Ningependa sana kushiriki katika mkutano huu, lakini ni mbali sana kutoka mahali pa kazi yangu ya sikuhizi: Maroko. Indaba ikija Afrika ya Kaskazini nitajaribu. ChriKo (majadiliano) 12:40, 5 Novemba 2013 (UTC)Reply
Sawa kabisa, Ndugu ChriKo, nakuelewa. Hata mimi sitaweza kuhudhuria. Gharama ya kwenda Afrika Kusini kutoka Nairobi ni sawasawa na ile ya kwenda Ulaya. Mzee Kezilahabi alivyoandika, "Dunia Uwanja wa Fujo". Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 06:12, 6 Novemba 2013 (UTC)Reply

Edits

hariri

ChriKo, nimefurahi sana kuona edits zako. Unajenga habari za maana sana ! Asante! 23:21, 20 Januari 2014 (UTC)

Usijali ndugu, kwa furaha! ChriKo (majadiliano) 23:46, 20 Januari 2014 (UTC)Reply
Nisamehe - ni mimi Kipala (majadiliano) 06:18, 21 Januari 2014 (UTC)Reply
Ah Kipala, salaam. Sikupata habari zako kwa muda. Natumaini u mzima.ChriKo (majadiliano) 12:20, 21 Januari 2014 (UTC)Reply

Update on Upcoming Wiki Indaba Conference

hariri

My name is Rexford Nkansah, currently serving as a Wikipedian in Residence at the Africa Centre in Cape Town.

The Wikimedia Foundation has shared with us the incredible number of edits that you have done on this Wikipedia. You have are one of those with the high contribution to this Wikipedia.

As one of the highest contributors to one of the languages of the African continent, I want to inform you about the upcoming Wiki Indaba Conference which is similar to Wikimania, however, its designed by Africans for Africans.

This message is to inform you about scholarship to attend application currently open. You're invited to apply for scholarship to attend this conference.

Please see the main Wiki Indaba Website for more details on Eligibility and Deadline – look at www.wikiindaba.net for more details. And like the facebook page for updates.

Please don't hesitate to get in touch should you have any questions.

my contact is rexford[@]wikiafrica.net

Naomba ushirikiano wako!

hariri

Mpendwa, nakuomba uangalie baada ya siku 2,3 kurasa hizi mbili:

1. Wikipedia:Wakabidhi#Kusafisha_orodha_ya_Wakabidhi_mwaka_2014
2. Wikipedia:Ukurasa_wa_jumuia#Wiki_Indaba_2014

Kuhusu 1) napendekeza kuwachagua wakabidhi wapya na kuondoa wale waliomo katika orodha ya wakabidhi lakini hawakuwepo tangu miaka 2.

Kuhusu 2): nahitaji msaada na mawazo yenu. Nitashiriki kwenye mkutano wa Wikimedia mwezi wa Juni. Inaonekana mimi ndipo mchnagiaji wa pekee kutoka Wikipedia yetu. Ninajitahidi kupeleka mawazo ya jumuiya yetu. Naomba michango!

Nitaongeza karibuni mawazo yangu kuhusu mambo ninayoona kuwa na maana kwa mtazamo wangu. Ujumb huu natuma kwa wachangiaji wanaoonekana katika orodha ya wachangiaji hai waliochangia zaidi ya mara 3 katika siku 30 zilizopita!

Ndimi wako Kipala (majadiliano) 20:18, 13 Mei 2014 (UTC)Reply

Kipala salaam. Nakushukuru kunipendekeza kwa kuwa mkabidhi. Hata sasa nimekataa, lakini nafikiri siwezi kuendelea kukataa. Kama watu wa kutosha wakisema ndiyo nitafanya bidii. Natumaini kwamba nitapata hatua ya kutosha.
Kuhusu mkutano, nilitaka kwenda lakini kwa bahati mbaya nilipata kazi ya ushauri wakati huo huo (si mbaya sana kwa mfuko wangu bila shaka). Nafikiri ni lazima uzungumze kuhusu shida ya kupata wachangiaji kwa Wikipedia ya Kiswahili. Nadhani ni sawa kwa lugha nyingine za kiafrika. Ninajua kwamba ni hivyo kwa ile ya Wolof. Tunahitaji waafrika wa kike hasa kwa wachangiaji, ijapo hata nambari ya waafrika wa kiume si kubwa sana. Nimejaribu tangu miaka bila mafanikio mengi. Tangu mwaka uliopita mtu fulani huko Kenya anasaidia kutafuta wachangiaji, lakini hajafanikiwa. Watu wengi huuliza mara moja kama watalipwa. Tukisema hapana hatusikii habari zao tena kwa kawaida. Tunahitaji mpango mbunifu ili kuhimiza vijana hasa wakuwe wachangiaji. Na labda tungelipa watu mara kwa mara, lakini ni ya kukanganya.
Heri kwako! ChriKo (majadiliano) 20:28, 14 Mei 2014 (UTC)Reply
Kwanza nafurahi ya kwmaba umekubali kuwa mkabidhi. Kuhusu Joburg: mwenyewe sipendezwi na kuwalipa watu - lakini naweza kuitaja kama hoja. (ingawa neno "kukaganya" sijaelewa). Binafsi naona maana ya kuchangia kama kazi kwa wakati ujao. Hali jinsi ilivyo sasa ni chombo kinachotumika tayari na watu - naona karibu lakhi 1 kila siku! (http://stats.wikimedia.org/EN_Africa/TablesPageViewsMonthlyCombined.htm). Kila tunapoboresha watu wanaona. Idadi ndogo ya wachangiaji kwangu ni mazingira magumu.. yatakayobadilika. Kipala (majadiliano) 12:30, 19 Mei 2014 (UTC)Reply
Sawasawa, hakuna shida. ("Kukanganya" ni kama "kutatiza") ChriKo (majadiliano) 21:08, 20 Mei 2014 (UTC)Reply

Kura kwa Malangali

hariri

Salaam, Ndg ChriKo. Nilivyoandika kwenye ukurasa wa Wakabidhi, nimefurahi sana kuwa Ndg Malangali amerudi kwetu. Sasa ungeweza kutafakari kura yako tena kuhusu kumwondolea haki au la. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 07:30, 20 Mei 2014 (UTC)Reply

Ndg Tabita salaam. Asante kwa kunijulisha. Nimebadilisha kura yangu. ChriKo (majadiliano) 21:15, 20 Mei 2014 (UTC)Reply

Mbwa na jamaa vs Canidae

hariri

Salaam ChriKo naona sasa tu kuna mifumo miwili, moja chini ya Mamalia ni "Majina ya mamalia kwa Kiswahili" . Nimeigundua katika orodha mbili za Jamii:Mbwa na jamaa upande moja na Jamii:Canidae. Ulilenga nini? ni sawa kuziweka pande zote mbili au tujenge utaratibu kivipi? Kipala (majadiliano) 20:06, 31 Mei 2014 (UTC)Reply

Salaam Kipala. Nimeweka njia mbili za kufika ukurasa fulani wa wanyama au mimea: kupitia majina ya Kiswahili au kupitia majina ya sayansi. Ukitazama vizuri utaona majina ya Kiswahili tu katika jamii Mbwa na jamaa, na majina ya sayansi tu katika jamii Canidae. Natumaini ni sawasawa. ChriKo (majadiliano) 21:05, 31 Mei 2014 (UTC)Reply

Uko wapi?

hariri

ChriKo, samahani nikiuliza swali la binafsi. Je uko Ulaya? Maana naangalia takwimu kwa ajili ya somo langu kwenye mkutano wa WikiIndaba; naona takwimu ya kuwa asilimia 24 za hariri zetu zatoka "Europe unspecified". Ilhali "Iran" (=mimi) inaonyeshwa kwa 15% nafikiri wewe labda umo katika hizi 24%. Ni kweli wewe? (Nyingine zinazotajwa ni Tanzania 30% = nadhani Muddy, Riccardo na wengine moja-moja, Canada 5% (?), Italy 4 % (?), USA 3 %...)

Kipala, usijali. Hii si siri. Kwa kweli, ninasafiri sana, lakini siko katika Ulaya mara nyingi. Takriban 60% ya wakati niko Maroko, 25% huko Kenya na mabaki katika nchi nyingine, Afrika hasa. ChriKo (majadiliano) 10:03, 4 Juni 2014 (UTC)Reply
Nashangaa kwamba nchi ya Kenya haijatajwa katika takwimu ya Kipala, hasa kama ChriKo, unasafiri kwetu mara kwa mara, tena nami naishi hapa Kenya 80% za muda wangu wote. Labda tuangalie orodha hii mwezi kwa mwezi. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 10:48, 4 Juni 2014 (UTC)Reply

Jumuiya

hariri

Salaam, naomba uangalie hapa Wikipedia:Ukurasa_wa_jumuia#Salamu_kutoka_mkutano_wa_Wikiindaba_mjini_Johannesburg.2C_Afrika_Kusini Kipala (majadiliano) 11:17, 24 Juni 2014 (UTC)Reply

Virusi

hariri

Ndugu, kwanza nakupongeza kwa kazi zako. Sizipitii sana kwa sababu si mtaalamu wa biolojia. Mimi na wewe tunachangia Wiki katika mada tofauti, ila kwa lengo moja. Juzi nilipendekeza tujadili msamiati virusi kwa kuwa unasumbua, lakini leo naona umebadilisha virusi vi... kwenda virusi i... Nimechunguza katika kamusi za hivi karibuni, lakini hazikubali sahihisho hilo. Zinasemba ngeli yake ni vi. Isitoshe kamusi mbili zinakubali hata kirusi katika umoja. Ni kweli kwamba virusi ni neno la Kizungu, na halianzi kwa vi- kwa sababu ya ngeli, lakini katika maisha ya kila siku matumizi ni kama haya. Wasalamu. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:47, 18 Agosti 2014 (UTC)Reply

Baada ya kuandika hivyo, nimekuta jibu lako katika Majadiliano ya Ebola. Basi, naongeza kwamba lugha mara nyingi haina mantiki. Inakwenda na watu ambao mara nyingi hawaelewi asili ya maneno. Tunaweza kupinga kwa muda, k.mf. wanaposema "Ana malaria mengi", lakini hatimaye hata wanaistilahi lazima wakubali. Kwa mfano kitabu na kibali si maneno ya ngeli ki-/vi-, bali i-/zi- kadiri ya Kiarabu, lakini nana atayatumia tena hivyo? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:53, 18 Agosti 2014 (UTC)Reply
Asante. Ndiyo, mara nyingi lugha hazina mantiki. Nimekupa hoja yangu, lakini najua kama nimeshindwa. Watu wameanza kutumia kirusi/virusi. Kipala alijaribu pia, lakini hata yeye ameshindwa. Angalia: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/75780-virusi-vya-au-virusi-ya-za.html. ChriKo (majadiliano) 21:30, 18 Agosti 2014 (UTC)Reply
Samahani kama sishiriki sana katika majadiliano haya, niko safari sasa Marekani kumtembelea kijana wangu nakaa hasa kwenye makambi (camping) na intaneti inapatikana mara chache tu. Ni kweli ya kwamba watu wasio wachache wanaona "VIRUSI" kuwa katika ngeli ya ki-vi ingawa sijaona mtaalamu yeyote kusema hivyo.
Basi naona mawili: A) inafaa kuangalia jinsi watu wenyewe wanavyosema (maana mimi ni mluteri na mzee wetu alisema "sharti kutazama midomo ya watu") B) inafaa pia kuwakumbuka Waswahili (yaani watumiaji wa lugha) wasiozoea Kiswahili sanifu kwa namna yoyote kama huko Kenya au Kongo. Kutokana na A na B naona haina kasoro tukiendelea kutumia virusi moja - virusi nyingi maana wote wanaelewa hata kama wengine wanalalamika.
Lakini kama mchangiaji fulani anaona tofauti basi tumwache. Menginevyo siku ile Kiswahili sanifu inayoeleweka na kukubaliwa kitatokea tunaweza kusahihisha kila kitu. Mnaonaje? Kipala (majadiliano) 05:57, 20 Agosti 2014 (UTC)Reply
Poleni kwa zogo. Mnafikiria sana juu ya hizi lugha. Nionacho mimi hapa ni A) Mmegubikwa na tafsiri halisi ya Kiingereza - hivyo mnajaribu kuleta maana ya Kiingereza hata katika istilahi za Kiswahili. Kama imeshindikana kwa Kiingereza - si lazima kwa Kiswahili ishindikane! B) Nimeona wataalamu kabisa wanasema virusi na kirusi. Tena naenda mbali zaidi Mwalimu wangu wa bailojia alikuwa anazungumza lugha hizi za kirusi na virusi mara kwa mara. HITIMISHO: Kwetu tunasema virusi/kirusi. Yaani, tunatumia lugha za wingi na umoja kana kwamba hili neno tumelizaa sisi! Hadi raha! Kila la kheri.--MwanaharakatiLonga 08:04, 20 Agosti 2014 (UTC)Reply
Kama nimeshasema, nafikiri muda umekwisha. Hatuwezi kusimamisha tsunami, hata kama wataalamu wa lugha ya Kiswahili wataamua kwamba virusi ni 9/10. Lakini kila mtu afanye vile anafikiri ni bora. ChriKo (majadiliano) 10:35, 21 Agosti 2014 (UTC)Reply
Mzee ChriKo hapo utakuwa umesusa. Na hilo halikuwa lengo! Kila la kheri..--MwanaharakatiLonga 07:14, 22 Agosti 2014 (UTC)Reply
Sikuwa na nia ya kusababisha zogo, ila kuona namna ya kwenda pamoja tusianze vita vya uhariri. Nadhani kitu kikubwa ni kwamba huku umepita moka kwa moja msamiati VVU kwa HIV, na tafsiri yake ni Virusi Vya Ukimwi. Ndugu Kipala, ukitaka kuona wataalamu waliopitisha Kirusi, kuna Concise Dictionary by Snoxwall and Mshindo, pia Kamusi Teule. Hata mimi sipendi sana, lakini tunajikuta katika hali hii. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:32, 22 Agosti 2014 (UTC)Reply
Ndiyo Riccardo, tusianze vita vya uhariri. Na la Muddyb, sitaki kususa. Nitaacha kusahihisha "virusi vya" au "kirusi cha", lakini mimi mwenyewe nitaendelea kuandika "virusi ya" na "virusi za". Hata maneno mengine, kama "vita", yalikuwa katika ngeli mbili, walau zamani. ChriKo (majadiliano) 18:43, 24 Agosti 2014 (UTC)Reply
Bado niko mbali likizoni (yaani siwezi kuangalia kila siku) lakini napenda kusema mawili:
A) asante Muddy na Ricardo kwa kutuelimisha ya kwamba Kirusi siku hizi si lugha pekee mbali mdudu pia (pole lakini!)
B) Menginevyo namwunga mkono Chriko. Sioni hasara tukiacha yote kandokando (yaani kirusi cha na virusi ya) ilhali tu wasomaji wanaelewa. Hata kama wachache wanashagaa. Kama msemaji wa Kirusi anapata kirusi cha mafua, pole yake! Hata niko tayari kuangalia filamu kwa njia ya kideo, kama ni lazima sana. Pia namshukuru Mungu kila siku kwa sababu sijawahi kuona mwenyewe hata kita kimoja mwaishani mwangu. -- Basi, niache michezo hii maana lugha yangu ya Mama (Kijerumani) haina mantiki yoyote katika sarufi (der - die - das) kwa hiyo sina haki ya kulalamika uhaba wa mantiki kwa Kiswahili. (Ila tu zamani mwalimu wangu alidai iko...) Kipala (majadiliano) 05:50, 25 Agosti 2014 (UTC)Reply

Kupakia mafaili, Sogora ya kupakia?

hariri
 

Hello! Sorry for writing in English. As you're an administrator here, please check the message I left on MediaWiki talk:Licenses and the village pump. Thanks, Nemo 19:22, 18 Septemba 2014 (UTC)Reply

Upangaji wa kurasa za Punda, Punda-Kaya, na Asinus

hariri

Habari yako ChirKo. Inaonekana nilifanya makosa kwa kusogeza matini ya orodha ya spishi za Punda toka ukurasa wa Punda mpaka ukurasa wa Asinus. Naomba msamaha sana. Sasa, nafahamu ungependa kutumia ukurasa wa Punda kuwakilisha nusujenasi yote ya Asinus, na ukurasa wa Punda-Kaya kuwakilisha Punda afugwaye. Je, ninaelewa kwa usahihi unavyokusudi? Rberetta (majadiliano) 04:46, 26 Oktoba 2014 (UTC)Reply

Rberetta salaam. Umefahamu vizuri lakini hakuna haja kuomba samahani. Ulifanya vile ulifikiri ni bora. Lakini tunapendelea kurasa zenye vichwa kwa Kiswahili. Endelea kazi yako nzuri. ChriKo (majadiliano) 18:17, 26 Oktoba 2014 (UTC)Reply

Swali kuhusu mbinu ya viungo

hariri

Salaam ChirKo - nina swali jingine: Umeandika vigezo kadhaa vya oda za mamalia. Vigezo vichache vinatumia viungo nyoofu, kama hiki:

  • [[Paa (Bovidae)|Cephalophinae]] --> Paa (Bovidae)

huko vingine vinatumia kurasa za kuelekeza, kama hiki:

  • [[Cephalophinae]] --> #REDIRECT [[Paa (Bovidae)]] --> Paa (Bovidae)

Tukiendelea mbele, ungependelea mbinu ipi? Ninafikiri kurasa za kuelekeza ni bora, kwani mbinu hii itadumu zaidi kama mtu mwingine aje kuandika makala yenye majina ya Kilatini.

Nikihariri vigezo vyako kusahihisha viungo ambavyo vimevunjika, ningependa kufanya kawaida hivyo viungo pia. Je, unakubali? Rberetta (majadiliano) 15:46, 28 Oktoba 2014 (UTC)Reply

Rberetta salaam. Tafadhali nieleze maana ya "kiungo nyoofu". Isipokuwa hiyo nani ameweka Cephalophinae kama ukurasa wa kuelekeza? Ukurasa huu haupo bado. Au umeiandika kama mfano? Unanikumbusha nimwumbe ukurasa huu. Pengine ukurasa wa kuelekeza ni bora lakini sikubali kwa mfano wa majina ya Kilatini. Sitaki watu waandike kurasa zenye vichwa kwa Kilatini isipokuwa kama hakuna tafsiri katika Kiswahili. ChriKo (majadiliano) 22:48, 28 Oktoba 2014 (UTC)Reply
Pole - nilieleza vibaya. Nilitumia ukurasa wa Cephalophinae kama mfano tu - ndiyo kabla ya wewe kuandika ukurasa huo, haukuwepo. Niliandika "kiungo nyoofu" kumaanisha "direct link", kama hiki:
  • [[Paa (Bovidae)|Cephalophinae]] --> Paa (Bovidae)
Kiungo hiki chafanya kazi bila kutumia ukurasa wa kuelekeza. Sasa hivi, kiungo hiki kipo katika Kigezo:Artiodactyla. Kigezo:Lagomorpha inatumia viungo na kurasa za kuelekeza, kama hiki:
  • [[Bunolagus]] --> #REDIRECT [[Sungura]] --> Sungura
Katika vigezo ulivyoandika, viungo vingi ni viungo nyoofu, na viungo vichache vinatumia kurasa za kuelekeza. Lakini, umefanya kazi nyingi kuumba kurasa nyingi za kuelekeza, kwa hiyo mimi sikujua mbinu uliyopendelea.
Mimi sitaki kukushawishi kutumia mbinu yoyote - nataka kujua tu pendekezo lako, na nitafuata hilo pendekezo.
Pia - tafadhali nifundishe njia sahihi ya kusema "direct link" kwa Kiswahili!
Ok, sawasawa tu. Ninatumia ukurasa wa kuelekeza nikifikiri kwamba kuna uwezekano mzuri kwamba mtu fulani atatafuta neno hili katika Wikipedia ya Kiswahili. Na kama likiwa jina kwa Kilatini, faida ya ukurasa wa kuelekeza ni nafasi ya kuingiza jamii. Nadhani uliona kwamba ninatumia jamii za majina kwa Kilatini na jamii za majina kwa Kiswahili ili kufika kwenye ukurasa fulani wa kiumbehai.
Swali lako kuhusu "direct link" ni ngumu kidogo. Ningependekeza "kiungo cha moja kwa moja".
ChriKo (majadiliano) 23:47, 29 Oktoba 2014 (UTC)Reply

Naomba ushauri wako kuhusu muundo wa kurasa za wanyama

hariri

ChirKo Salaam. Nimekuwa nikifanya kazi kufanya kawaida kurasa zote za familia Bovidae. Labda umekuwa ukiniangalia. Sasa, nipo karibu na kuimaliza kazi hii, na naomba maoni na ushauri zako. Kama kuna kitu chochote ambacho ungependa kufanywa tofauti, tafadhali niambie, na nitafanya hivyo. Kwa mfano:

  • Kurasa chache zilikuwa zikitumia <small> kwenye maelezo ya ngazi za uainishaji. Niliondoa <small> kuzifanya kawaida kurasa hizo. Lakini, labda ungependa <small> kutumiwa? Kama hivyo, hamna shida - nitazibadilisha zote.
    • Mfano wa matumizi ya <small> ni: "Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
  • Nilianzisha kurasa tano zilizo na majina ya Kilatini, kwa sababu sijui majina ya Kiswahili yangefaa. Kurasa hizo ni Alcelaphinae, Antilopinae, Bovinae, Hippotraginae na Reduncinae. Wewe ukijua majina ya Kiswahili ambayo ungependelea, tafadhali niambie na nitazisogeza kurasa hizo.
  • Nilianzisha kurasa mpya kadhaa za kuelekeza kwa ajili ya jenasi na nusufamilia kadhaa ambazo hazikuwa na kurasa. Sasa, [[Jamii:Bovidae]] inakuwa kubwa kidogo. Ungependa nibadilishe kurasa za kuelekeza kutumia ngazi mbili - ngazi ya kwanza ikitumiwa kwa nusufamilia zote, na ngazi ya pili ikitumiwa kwa jenasi zilizo chini ya ngazi ya nusufamilia? Au niziache kama zilivyo?

Kukuhabarisha, Orodha kamili ya kurasa za familia ya Bovidae ninazingatia ni:

Alcelaphinae, Antilopinae, Baisani, Bovinae, Choroa, Digidigi, Dondoo, Hippotraginae, Kondoo-kaya, Kongoni, Korongo_(Bovidae), Kuro_(jenasi), Maksai_aktiki, Mbuzi, Mbuzi-kaya, Ng'ombe, Ngurunguru, Nyamera_(jenasi), Nyati_wa_Afrika, Nyumbu, Paa_(Bovidae), Pofu_(jenasi), Pongo, Reduncinae, Suni, Swala, Swala_pala, Tandala, Taya_(mnyama), Tohe

Rberetta salaam. Ndiyo, niliangalia kazi yako, ni kazi nzuri. Endelea tu. Sina malalamiko mengi. Nisipopenda kitu, ninakibadilisha, hakuna shida. Halafu utaona vile ninaipenda. Jambo hili la kuweka maelezo ya ngazi kwa herufi ndogo nafikiri ni fikira nzuri. Ukitaka badilisha tu yote, lakini itakuwa kazi kubwa.
Kurasa zenye majina ya Kilatini ni sawa isipokuwa majina ya Kiswhahili. Hata kwa lugha nyingine, kama Kiingereza, familia na nusufamilia hazina majina ya kienyeji. Lakini nadhani kwamba hakuna haja kuweka spishi zote za nusufamilia ndani ya ukurasa wake. Weka tu majina ya jenasi. Nimebadilisha ukurasa wa Alcelaphinae kukuonyesha jinsi ningefanya kazi hii. Mwsihowe, usisahau kutia sahihi ukiandika kitu katika majadiliano (~ nne). ChriKo (majadiliano) 23:50, 10 Novemba 2014 (UTC)Reply
Asante ChirKo. Sawa, nitatumia mabadilisho uliyofanya katika Alcelaphinae kama mfano, na nitafanya hivyo katika kurasa mpya nilizoanzisha. Lakini niliona suala moja - ulibadilisha [[Jamii:Bovidae]] kuwa [[Jamii:Alcelaphinae]]. Je, ulikusudi kufanya hivyo? Alcelaphinae siyo nusufamilia ya Alcelaphinae yenyewe, ni nusufamilia ya Bovidae. Au mimi sielewi? Rberetta (majadiliano) 01:02, 11 Novemba 2014 (UTC)Reply
Ndiyo, ni kweli kwamba Alcelaphinae ni nusufamilia ya Bovidae, lakini ukurasa wa nusufamilia fulani lazima uwemo katika jamii ya nusufamilia yake. Halafu jamii hii itakuwamo katika jamii ya familia yake. ChriKo (majadiliano) 11:07, 11 Novemba 2014 (UTC)Reply
Sawa - naelewa. Nilitumia mfano wako kubadilisha kurasa zote za nusufamilia. Asante. Rberetta (majadiliano) 17:50, 11 Novemba 2014 (UTC)Reply

Aloe - Mshubiri

hariri

Salamu ChriKo, katika Majadiliano:Shishiyu kijana wa huko ameuliza swali kuhusu Aloe vera. Ningependa kusaidia lakini si mtaalamu. Unaonaje: Ingekuwa sawa kuanzisha makala ya "Mshubiri" kwa jenasi "Aloe" halafu "Aloe vera" kama makala ya spishi? Nimekuta hii: Traditional Food Plants: A Resource Book ambako mwandishi anaona jina "mshubiri" pia kwa Aloe maculata - prev. A. saponaria lakini kufuatana na en:Aloe maculata maculata ni mmea wa Afrika Kusini pekee (siku hizi pia mmea wa mapambo Marekani).

Halafu: tuna neno kwa "succulents"? "Mimea ya utomvu"? "Mimea chapachapa /chepechepe" (pendekezo la KAST). Una ushauri? Asante Kipala (majadiliano) 14:53, 29 Novemba 2014 (UTC)Reply

Kipala salaam. "Mshubiri" au "msubili" ni majina kwa spishi kadhaa za Aloe. Nimepata "kisimamleo" pia, lakini sijui ni spishi gani. Kwa asili majina ya kwanza yalitumiwa kwa spishi za Afrika ya Mashariki, lakini nafikiri tunaweza kuyatumia kwa spishi zote sasa. Kwa hivyo, hata Aloe maculata ni "mshubiri". Nitajaribu kupata nafasi kuanzisha makala yake.
Tafsiri ya "succulent plant" si rahisi. Niliona tafsiri kadhaa lakini sizipendi. Ni wazi kwamba wafasiri/wapendekezaji wengi hawafahamu biolojia sana. Sijui kwamba istilahi moja imeshazagaa sana katika shule na vyuo nyingi. Mimi ninapenda "mmea mwenye majani manono". ChriKo (majadiliano) 20:25, 29 Novemba 2014 (UTC)Reply
Asante kwa maelezo. makala iliyotafutwa hasa ilikuwa kuhusu Aloe vera. Hapa sioni tatizo kutumia jina hili la Kilatini maana inatumiwa kwa Kiswahili siku hizi. ila tu kwa maelezo sawa tutumie mshubiri kwa jenasi Aloe. Kuhsu succulentes sina upendeleo wowote ila ti swali: je "mmea mwenye majani manono" ni kweli tunachotaka? Si mtaalamu lakini nikiangalia maelezo mimea hii inatunza maji mara nyingi kwenye majani, lakini mengine pia katika shina. Nimeelewa vema? Sasa kama tunatumia lugha inayotaja majani pekee - je tunaweza kuingiza pia mimea inayotunza maji shinani? Kipala (majadiliano) 17:28, 30 Novemba 2014 (UTC)Reply
Ndiyo, "Aloe vera" inaweza kuwa kichwa cha makala. Kuhusu "succulents", ukitaka kutumia uhakika kwamba mimea hii ina utomvu mwingi katika majani na mashina, basi sema "mimea wenye utomvu mwingi". Lakini kwa mtazamo mwangu, hakuna tafsiri fupi ambaye inajulisha maana yake kabisa. Kwa hivyo ninapendekeza kuswahilisha (kuna neno kama hili?) istilahi hii: "sukulenti". Maneno mengi yameswahilishwa. ChriKo (majadiliano) 18:14, 30 Novemba 2014 (UTC)Reply
Labda "sukyulenti"? Silabi "kyu" ni adimu sana katika Kiswahili, lakini neno lingine lililo na silabi hayo ni neno lililoswahilishwa pia "molekyuli". Rberetta (majadiliano) 18:45, 30 Novemba 2014 (UTC)Reply
Tukichagua "sukyulenti", basi tunafanya "barbarishaji" (shenzishaji?) mbili: kwanza uingerezishaji kutoka Kilatini na halafu uswahilishaji. Kwa sababu mimi si Mwingereza, siipendi sana. ChriKo (majadiliano) 19:31, 30 Novemba 2014 (UTC)Reply
☺☺ Unasema kweli! Pia ni ya ukweli kwa mfano wa molekyuli - Kilatini lilikuwa "molecula" --> swahilisha --> "molekula". Kwa bahati mbaya, wasemaji wengi sana wa Kiswahili wanalazimishwa kusoma Kiingereza, yakisababisha Kiswahili kuingerezishwa. Haya pia yalikuwa ya kishenzi... Rberetta (majadiliano) 00:41, 1 Desemba 2014 (UTC)Reply
Kuhusu "upijinizaji" naunga mkono. Haya twende kwa "sukulenti" pamoja na "mimea wenye utomvu mwingi" (redirect). "Mimea nono" ingekuwa fupi zaidi na kulingana na majina mafupi katika lugha za Kizungu (Fettpflanze, fat plant, vetplant) lakini sijaona lugha kama hii kwa Kiswahili Kipala (majadiliano) 06:43, 1 Desemba 2014 (UTC)Reply


Kuhusu mkutano wa Machi 2015 na mawasiliano na WMF

hariri

Salaam naomba utazame hapa: Majadiliano_ya_Wikipedia:Wakabidhi#Mawasiliano_na_ofisi_ya_WMF_-_Wikimedia_Foundation_.2F_Asaf_Bartov na kuchangia. Kipala (majadiliano) 09:56, 3 Desemba 2014 (UTC)Reply

Hua - Columbidae

hariri

Salaam Christiaan naomba uangalie Majadiliano:Hua nimeshauliza huko je hii makala kweli inahusu streptopelia tu... Wakati ule nilitaka kuongeza jinsi nilivyotaja, sasa niangalia upya kwa sababu niko kwenye makala 1000 na kama ni sawa kuunganisha na Columbidae, basi - naweza kufuta hii kwenye orodha yangu. Unasemaje ? Kipala (majadiliano) 20:58, 14 Desemba 2014 (UTC)Reply

Salaam, nimejibu swali lako kwenye Majadiliano:Hua. Spishi za Columbidae zina majina kadhaa: njiwa, hua, tetere, kuyu, fumvu, pugi na huji. ChriKo (majadiliano) 18:41, 15 Desemba 2014 (UTC)Reply

Matamvua?

hariri

Salaam Chriko, naandika sasa juuu ya mfumo wa upumuaji na upumuo. Samaki huwa na matamvua (gills), lakini naona unatumia neno hili katika makala juu ya Bundi (Strigidae). Tutofautishe namna gani? Kipala (majadiliano) 20:48, 12 Juni 2015 (UTC)Reply

Kipala salaam. Hiki ni kitu ambacho sijamaliza. Kwa kweli neno "matamvua" lina maana nyingine pia, k.m. "fringe, edge" (maana ya asili nadhani). Nilitaka kutafsiri "serrated edge" lakini sikuweza na baadaye nimesahau kitu hiki. ChriKo (majadiliano) 09:54, 18 Juni 2015 (UTC)Reply

Mume na mke

hariri

Salamu nyingi kutoka Morogoro. Nimeona pendekezo lako la kuunganisha mume na mwanamume, mke na mwanamke. Kwa kweli sijaelewa sababu. Katika lugha nyingi kurasa hizo ni tofauti, k.mf. man na husband, woman na wife kwa Kiingereza. Mimi ni mwanamume lakini sijawahi kuwa mume, wala sina mpango... --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:13, 29 Juni 2015 (UTC)Reply

Salamu kutoka Nanyuki ambapo kwetu muunganisho kwa mtandao ni mbaya. Ninaona vile unataka kusema. Ok, nitaondoa ombi la kuunganisha. Lakini fafanua tafadhali katika makala hizi. ChriKo (majadiliano) 20:35, 30 Juni 2015 (UTC)Reply

Silausi Nassoro

hariri

Ndugu Christiaan, salaam. Nimeanza kuchoka na Silausi alivyochoka pia Ndg Muddyb. Huyo Silausi akiendelea kubadilisha makala bila kufuata mashauri yetu na kanuni za Wikipedia:Umaarufu, nitamzuia kwa muda kadhaa. Bahati mbaya inaonekana kama ataanzisha akaunti nyingine tena alivyofanya baada ya kuzuiliwa kama Mtumiaji:Lusajo Chicharito Brown. Unaonaje? Wasalaam, Baba Tabita (majadiliano) 16:46, 29 Juni 2015 (UTC)Reply

Salaam ndugu Oliver. Hata mimi nimechoka na huyo Silausi. Mzuie basi asichange tena. ChriKo (majadiliano) 20:42, 30 Juni 2015 (UTC)Reply

Tafadhali uangalie jamii kuhusu mfumo wa kuanzisha makala

hariri

Mpendwa, nakuomba kuaangalia ukurasa wa Jumuiya. Tuliomba wikimedia ya kutpa mfumo wa kuzuia watumiaji wasiojiandikisha wasianzise makala mapya. Kusudi lilikuwa kupunguza idadi ya makala mabaya yasiyotosheleza masharti ya wikipedia ilhali tuko wachache mno kuziangalia. Wikipedia kubwa kadhaa zinatumia utaratibu huu (kama en:wikipedia) lakini sisi tunapaswa kupeleka ombi kwa kamati fulani. Kamati hii wametupa nafasi kwa kipindi ha miezi 6 tu inayokwisha karibuni. Sasa wanakamati wamekuja wanadai tujieleza au watarudisha mfumo huu nyuma. Mimi nikiwa 1 kati ya wachache wanaochugulia makala mapya naona itaturudisha nyuma. Naomba mchangie! Sanaaaaa!! Kipala (majadiliano) 23:35, 10 Septemba 2015 (UTC)Reply

Kidusia / Kimelea

hariri

Salaam ChriKo, nimetunga makala mafupi kuhusu vimelea. Nimeona ya kwamba wewe unapendelea Kidusia. Nikitazama kamusi naona kila sehemu kimelea, isipokuwa kwenye KAST inayotumia lemma "Kidusia (pia kimelea)". Hata nikitafuta kupitia googel napata mara nyingi kilemea. Sasa ukiona kudusia ni kawaida katika fani ya biolojia basi tuhamishe yote kule. Naomba ushauri wako! Kipala (majadiliano) 19:15, 2 Desemba 2015 (UTC)Reply

Kipala salaam. Ndiyo, najua kwamba takriban watu wote hutumia "kimelea" kwa kutafsiri "parasite" katika maana zote za neno la Kiingereza. Lakini neno kimelea linatoka kwa "kumelea" yaani kumea mahali popote na kufunika na kukaba mimea mingine ya shamba au bustani. Kwa hivyo kimelea kwa asili ni mmea unaomea namna hiyo. Baadaye neno limeanza kutumika kwa mmea unaomea juu ya miti (mimea hii huitwa virukia pia). Wakati wa karne ya 20 neno limekopwa kwa kueleza viumbehai ambavyo vinaishi au vinamea ndani ya viumbehai vingine na hata wanyama wanaoishi juu ya wanyama wengine au mimea mingine wakifyunza damu au utomvu. Naweza kukubali kutumia kimelea kwa kueleza vidubini na kuvu fulani, lakini kwa wanyama hapana. Neno "kidusia" ni bora kwa sababu linatoka kwa kudusa yaani kula kwa gharama ya wengine. Siku moja nitatunga makala kuhusu kidusia. Nafikiri wewe hujachanga makala yako kuhusu kimelea. Ukifanya nitajaribu kuiboresha. ChriKo (majadiliano) 23:42, 2 Desemba 2015 (UTC)Reply
Kimelea kipo tangu jana, pamoja mwelekezo kutoka kidusia. Menginevyo asante kwa maelezo kuhusu "kudusa", sijalijua neno sasa nimejifunza na kuelewa asili ya chaguo cha KAST iko wapi! Kipala (majadiliano) 06:19, 3 Desemba 2015 (UTC)Reply


Amerika ya Kusinii

hariri

Salaam Christiaan, naomba angalia hapa [[2]]. Nimejaribu kuteua majina ya wanyama hao wa pekee lakini sijui kama yanafaa. Sahihisha tu! Kipala (majadiliano) 10:02, 5 Machi 2016 (UTC)Reply


Steppe?

hariri

Salaam, natumaini ulikuwa na Pasaka njema! Siku hizi naangalia Urusi kwa sababu ya mgeni wetu.. Nahitaji neno kwa "steppe". Una ushauri? Mbuga wa manyasi? Pori ya manyasi? Pori manyasi? Porinyasi ? Kipala (majadiliano) 22:55, 7 Aprili 2016 (UTC)Reply

Salaam. Pasaka yetu haikuwa njema kama tulivyopenda kwa sababu mke wangu hajaweza kutembea bado. "Steppe" ni eneo la manyasi bila miti au lenye miti michache na kwa Kiswahili eneo kama hili linaitwa mbuga. Kama eneo likiwa na miti mingi zaidi linaitwa savana. Pori ni istilahi ya jumla au eneo lenye miti na vichaka. Kwa hivyo nadhani kwamba tafsiri nzuri ya "steppe" ni mbuga. ChriKo (majadiliano) 20:14, 8 Aprili 2016 (UTC)Reply
Asante kwa ushauri. Nimesita kutumia "mbuga" maana ni aina ya nchi inayopatikana Afrika. KWANZA Steppe ni aina ya nchi inayopatikana nje tabianchi ya tropiki. Vipi mbuga baridi? PILI nadhani mbuga ni steppe pamoja na aina za savannah, sivyo? Kipala (majadiliano) 19:14, 11 Aprili 2016 (UTC)Reply
Kipala, samahani kwa sababu sinakubaliani na wewe. Kwa maoni yangu ukweli kwamba "steppe" haipatikani hapa Afrika siyo sababu ya kutotumia neno "mbuga". "Steppes" ni aina za "grasslands" na katika sehemu nyingine za dunia zinaitwa "prairy", "cerrado" na "grass savanna". Na "grassland" ni mbuga kwa Kiswahili. Kama "pori" likitumika kumaanisha aina maalumu ya mandhari hili ni eneo lenye vichaka vifupi vyingi (kama "maquis" au "karoo"). Kwa hivyo nadhani kwamba kutumia istilahi mpya "pori ya manyasi" si wazo zuri. Ukitaka tumia "mbuga baridi". ChriKo (majadiliano) 22:04, 15 Aprili 2016 (UTC)Reply
Asante, twende mbuga baridi. Kipala (majadiliano) 14:07, 16 Aprili 2016 (UTC)Reply

Famouse Ukrainian People or maarufu Kiukreni

hariri
Hello ChriKo! Sorry for writing in English. I don`t understand Swahili. I ask you to contribute with translation into the Swahili language. Could you or other users of your wikipedia translate some articles, that dedicated for prominent figures in Ukraine. The list shown on the page Wikipedia:Makala zilizoombwa. It is equipped interlanguage links and given pronunciation on Latin alphabet.--Yasnodark (majadiliano) 11:36, 10 Aprili 2016 (UTC)Reply


Udachi, Uholanzi...

hariri

Salaam ChriKo safari hii nahitaji utalaamu wako si kuhusu wadudu au magugu lakini kuhusu majina yetu... Naomba uangalie makala ya Ujerumani rejeo la kwanza, ama nipa baraka au laana au afadhali sahihisho... --Kipala (majadiliano) 21:51, 25 Aprili 2016 (UTC)Reply

Kipala salaam. Sioni kosa lo lote. Ni mzuri. ChriKo (majadiliano) 15:47, 26 Aprili 2016 (UTC)Reply

msaada tafadhali

hariri

Please write here question in english language why me blocked in russian wikipedia, then wikipedia talk and then wikimail (they not understood what happened and just blocked everywhere) this very easy write (likely me block and in kiswahili wikipedia). CYl7EPTEMA777 (majadiliano) 08:13, 9 Mei 2016 (UTC)Reply

msaada tafadhali

hariri

Please write here (this talk user page) question in english language why me blocked in russian wikipedia, then wikipedia talk and then wikimail (they not understood what happened and just blocked everywhere) this very easy write (likely me block and in kiswahili wikipedia). CYl7EPTEMA777 (majadiliano) 22:11, 17 Mei 2016 (UTC)Reply

Majina ya wanyama

hariri

Jerry salaam. Asante sana kwa kuchangia makala kuhusu wanyama wa baharini. Lakini tafadhali hakikisha majina unayotumia. Unaweza kupendekeza majina mapya endapo hakuna majina kwa Kiswahili, lakini majina yaliyoko yana kipaumbele. Kwa mfano "papa kichwanyundo": ulibuni jina hili au linatumika kweli? Mimi, silijua. Ninajua "papa mbingusi" na "papa nyundo". ChriKo (majadiliano) 16:46, 3 Novemba 2016 (UTC)Reply


Asante ndugu. Nitazingatia ushauri wako. tafadhali naomba viungo vya wavuti za kamusi ili niwe nahakiki majina. siku njema - Jerry

Share your experience and feedback as a Wikimedian in this global survey

hariri
  1. This survey is primarily meant to get feedback on the Wikimedia Foundation's current work, not long-term strategy.
  2. Legal stuff: No purchase necessary. Must be the age of majority to participate. Sponsored by the Wikimedia Foundation located at 149 New Montgomery, San Francisco, CA, USA, 94105. Ends January 31, 2017. Void where prohibited. Click here for contest rules.


Kura kuhusu wikisource

hariri

Salaam kuna Pendekezo: Tuanzishe kitengo cha WikiSource NDANI ya wikipedia yetu unaombwa kuiangalia na kupiga kura!Kipala (majadiliano) 02:07, 29 Januari 2017 (UTC)Reply

Your feedback matters: Final reminder to take the global Wikimedia survey

hariri

(‘’Sorry to write in English’’)

WMCon 2017 Berlin

hariri

Ndugu, salaam. Nataka kukujulisha tu kwamba nimealikwa kuhudhuria Wikimedia Conference 2017, nami nikajisajili tayari. Sitahudhuria rasmi kwa ajili ya wikipedia yetu bali kama mwanakamati wa LangCom. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 20:57, 4 Machi 2017 (UTC)Reply

Ombi la MetaWiki

hariri

Salaam, Naomba munichangie msaada wa kukubali ombi langu la kupewa laptop kule Meta-Wiki. Kiungo hiki hapa. Wako,--MwanaharakatiLonga 13:17, 17 Machi 2017 (UTC) Reply

Mito ya Kenya

hariri

Asante kwa kuongeza majina mengine, ila nina wasiwasi kuhusu Kathita na Kazita: ni tofauti au ni uleule? Pia sijaelewa mistari ya mwisho, nadhani ni GPS, inakaaje. Napendekeza uongeze majina hayohayo katika en.wikipedia. Pia huo mto Mononoase, uliokuwepo tayari katika orodha, uko wapi? Siuoni kokote. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:12, 23 Novemba 2017 (UTC)Reply

Ni kweli, sikuona mfanano kati ya Kathita na Kazita. Huo ni mto mmoja tu. Ulitumia tahajia ya Kikikuyu. Lakini sijui Mto Mononoase. Nilimwona katika orodha kadhaa lakini bila viratibu vyake. Nimeshaondoa mistari ya mwisho. Nilikopi aridhio hili kutoka tovuti nyingine ili kunisaidia kuweka majina katika orodha. ChriKo (majadiliano) 19:20, 23 Novemba 2017 (UTC)Reply

Majadiliano:Khanga#Tahajia

hariri

Tafadhali pitia hapa.--MwanaharakatiLonga 09:56, 20 Desemba 2017 (UTC) Reply

KiDUDUMTU

hariri

Shikamoo! Naomba unisaidie kutujua jina la mdudu huyu kwa kiingereza na jina lake la kisayansi

Marahaba Dennis. Wakati ujao tafadhali weka ~~~~ kwa mwisho wa matini yako ili kuonyesha saini yako. Kuhusu swali lako, sijui jibu. Hata mimi nimejiuliza huyu ni mdudu gani? Niliangalia picha kwenye mtandao na nafikiri mdudu huyu ni mwana wa familia ya kunguni. Kwa Kiingereza huitwa "true bugs" au "typical bugs" na kwa kisayansi ni nusuoda ya Heteroptera. Lakini siwezi kusema ni spishi gani. ChriKo (majadiliano) 19:30, 29 Januari 2018 (UTC)Reply

Sherehe!!!

hariri

Angalia hatua aliyoifikisha Ndugu Riccardo: Matukio ya hivi karibuni. Sherehe!!! --Baba Tabita (majadiliano) 10:02, 17 Machi 2018 (UTC)Reply

Ndiyo, niliona. Ni mzuri sana. ChriKo (majadiliano) 15:53, 17 Machi 2018 (UTC)Reply


Mkabidhi mpya, pendekezo

hariri

Naomba angalia hapa Wikipedia:Jumuia#Mkabidhi_kwa_Jadnapac. (Halafu: je ungekuwa na nafasi ya kuja Dar mwisho wa Novemba Ijumaa-Jpili kwa warsha ya hapa? basi niandikie email) Kipala (majadiliano) 21:37, 30 Oktoba 2018 (UTC)Reply

Mlawangi

hariri

Salaamu ChriKo, sasa hivi nimeondoa neneo "mlawangi" katika makala mnyama maana siwezi kuithibitisha. Sasa naona wewe ulitumia neno hili katika makala Nguruwe-kaya. Umepata istilahi hii wapi? Kipala (majadiliano) 07:28, 29 Januari 2019 (UTC)Reply

Kipala salaam. Ni sawasawa. Hata mimi sifahamu etimolojia yake. Lakini matini ya Nguruwe-kaya ni yako. Mimi nilibadilisha kichwa tu (kichwa cha asili kilikuwa Nguruwe). Nafikiri umepata "mlawangi" katika KAST. Mimi ningesema "mlamingi" ama kitu kama hiki. KBPC inapendekeza mlavyote. ChriKo (majadiliano) 12:45, 29 Januari 2019 (UTC)Reply
Naona "walavyote" itaeleweka vizuri sana, jinsi ilivyo pendekezo la KBFK.Kipala (majadiliano) 09:35, 30 Januari 2019 (UTC)Reply

Document your culture with Wiki Loves Love 2019 and win exciting prizes!

hariri
 

Please help translate to your language

Africa has many beautiful festivals, ceremonies and celebrations of love and we need your help to document these! They are the core part of African culture and in order to make sure this way of life followed by our ancestors remain among us, we need to have them online to make sure they are preserved. Join hands with Wiki Loves Love that aims to document and spread how love is expressed in all cultures via different rituals, celebrations and festivals and have a chance to win exciting prizes!! While uploading, please add your country code in the Wikimedia Commons upload wizard. If you want to organize an on-site Wiki Loves Love event, then contact our international team! For more information, check out our project page on Wikimedia Commons.

There are several prizes to grab. Hope to see you spreading love this February with Wiki Loves Love!

Imagine...The sum of all love!

Wiki Loves Love team 07:34, 4 Februari 2019 (UTC)

Farasi

hariri

Ndugu, ukipenda kuunganisha farasi na farasi mwitu, sina pingamizi, ila kwa Kiingereza na lugha nyingine mbalimbali kurasa hizo ni tofauti. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:35, 29 Julai 2019 (UTC)Reply

Community Insights Survey

hariri

RMaung (WMF) 00:48, 7 Septemba 2019 (UTC) Reply

Reminder: Community Insights Survey

hariri

RMaung (WMF) 18:56, 20 Septemba 2019 (UTC) Reply

Reminder: Community Insights Survey

hariri

RMaung (WMF) 15:27, 4 Oktoba 2019 (UTC) Reply


Jenga / Wikimedia Summit

hariri

Tafadhali angalia na changia hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Jumuia#Jenga_Wikipedia_ya_Kiswahili_-_mkutano_Berlin_na_mawazo_kuhusu_Wikimedia_2030_strategy Kipala (majadiliano) 13:14, 17 Desemba 2019 (UTC)Reply

Spam

hariri

Asante kwa kusahihisha uchafu. Je unajua una pia uwezo wa kuzuia URL za aina hii? Nimeweka sasa hivi block ya milele. Usisite. Kipala (majadiliano) 06:53, 28 Machi 2020 (UTC)Reply

Tangazo

hariri
Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 17:32, 5 Aprili 2020 (UTC)Reply

Hemp

hariri

Naomba uangalie makala ya Hemp, pamoja na katani. Hemp imeletwa sasa na mgeni; kwa Kiingereza kuna makala tofauti kwa en:Cannabis na en:Hemp. Makala yetu ya katani ilianzishwa na kijana ambaye alichangya na mkonge. Kamusi ya Mada ya 1905 (kabla ya kusambaa kwa mkonge) inasema "*Katani, n. also Kitani, flax, and what is made from it, linen, string, strong thread, twine. Uzi wa k, thread made of flax or hemp, as dist. from uzi wa pamba, cotton thread. (Ar. Cf. uzi, ugwe, kigwe, kamba.)" So should we have mkatani as separate entry (now wrongly redirect) - but then it is not clear to me if it is flax or hemp? Kipala (majadiliano) 05:19, 3 Julai 2020 (UTC)Reply

Kipala salaam. Nadhani mchangiaji wa Hemp alitaka kuandika kuhusu aina za bangi zinazokuzwa ili kuzalisha nyuzi. Hiyo ni sawa kwangu, lakini anapaswa kutumia jina la Kiswahili. Nilipendekeza mbangi-mwitu kama tafsiri ya Cannabis sativa, lakini labda jina hili si zuri sana. Nitafikiria tena na kwa wakati huu niko wazi kwa maoni.
Suala la katani / kitani ni utata. Nadhani ni kweli neno moja, lakini siwezi kujua ni gani iliyokuja kwanza. Sina hakika kama ka- / ki- ni viambishi. Kwa hali yoyote, kuna majina kiasi ya mimea ya Kiswahili ambayo huanza na mki-, kwa hivyo mkatani na mkitani yangekuwa majina yanayokubalika. Nadharia tete yangu ni kwamba neno hilo lilitumiwa hapo awali kwa nyuzi za mimea kwa jumla, ingawa sijapata ushahidi madhubuti kwa hilo. Kwa vyovyote vile, utafiti wangu wa kwanza ulikuja na katani kwa hemp (mara nyingi sisal hemp lakini cannabis hemp pia) na kitani kwa flax. Leo nilichambua idadi kadhaa ya sentensi za Kiswahili zilizo na mojawapo la maneno haya. Isipokuwa visa vichache sana, katani ilitumika kwa hemp (pamoja na sisal tena) na kitani kwa flax. Kwa hivyo, tunaenda wapi kutoka hapa? Tunaweza kukubali kuwa katani hutumiwa kwa hemp na sisal pamoja au tunape kipaumbele matumizi yake kwa sisal na tunapendelea aina ya bangi kwa hemp. Unafikiria nini? ChriKo (majadiliano) 16:45, 3 Julai 2020 (UTC)Reply
Kamusi ya Krapf, aliyekusanya maneno yake pale Mombasa (Kivita) ana hii: "KITANI, s., flax, linen;"
Ukiangalia hapa: mwongozo wa serikali ya TZ kwa ghala za korosho unatumia istilahi hivyo: "Korosho ghafi zimefungashwa kwenye gunia ya kitani(jute) au katani(sisal)".
Kamusi Kuu (BAKITA) inaeleza Katani kama kisawe cha mkonge, pia kama kamba, haina Kitani
Tuki Kisw-Kiing.: katani nm [i/zi-] hemp, sisal fibre.; robota* nm ma- [li-/ya-] bale: ~ la katani sisal bale. -- kitani nm vi- [ki-/vi-] linen, flax, duck
Kamusi Teule: kitani nm [ki-vi] nguo, kipande cha nguo, jora
Nimeangalia pia kamusi za Velten (1910), wakati Mkonge ulikuwa bado mmea mmpya. Natuma kopi kwako kwa baruapepe. Inaonekana hata kwake (nadhani alikusanya mengi pale Tanga) kitani na katani ni kama visawe, kiasili ni flax/hemp, lakini nyuzi zilizosafishwa ziliitwa "katani/kitani" bila kujali mmea gani. Hii inafanana na Kijerumani ambako zamani "Sisalhanf" ilikuwa kawaida (does NL not have "sisalhennep"?). Kwa hiyo walianza kuchanya maana hata siku zile.
Naona sasa pia interwiki imechanganywa katika swwiki kwa mkonge na katani. Kipala (majadiliano) 22:43, 3 Julai 2020 (UTC)Reply
Kumbe, jute pia? Nilitafuta kwenye internet na ni kweli. Sasa tutafanyaje? Tutumie kitani kwa flax na jute na katani kwa sisal na hemp? ChriKo (majadiliano) 16:45, 4 Julai 2020 (UTC)Reply

We sent you an e-mail

hariri

Hello ChriKo,

Really sorry for the inconvenience. This is a gentle note to request that you check your email. We sent you a message titled "The Community Insights survey is coming!". If you have questions, email surveys@wikimedia.org.

You can see my explanation here.

MediaWiki message delivery (majadiliano) 18:54, 25 Septemba 2020 (UTC)Reply

Fumbatio

hariri

Ndugu, vipi Kenya? Samahani, KKK na KK21 zinaweka fumbatio katika ngeli li/ya. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:56, 17 Oktoba 2020 (UTC)Reply

Jambo, Kenya ni poa. Nilifuata TUKI ambayo inasema ngeli ya fumbatio ni n-. Lakini nimeona sasa kwamba li/ma ni kawaida. Asante. ChriKo (majadiliano) 13:31, 17 Oktoba 2020 (UTC)Reply

Mtama

hariri

Ndugu, katika List of articles every Wikipedia should have, wameondoa Sorghum na kuweka badala yake Sorghum bicolor. Makala yetu imechanganya aina zote. Nakuomba utenganishe aina hiyo ili twende sawa na wenzetu. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:37, 8 Februari 2021 (UTC)Reply

Asante ndugu kwa ujumbe wako. Niliangalia ukurasa wa mtama, lakini ni kuhusu Sorghum bicolor tu. Ama kuna ukurasa mwingine tena? ChriKo (majadiliano) 12:45, 8 Februari 2021 (UTC)Reply
Nimefuatilia historia ya ukurasa: Kipala aliuanzisha kuhusu mtama aina zote, baadaye wewe uliufanya uhusu zaidi bicolor. Sasa napendekeza tutenganishe, la sivyo tubadilishe link. Asante. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:05, 8 Februari 2021 (UTC)Reply
Basi, nikielewa vizuri unataka makala mbili tofauti, moja kuhusu Sorghum na moja kuhusu Sorghum bicolor? ChriKo (majadiliano) 08:27, 9 Februari 2021 (UTC)Reply
Walau mbili, kwa sababu mimi mwenyewe nililima mtama (millet, sorghum) na najua kuna aina nyingi: serena, ferefere, mzumai, ulezi, mawele, wimbi n.k. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:53, 9 Februari 2021 (UTC)Reply
Sawa, nimepata sasa. Serena na ferefere ni aina za mtama, lakini maelezo yao sinayo na siyaoni kwenye mtandao. Lakini makala za mzumai, ulezi, mawele na mwimbi zipo. ChriKo (majadiliano) 15:58, 9 Februari 2021 (UTC)Reply

Makala za viumbe hai

hariri

Nashukuru sana kwa msaada kuhusu makala za viumbe hai. Mimi ni mwanabiolojia/bioteknolojia niliyebobea zaidi kwenye kilimo, hivyo nina ujuzi kwenye mimea zaidi na wadudu kwa kiasi. Kwa sasa ninatafsiri makala hii List of Orchidaceae genera kwenda Orodha ya jenasi za Orchidaceae. Swali la kwanza, kuna sehemu nakuta jina la jenasi linafuatiliwa na jina lingine (common name) kwa kingereza, nimetoa common names zote kwenye makala ya kiswahili kwa kuhofia kunaweza kua na common name nyinginge ambayo tunaita sisi. Hili ni sawa?

mnyama mbuai?

hariri

Habari, naona uliingiza lugha mnyama mbuai katika makala ya duma. Je maana yake ni nini? Umeikuta wapi? Kipala (majadiliano) 22:29, 30 Agosti 2021 (UTC)Reply

Ni mnyamapori, hasa akishambulia wengine. Tazama KKK. Amani kwa wote wawili! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:03, 31 Agosti 2021 (UTC)Reply
Habari zenu? Maana ya mbuai ni "predator". Mawindo yake huitwa mbuawa. ChriKo (majadiliano) 20:39, 31 Agosti 2021 (UTC)Reply

Wariomiller40

hariri

Hi! I see that you commented on Cherish Perrywinkle. I think that you should be aware that the user who created it is a long-term crosswiki vandal, see en:Wikipedia:Sockpuppet investigations/Angelmunoz50/Archive and [3]. Typical edits include translating articles about killed children but changing important information like age, years and cause of death. I couldn't find the Administrators noticeboard here so I take the liberty of contacting you on your talk page. Sjö (majadiliano) 09:02, 14 Novemba 2021 (UTC)Reply

Hi Sjö. Thanks for the information. I shall discuss with the other admins how to deal with this person. ChriKo (majadiliano) 17:04, 14 Novemba 2021 (UTC)Reply

How we will see unregistered users

hariri

Hi!

You get this message because you are an admin on a Wikimedia wiki.

When someone edits a Wikimedia wiki without being logged in today, we show their IP address. As you may already know, we will not be able to do this in the future. This is a decision by the Wikimedia Foundation Legal department, because norms and regulations for privacy online have changed.

Instead of the IP we will show a masked identity. You as an admin will still be able to access the IP. There will also be a new user right for those who need to see the full IPs of unregistered users to fight vandalism, harassment and spam without being admins. Patrollers will also see part of the IP even without this user right. We are also working on better tools to help.

If you have not seen it before, you can read more on Meta. If you want to make sure you don’t miss technical changes on the Wikimedia wikis, you can subscribe to the weekly technical newsletter.

We have two suggested ways this identity could work. We would appreciate your feedback on which way you think would work best for you and your wiki, now and in the future. You can let us know on the talk page. You can write in your language. The suggestions were posted in October and we will decide after 17 January.

Thank you. /Johan (WMF)

18:19, 4 Januari 2022 (UTC)

Have you voted in the UCoC enforcement guidelines ratification?

hariri

Hi! @ChriKo:

The ratification voting process for the revised enforcement guidelines of the Universal Code of Conduct (UCoC) is now open! Voting commenced on SecurePoll on 7 March 2022 and will conclude on 21 March 2022. Please read more on the voter information and eligibility details.

Please vote and encourage other editors of Swahili Wikipedia to also vote.

Regards,

Stefania Turkewich

hariri

Hello ChriKo, I've entered the article into the languages, into the list with the other languages of this article. Thank you so much for this! Nicola Mitchell (majadiliano) 19:29, 24 Juni 2022 (UTC)Reply

If you can keep what I've added, you might want to check my language. Thank you for all your help with this article! Nicola Mitchell (majadiliano) 10:47, 25 Juni 2022 (UTC)Reply

Jina la makala Kumguni-maji mtambaazi

hariri

Habari ChriKo, heri ya mwaka mpya.

Hongera kwa makala nzuri pia ya kunguni-maji mtaambaaji. Nimeona kwenye jina la makala umeandika kungumi, je ni sawa au ni kunguni? Sikumbuki namna ya kubadilisha jina la makala hivyo nikaandika hapa.

Wako, Asterlegorch367 (majadiliano) 10:38, 3 Januari 2023 (UTC)Reply

Jambo Aneth. Kwako heri ya mwaka mpya pia. Asante kwa ujumbe wako. Jina limesharekebishwa. Wako, ChriKo (majadiliano) 20:20, 3 Januari 2023 (UTC)Reply