Noti ya benki : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa umeelekezwa kwenda Benknoti
 
Removed redirect to Benknoti
Tag: Removed redirect
Mstari 1:
[[Picha:Jiao_zi.jpg|thumb|300px|Karatasi ya pesa ya kwanza kutoka China]]
#REDIRECT [[Benknoti]]
 
'''Noti ya benki''', kifupi '''noti''', ''(kutoka Kiingereza "banknote")'' kwa kawaida ni kipande cha [[karatasi]] (pia: [[plastiki]]) kinachochapishwa na kuonyesha namba fulani na jina la [[pesa]] ya nchi fulani. Inakubaliwa kama njia ya malipo halali- Pamoja na [[sarafu]] ni [[pesa taslim]] ya nchi fulani.
 
Kwa kawaida vipande vya [[sarafu]] au pesa taslim metalia huwa na viwango vidogo zaidi na noti huwa na viwango vikubwa zaidi.
 
== Usalama wa noti za benki ==
Tangu kutolewa kwa noti wahalifu walijaribu kutengeneza noti bandia wakiiga zile zinazotolewa na benki rasmi. Kwa sababu hiyo benki kuu na serikali zinajitahidi kutoa noti ambazo ni vigumu kuiga. Hapa wanatumia karatasi za pekee zisizopatikana madukani, wanachapisha kwa rangi zisizosomeka na mashine ya fotokopi, wanaingiza nyuzi za metali ndani ya karatasi na kadhalika.
 
Tangu mwisho wa karne ya 20 nchi kadhaa zimeanza kutoa noti za plastiki badala ya karatasi. Hizi zina gharama kubwa zaidi ya kuzitengeneza lakini hadi sasa usalama ni kubwa zaidi ni vigumu sana za kuiga pia hazichakai haraka kama vile noti za karatasi.
 
== Historia ya noti za benki ==
 
Chanzo cha historia ya noti za benki ni barua zinazoahidi kulipa kiasi fulani cha pesa kwa mtu yeyote anayeshika barua ile. Kwa hiyo noti zilikuwa sawa na [[hundi]] za leo.
 
=== Barua badala ya sarafu nzito ===
Kiasili vipande vya [[metali adili]] kama [[dhahabu]] au [[fedha]] vilitumiwa kama pesa vikipimwa kuwa na uzito fulani kwa mfano "pound" ya Uingereza ilikuwa sawa na uzito wa "pauni" au [[ratili]] moja ya fedha.
 
Wakati uchumi uliongezeka watu walianza kutumia viasi vikubwa vya pesa na hii ilikuwa kazi ngumu kutokana na uzito wa sarafu nyingi. Hapo wafanyabiashara waliacha sarafu zao kwa mtu aliyeaminiwa na kushika barua kutoka kwake iliyothebitisha ya kwamba alishika kiasi fulani kwa niaba ya mwingine. Pale ambako watu waliaminiana waliweza kutumia barua hizi kama malipo badala ya sarafu yenyewe.
 
=== China ===
Serikali ya kwanza ya kutoa pesa ya karatasi ilikuwa [[nasaba ya Song]] nchini [[China]] mnamo mwaka [[960]]. Noti hizi zilikuwa na maandishi zilizomwahidi mwenye kuishika ya kwamba atapewa kiasi fulani cha fedha akiipeleka noti za benki kwa idara ya fedha ya serikali. Kimsingi hii ilibaki muundo wa noti hadi karne ya 20 yaani zilikuwa ahadi za serikali au za benki kubwa kumpatia mwenye noti kiasi fulani cha dhahabu au fedha.
 
Tatizo la pesa ya karatasai tangu mwanzo ilikuwa ya kwamba serikali yenye matatizo iliweza kuendelea kuchapisha noti mpya kata kama haikuwa na dhahabu au fedha ya kutosha. Hii haikuwa tatizo mara moja kwa sababu hali halisi noti zilifanya kazi zao kama thamani ya noti zote ililingana na thamani ya bidhaa zilizopatikana katika nchi fulani. Lakini kama serikali iliendelea kuchapisha pesa hovyo watu walianza kuona ya kwamba pesa haina thamani tena na bei zilianza kupanda haraka sana.
 
=== Ulaya ===
Katika Ulaya pesa ya karatasi ya kwanza iliyotolewa na serikali au kwa niaba ya serikali ilianza kupatikana tangu karne 16 katika [[Uholanzi]] na [[Ufaransa]]. Mara kwa mara majaribio haya ya kwanza yalivurugika kutokana na kuchapisha noti nyingi mno na kushuka kwa thamani ya pesa hii.
 
Noti za benki zilianza kuwa kawaida hata kwa watu wa kawaida wakati wa karne ya 19. Mwanzoni [[benki kuu]] ya kila nchi kisheria ilipaswa kuwa na akiba ya dhahabu au fedha iliyolingana ama na noti zote au angalau na sehemu kubwa zao. Masharti haya yalifutwa polepole kwa sababu ilionekana ya kwamba kama kiasi cha noti haizidi thamani ya bidhaa nchini uchumi unaendelea bila mvurugo. Tena baada ya kupatikana kwa mawasiliano ya kisasa kama simu na intaneti kiasi kikubwa cha ahadi za kulipana inazunguka katika uchumi na hizi ahadi zinafanya kazi kama pesa hata kama si pesa taslim.
 
== Viungo vya Nje ==
;Picha za benknoti za dunia
* [http://www.banknoteworld.com/ Ron Wise's Banknote World]
* [http://www.worldpapermoney.org worldpapermoney.org Online World Paper Money Museum]
* [http://www.banknotewiki.com/ Bank Note Wiki - A collectors wiki that any user can edit]
* [http://numismondo.com Numismondo - World Paper Money Picture Catalog]
* [http://public.fotki.com/sanmiguel/world_banknotes/ Gallery describing who/what is featured on modern world banknotes]
* [http://www.bank-note.ru World Banknotes issued since 1961 illustrated catalogue]
 
;Benknoti za plastiki
* [http://www.polymernotes.org Polymer Bank Notes of the World]
* [http://www.polymernotes.de Polymer Bank Notes in German by Thomas Krause]
 
;Vyama vya watu wanaokusanya aina nyingi za benknoti
* [http://www.banknotebank.com/ Banknotebank.com]
* [http://www.theibns.org/ International Bank Note Society]
* [http://www.apnaonline.ca/ Atlantic Provinces Numismatic Association]
 
;Wachapishaji
* [http://www.bep.treas.gov/ US Bureau of Engraving and Printing]
* [http://www.noteprinting.com/ Note Printing Australia]
* [http://abncompany.com/ American Bank Note Company]
* [http://www.cbnco.com/ Canadian Bank Note Company Ltd]
* [http://www.gi-de.com/ Giesecke & Devrient]
* [http://www.delarue.com/ Thomas de la Rue]
* [http://www.oberthur.com/ François-Charles Oberthur]
 
{{wiktionary}}
 
[[Jamii:Pesa]]