Mataifa ya Kati : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
(Hakuna tofauti)

Pitio la 21:55, 27 Juni 2020


Mataifa ya Kati yalikuwa ushirikiano wa nchi zilizoshikamana katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia dhidi ya Mataifa ya Ushirikiano. Nchi hizo zilikuwa Ujerumani, Austria-Hungaria, Milki ya Osmani (baadaye Uturuki) na Bulgaria.

Mataifa ya Kati (Central Powers (nyekundu)) na wapinzani wao katika Ulaya wakati wa Vita Kuu ya Kwanza

Nchi hizo zilipigana dhidi ya Ufaransa, Uingereza, Ubelgiji, Ureno, Serbia, Urusi na Italia. Tangu mwaka 1917 Urusi ilitoka katika vita lakini Marekani na nchi mbalimbali zilingia upande wa ushirikiano, mfano Najd (baadaye Saudia), Japani, na nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini.

Mataifa ya Kati yalishindwa; tokeo la vita lilikuwa mwisho wa Dola la Osmani na milki ya Austria-Hungaria, pamoja na kutokea kwa idadi ya nchi mpya katika Ulaya ya Mashariki (Poland, Chekoslovakia, Kroatia), na kukabidhiwa kwa koloni za Ujerumani (pamoja na Tanganyika, Rwanda, Burundi) kwa nchi nyingine kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa.


[[Jamii:Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia]]