Asilimia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: '''Asilimia''' ni njia ya kutaja uhusiano kati ya viasi viwili. Alama yake ni '''<big>%</big>'''. Kiasi kimoja huteuliwa kuwa ni namba ya 100 ya kiasi kingine. Sehemu yake ya mia ni 1 %. ...
(Hakuna tofauti)

Pitio la 22:45, 5 Machi 2008

Asilimia ni njia ya kutaja uhusiano kati ya viasi viwili. Alama yake ni %. Kiasi kimoja huteuliwa kuwa ni namba ya 100 ya kiasi kingine. Sehemu yake ya mia ni 1 %.

Sasa inawezekana kugawa kiasi kingine kwa ile 1% na kuona inashika asilimia ngapi za kiasi husianifu.

Mfano

Mfano: Jumla ya maksi kwenye mtihani ni 250. Sheria inasema ya kwamba 65 % ni sharti kwa kupita. Je maksi ngapi zinahitajika ila kupita mtihani huu?

Jibu: Jumla ni 250 hivyo 250 zachukuliwa kama asilimia mia moja. Sehemu ya mia moja yaani 1 % ni 2.5. Asilimia 65 ni 2.5 zidisha 65 jumla 162.5. Maana yake kuanzia maksi zisizopungua 163 mwanafunzi amepita.

Sehemu na asilimia

Kuna viwango kadhaa za sehemu zinazokumbukwa kirahisi kwa asilimia:

Nusu = 50% robo = 25% robo tatu = 75% humusi = 20% theluthi = 33%