Nzige-jangwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{Uainishaji | rangi = pink | jina = Nzige-jangwa | picha = Copulating desert locust pair.jpg | upana_wa_picha = 250px | maelezo_ya_picha = Jike na dume ya nzig...'
 
Nyongeza picha
Mstari 25:
Kisha jike hutafuta udongo laini unaofaa kwa kutaga mayai yake. Lazima uwe na joto sahihi na kiwango kizuri cha unyevu na kuwa karibu na majike wengine wanaotaga. Anachunguza mchanga kwa fumbatio yake na kuchimba kishimo ambacho ndani chake anaweka kibumba cha mayai kilicho na mayai hadi mia moja. Kibumba cha mayai kina urefu wa sm 3 hadi 4 (inchi 1.2-1.6) na ncha ya chini ni takriban sm 10 (inchi 4) chini ya uso wa ardhi. Mayai yamezungukwa na povu na hii inakauka mpaka kuwa utando na kuziba kishimo juu ya kibumba cha mayai. Mayai huchukua unyevu kutoka kwa mchanga unaozunguka. Kipindi cha kuatamia kabla ya kujiangua kwa mayai kinaweza kuwa wiki mbili au zaidi sana, kulingana na nyuzijoto.
 
[[Picha:S. gregaria dense hopper band.jpg|thumb|left|Kundi zito la tunutu nchini Sudani]]
Baada ya kutoka kwenye yai tunutu mpya huanza kujilisha punde si punde na, ikiwa ana awamu ya kukaa pamoja na wenzake, anavutiwa na tunutu wengine na wanajikusanya. Wakati wa ukuaji anahitaji kuambua [[ngozi]] (kuacha [[kiunzi-nje]] chake) mara kwa mara. [[Ganda]] lake gumu la nje linapasuka na mwili wake unatanuka wakati kiunzi-nje kipya bado ni chororo. Hatua kati ya [[uambuaji|maambuaji]] zinaitwa “instars” na tunutu wa nzige-jangwa hupitia maambuaji matano kabla ya kuwa mpevu mwenye mabawa. Tunutu wa awamu ya kukaa pamoja huunda makundi yanayojilisha, kukota jua na kusonga mbele katika vikosi vinavyoshikamana, wakati wale wa awamu ya kutokaa pamoja hawaundi makundi.